Sabodo amgeuka Butiku, amsifu Mtei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabodo amgeuka Butiku, amsifu Mtei

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Dec 24, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MFANYABIASHARA maarufu nchini Jaffar Sabodo amehoji matumizi katika taasisi ya Mwalimu Nyerere na kuitaka itoe mchanganuo wa Sh1bilioni alizoichangia taasisi hiyo mwaka jana.

  Katika tangazo lake alilotoa jana kupitia vyombo vya habari, Sabodo alitaka kueleza namna ilivyotumia Sh 1bilioni aliyotoa wakati wa mchezo wa bahati nasibu ulioendeshwa na taasisi hiyo.

  Pia ameitaka ieleze mafanikio yake tangu ilipoanzishwa.

  Katika tangazo hilo alilotoa kuulezea utawala wa rais Jakaya Kikwete miaka minne tangu aingie madarakani, Sabodo ameitaka taasisi hiyo kueleza matumizi ya taasisi hiyo kwanza kabla ya kumshutumu rais Kikwete.

  “Kupitia mchezo wa bahati nasibu ulionzishwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere nilichangia Sh1 bilioni lakini kutokana na mapungufu makubwa ya mfuko huo imeshindwa hata kufikisha Sh200 milioni kwa kuuza bidhaa mbalimbali katika bahati nasibu hiyo," alisema Sabodo katika taarifa hiyo na kuongeza:

  "Mbali na mimi, watu wengi pia wamechangia katika mfuko huo. Fedha zote walizochangiwa zipo wapi?, waseme walichofanya, waseme walichopoteza?".

  Maelezo ya Sabado yanafuatia kuwepo na ongezeko kubwa la watu kutoka ndani ya CCM ambao wamejitokeza hadharani na kumkosoa Rais Kikwete kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu, hasa dhidi ya mafisadi huku wengine wakikiona chama hicho kikipoteza mwelekeo na kuachana na wakulima na wafanyakazi.
  Miongoni mwa watu hao ni mawaziri wa zamani, Mussa Nkangaa na Matheo Qares ambaye alidiriki kusema kuwa iwapo Kikwete atashindwa kufanya maamuzi magumu ifikapo 2010, basi CCM isimteue kugombea urais. Kikwete alijibu kuwa hashangazwi na maneno ya watu hao, lakini akasema kuwa atakaa na wenzake, ambao hakuwataja, kuandaa majibu.

  Katika tangazo hilo Sabodo anaona kuwa sasa ni wakati wa taasisi hiyo kueleza imetoa mchango gani kwa watanzania.
  “Aidha, wao waeleze walichofanya wakati walipokuwa katika nafasi nyeti za utawala, na si kuulaumu utawala wa sasa”. Imesema taarifa hiyo

  Sabodo, mmoja wa watu muhimu katika historia ya nchin hii, anaona kwamba Rais Kikwete atakubukwa na taifa la Tanzania kama atafanya mapinduzi ya kweli katika kilimo. “Hivyo ninamshauri rais kuunda Shirikisho la Umoja kama walivyofanya nchini Sweden. Namuomba muheshimiwa Kikwete ainge mfano kama wa aliyekuwa rais wa Marekani Goerge Washington na Nehru wa India ambao walifanya mapinduzi ya kweli ya kilimo katika nchi zao.”

  Akizungumza na Mwananchi jana kwa njia ya simu, mkurungezi wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema; “ Nenda kwa huyo huyo Sabodo akupe Clarification (maelezo) zaidi ya hayo aliyosema. Mimi siwezi kujibu kitu ambacho sikijui, sina la zaidi akakata simu.”


  Pia kupitia tangazo hilo Sabodo anadai
  Edwin Mtei ambaye alikuwa ni gavana na pia Waziri wa Fedha ndiye aliyemshauri hayati Mwalimu Julius Nyerere kupunguza thamani ya fedha kwa asilimia 20 lakini Mwalimu alipingana na ushauri huo. Wakati huo thamani ya fedha ya Tanzania ilikuwa kati ya Sh 14 na 15 kwa dola moja ya kimarekani.
  “Na kuanzia hapo ndio thamani ya fedha ya Tanzania ilianza kushuka,”ilisema taarifa hiyo.

  “Ni bora nimpende mtu ambaye si mwaminifu lakini anatimiza wajibu wake kwa kufanya mambo mazuri na yenye manufaa kuliko kumpenda mwaminifu ambaye hawezi kutimiza wajibu,”

  Sabodo alisema mwalimu alikuwa ni mtu muelewa, mwenye kujali na aliyetumia maisha yake kwa ajili ya kuwatumikia watu na wala hakuwa mchumi.

  Kama rais Kikwete ataweka mpango madhubuti wa kuhakikisha thamani ya fedha ya Tanzania inakuwa, uchumi utakuwa kwa kasi. Mfano ni nchi za Mauritius, Singapore na Thailand. Kulinda na kukutza thamani ya fedha ndio inayohitajika sasa na si vinginevyo.
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Who is Sabodo?alipo anzisha bahati nasibu kuchangia taasisi hiyo nilidhani ni mhusika kumbe?..
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ndio kwa mara kwanza nasikia kuna mtu muhimu katika historia ya nchi hii eti anaitwa Sabodo.

  Mwongo mkubwa, mpaka anang'atuka Mwalimu thamani ya dola ilikuwa chini ya sh 8 kwa dola. Katika hii safisha safisha kabla ya 2010, tutashuhudia mengi na huyo Sabodo labda ni zao la ufisadi.
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  HABARINDIYOHIYO


  Exchange rates hapa chini mazee

  Year Gross Domestic Product US Dollar Exchange

  1980 45,749 8.21 Shillings

  1985 115,006 17.87 Shillings

  1990 830,693 195.04 Shillings

  1995 3,020,501 536.40 Shillings

  2000 7,267,133 800.43 Shillings


  2005 13,713,477 1,127.10 Shillings
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Niliposikia kuna mfanyabiashara anaitwa Sabodo alichangia Bilioni 1 mfuko wa Bahati Nasibu ya Mwalimu ndipo nilipoanza kujiuliza...Huyu Sabodo ni nani mpaka leo sijapata jibu.

  Zaidi ya kuambiwa ni mfanyabiashara na "mtu muhimu" kwenye historia ya nchi naombeni wanaojua historia na wasifu wake wanielimishe yeye ni nani na biashara gani anafanya n.k
   
 6. e

  echonza Senior Member

  #6
  Dec 25, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aondoke zake huko. Itakuwaje mimi nimpe rafiki yangu au ndugu yangu msaada fulani falagha halafu kesho yake nakuja kuropoka publically eti nahoji jinsi zilivyotumika. Hawa ndiyo mafisadi wenye lengo la kujionyesha kwa watu, na yawezekana ana nia ya kwenda kugombea ndiyo maana kajitokeza kwa mgongo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere ili imbebe!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  HIvi.. wanaogopa sana Kikwete kutokugombea tena?
   
 8. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyu ni mfanya biashara maarufu, huichangia sana sisiem ila bahati mbaya hakupata cheo kama akina R.A! Ndo maana ameanza kupiga kelele, ooh pesa yangu imeibiwa..ooh...
  Kwani wewe ukishatoa mchango kwenye taasisi yenye wahasibu na inayokaguliwa na CAG, unaweza kuulizia hela zako ziliko?
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Ndie mwenye ekia complex na mwl nyerere movie thiettre pale mwenge...wanadai alikuwa ni best ya JKN na mfuasi wake mkubwa wa siasa na fikra za nwl!!
   
 10. k

  kitita Member

  #10
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii aina maana yeyote sasa. Ukweli ni kwamba Panapo matumizi mabaya pamulikwe. Na wahusika wawajibike. Hii tabia ya kiswahili ya kulumba ni ya fikra dhaifu. Jibu swali na siyo kurusha swali kujibu swali.
  Watanzania sio mbumbumbu wazungu wa reli. Msema kweli atatunzwa.
   
 11. k

  kitita Member

  #11
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kushuka kwa thamani ya fedha kunawiana na rushwa...
  Nchi inapokuwa na rushwa na siasa ya udanganyifu inayoliibia taifa rasilimali za dhahabu, almasi, na kadhalika, basi nchi hiyo huwa haina akiba ya taifa
  Hii ina maana nchi hupata madeni na fedha hulazimishwa kushuka thamani. Uchomaji wa benki kuu ni mfano mmoja wapo wa wizi wa mamilioni ya dola...na huchangia kuangusha shilingi yetu.
  Unapokuwa na upungufu wa dola, basi wewe hela yaku inapungua thamani....
  Viongozi wabebe dhamana hela inaposhuka thamani hata wakenya wana hela yenye nguvu kwa kuuza nyanya za Manyara....
   
 12. k

  kitita Member

  #12
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Echonza,
  Ni kwanini Tanzania ni maskini wakati tuna amani na rasilimali mbalimbali kuliko nchi nyingi za Afrika.
  Good governance requires OPEN government and not cheap talk. Sabodo asked and you should expect an answer...not a question.
  Nionyeshe vyama vya siasa vya ulaya vinavyomiliki magari, majengo, viwanja vya mpira na kadhalika....huu ni ujinga wa kisiasa nchi maskini hufanya.
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Unaongelea nini ? Mie am lost jamani nisaidieni kuelewa huyu Kitita anaongelea ama yeye mwenyewe afafanue .
   
 14. Offish

  Offish Senior Member

  #14
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JK should be the first to respond to questions raised by participants during the debate organised by Mwl Nyerere Foundation. It seems he's cunningly using his agents and the fault finding method to seek public sympathy. 'Chuki binafsi' is a lame excuse and the least expected from the President as a response to his critics, he owes the critics and the public at large some more explanation for embracing a foreigner such as RA et al to loot the country's resources...!

  JK seems good at using his agents for seeking public sympathy. Another example is the demolition of hotel constructed on a road reserve, already his agents are blaming Tanroads for the demolition on grounds that the parastatal had ashamed the President!

  The JK aides actually ought to ensure there was nothing wrong with the hotel before letting him go all the way to Arusha to officiate at the opening ceremony of the hotel? The President is supposed to protect the laws of the land, not to support those breaching the law. Tanroads, therefore, should not bear any blame for protecting the law.

  JK to me seems to be more comfortable when he is surrounded by sycophants such as Sabodo, Sheikh Yahaya, Augustine Mrema, etc than his critics, doesn't he?
   
 15. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Wahindi ndivyo walivyo hawakawii kugeuka kwenda kwenye masilahi,Sabodo anapenda kusujudiwa kisa pesa zake,kaona akina Butiku hawampigii magoti ndio maana kaamua kujilambisha kwa Kikwete,si ajabu katishiwa kuwa halipi kodi,janja ya nyani hiyo. kula hindi bichi bana
   
 16. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Hana lolote huyo hana hulka ya Ujamaa ni bepari wa kutupwa alimtumia mwalimu kwa kujikomba na kujifanya rafiki
   
Loading...