SACCOS ya Bumbuli Dev ya Januari Makamba yadaiwa kutafuna bil 2 za NSSF

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,934
3,228
Hii Saccos ya Bumbuli Development Corporation ipo Jimboni Bumbuli kwa Marope mdogo au ni ya wapi?

Ndani ya Mwaka mmoja wamelamba 2.4 billion mikopo ya NSSF kinyume na kanuni

Ama Kweli NSSF wametafuna..

Kumbe ndo maana hawataki kulipa FAO la KUJITOA

Haki za Wanyonge zinatafunwa sana na wakubwa

Viongozi wa Tanzania hawana huruma
 
Soma kwa makini hizi habari kuhusu mabilioni yanavyotafunwa NSSF

Ndio maana wanakwepa kulipa FAO LA KUJITOA..

Wafanyakazi msilale

TUCTA iko wapi uuwii

Lazima hawa mafisadi watakuwa wamewapa Viongozi wa TUCTA rushwa ili kuwaparalyse
 
Mpaka Sasa PPF na NSSF wanalipa FAO LA KUJITOA?

Au wanangoja Sheria ipite?
 
Bumbuli? Si jimbo LA January hilo??? Ohooooo kumbe zile Saccoss zilikua zinatumika kulipa wapiga kura?? Chadema walishinda kule Aiseee. Wale wasambaa watakapoona huu uozo hahahahaha watawakata mapanga
 
Tuhuma alizozitoa Musiba kupitia kwa waandishi wa habari kuwa ulikopa hela zetu za wachangiaji wa mifuko ya jamii na kwamba sasa hutaki kurudisha ni nzito sana

Tuhuma hizi zinatuuma sana na hasa ukizingatia kuna watu hatujalipwa kwa miezi nane na zaidi,
Sasa tunakushauri na kukuomba ufanye mambo mawili yafuatayo;

1. Utoe ufanunuzi au
2. Umpeleke mahakamani mhusika vinginevyo shida na maumivu tunayopata kusubiri mafao yetu tutajua yanasababishwa na wewe na wenzako wengine

Tunadhani ukifanya hivi ndani ya wiki ijayo itapunguza maumivu yetu, asante
 
Tuhuma alizozitoa musiba kupitia kwa waandishi wa habari kuwa ulikopa hela zetu za wachangiaji wa mifuko ya jamii na kwamba sasa hutaki kurudisha ni nzito sana...
Ningekua January siwezi kujibu huo upupu.....walio mkopesha au walio pewa dhamana yakusimamia hiyo mifuko ya jamii ndo waajibike sio mkopaji kwasababu hawezi kujikopesha mwenyewe
 
Tuhuma alizozitoa musiba kupitia kwa waandishi wa habari kuwa ulikopa hela zetu za wachangiaji wa mifuko ya jamii na kwamba sasa hutaki kurudisha ni nzito sana...
Katika hii thread kuna mambo mawili nimeyaona au makundi mawili nimeyaona.

1.Kundi la kwanza litamuona musiba hana maana anadhalilisha watu hili ndo kundi ambalo lipo kumtetea january makamba.

2.Kundi la pili linamuona musiba anachoongea kina mantiki.

Lakini tutazunguka kote hoja kuu ni pesa alizochukua makamba katika mifuko ya jamii ni kweli au sio kweli hiyo ndo hoja ya msingi.

Kama ni kweli basi alipe helaa tuu za watu hayo kama sio kweli basi ajibu
 
Ningekua January siwezi kujibu huo upupu.....walio mkopesha au walio pewa dhamana yakusimamia hiyo mifuko ya jamii ndo waajibike sio mkopaji kwasababu hawezi kujikopesha mwenyewe
Nilitaka kuchangia hili.
Yaani ni kope mimi mwingine aje aseme kwanini nimekopa. Kama kuna suala la kuhoji kwanini asihojiwe mkopeshaji?
Ningekua JM ni kukaa kimya tu.
 
Kama alikopeshwa maana yake alikuwa anakopesheka na kuna dhamana aliweka
 
Back
Top Bottom