Sabaya Naye Aachiwe(Asamehewe)

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,907
4,771
Habari za Mchana.
Mimi pia naona makosa mengi ya Sabaya ni ya #kisiasa japo mashitaka ni ya #kisheria.
Makosa haya ya kisiasa yanasameheka. Sabaya hatakuwa wa kwanza kusamehewa na mama kwa kumshauri DPP kumfutia makosa yote yanayomkabili na kushawishi ashinde rufaa kwa kesi ambayo tayari amehukumiwa na amekata rufaa.

Naamini akisamehewa atakuwa na adamu, heshima, utii, uadilifu na kufuata sheria
Haya mambo yanawezekana.
Makosa haya yanasameheka.

Kama kutakuwa na mtu mwenye malalamiko basi akafungue kesi kama yeye na sio kusaidiwa na Jamhuri kwa kesi ambayo kwa Jamhuri inaonekana kabisa makosa ni ya kisiasa zaidi.
 
Ungekua DPP wewe ungefungulia wahaifu wengi sana warudi mtaani, na wengine wangerudi kumalizia kazi walizoziacha za kihalifu na kusababisha maafa zaidi
 
Kwanza huyo unae amini atasamehewa (sisi hatujaomba kusamehewa, bali tumemtaka afutiwe mashtaka) hajakosea popote na hilo shtaka alilopewa ni mchongo.
Pili tambua kwamba Mbowe hajaiba, hajanyang'anya, haja dhulumu (bali ameshtakiwa kwa kosa la ugaidi).
Hii ni tofauti na Lengai ambae ameumiza watu wengi kwa kuwanyang'anya, kuumiza/kunyanyasa wafanya biashara, ujambazi na kadhalika....
 
Habari za Mchana.
Mimi pia naona makosa mengi ya Sabaya ni ya #kisiasa japo mashitaka ni ya #kisheria.
Makosa haya ya kisiasa yanasameheka. Sabaya hatakuwa wa kwanza kusamehewa na mama kwa kumshauri DPP kumfutia makosa yote yanayomkabili na kushawishi ashinde rufaa kwa kesi ambayo tayari amehukumiwa na amekata rufaa.

Naamini akisamehewa atakuwa na adamu, heshima, utii, uadilifu na kufuata sheria
Haya mambo yanawezekana.
Makosa haya yanasameheka.

Kama kutakuwa na mtu mwenye malalamiko basi akafungue kesi kama yeye na sio kusaidiwa na Jamhuri kwa kesi ambayo kwa Jamhuri inaonekana kabisa makosa ni ya kisiasa zaidi.

Sabaya hakua mwanasiasa alikua mtumishi wa umma period kuna tofauti, aliingiaje kwenye siasa wakati offisi yake haimtaki hajiusishe na majukumu ya kisiasa bali kusaidia wananchi wote bila kubagua kabila, chama nk
 
Ungekua DPP wewe ungefungulia wahaifu wengi sana warudi mtaani, na wengine wangerudi kumalizia kazi walizoziacha za kihalifu na kusababisha maafa zaidi
Wezi wengi wa mali za umma wameachiwa kwa kile kilichoitwa Plea Bargain wakati wa JPM, wakati wa mama wengine wakaachiwa bure hata wenye tuhuma nzito za ugaidi(mashehe) na wale wa ESCROW na wengine wamerudishiwa hela zao.
 
Sasa kama ndiyo hivyo mitazamo ya wengi ilivyo basi ujue tunashida sana, hatuwezi kuwaachia kila watu wahalifu kwa mitazamo ya makosa ya kisiasa
 
Hata tukiwaachia wote wenye mashataka yenye harufu ya kisiasa. Watu waje mtaani waanze upya. Hata wale wenye makosa madogo madogo tuwaachie waje mtaani kuanza upya. Hata wenye makosa makubwa kama wale watoto wa Bunju waachiwe waje waanze upya.
 
Sawa mkuu
 
meota mheshimiwa raisi amewafutia wote kesiii .... Jamhuri haina mpango wa kuendelea na kesi hizo

hahaaa men go back to work

next weekend after this is Christmas
 
Hizi kesi ni mtu na mdogo wake, pipa na mfuniko wake. Wote wawili wasamehewe. Warudi mtaani au kwenye siasa lakini wawe na adamu na heshima kwa mama.
#SABAYA naye asamehewe.
Hakuna lisilosameheka. Hata Mungu tunamkosea mara kwa mara lkn mafundisho ya dini na imani vinatuambia tukiomba msamaha na kutubj, tunasamehewa.
Mama SSH, RJMT(PoURT), nakuomba umsamehe Sabaya.
 
Sabaya hakua mwanasiasa alikua mtumishi wa umma period kuna tofauti, aliingiaje kwenye siasa wakati offisi yake haimtaki hajiusishe na majukumu ya kisiasa bali kusaidia wananchi wote bila kubagua kabila, chama nk

..kama Magufuli alisamehe walawiti walionajisi watoto wa shule, na akawapokea Ikulu na kufanya nao mazungumzo na maombi, nauona uwezekano wa Sabaya naye kusamehewa.
 
Habari za Mchana.
Mimi pia naona makosa mengi ya Sabaya ni ya #kisiasa japo mashitaka ni ya #kisheria.
Makosa haya ya kisiasa yanasameheka. Sabaya hatakuwa wa kwanza kusamehewa na mama kwa kumshauri DPP kumfutia makosa yote yanayomkabili na kushawishi ashinde rufaa kwa kesi ambayo tayari amehukumiwa na amekata rufaa.

Naamini akisamehewa atakuwa na adamu, heshima, utii, uadilifu na kufuata sheria
Haya mambo yanawezekana.
Makosa haya yanasameheka.

Kama kutakuwa na mtu mwenye malalamiko basi akafungue kesi kama yeye na sio kusaidiwa na Jamhuri kwa kesi ambayo kwa Jamhuri inaonekana kabisa makosa ni ya kisiasa zaidi.
Wewe utakuwa ni jambazi mwenzake.

Kwa mtanzania mwema na mpenda amani hawezi kushangilia kuachiwa huru kwa jambazi katili kama Sabaya.
 
..kama Magufuli alisamehe walawiti walionajisi watoto wa shule, na akawapokea Ikulu na kufanya nao mazungumzo na maombi, nauona uwezekano wa Sabaya naye kusamehewa.

Sabaya makosa yake yapo wazi na yana ushahidi.. Msilinganishe kesi za kuzushiwa na kesi zenye ushahidi
 
Back
Top Bottom