Sababu zilohalalisha Sudan Kusini na kuharamisha Somalia kujiunga na EAC

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
eac-foul.png


Sharti la msingi katika mengi,la kujiunga na EAC ni Utawala bora na kuheshimu haki za binadamu.

South Sudan, baada kukosa sifa za msingi, alikubaliwa kujiunga na EAC baada ya ushawishi mkali kutoka kwa waasisi na hasa Tanzania iliopelekea kufumbiwa macho masharti mengi kwa ahadi kuwa hayo masharti yatatekelezwa hatua kwa hatua.

Somalia ambayo inasafiri bahari moja ila kwenye vyombo tofauti tu, maombi yake yalitupiliwa mbali hasa kutokana na shinikizo kutoka Kenya na Uganda. Kikwete alizidiwa nguvu(?)na kusalim amri.

Wachunguzi wa mambo wakiyatafakari na kuyaweka kwenye mizani, wanaona kuwa sababu zinzotolewa za kuminywa kwa Somalia kuwa mwanachama ni nyepesi mno. Wachunguzi wanafikiria kumpa uanachama Somalia ungeweza hata kupunguza uhasama na jirani yake Kenya ambayo ina raia wengi wenye asili ya Somalia. Lakini sababu kuu ni inayowanyima Somalia kupata uanachama ni Udini. Hili jambo ni baya sana na tena la aibu.

Inanikumbusha pia Serikali ya Tanzania inapowawekea mikwamo wakati Zanzibar inapotaka kuwa mwanachama halisi wa kujitegemea,bila ya kubaki kwenye kwapa ya Tanzania.

Serikali ya Zanzibar inahoji kuwa ilikuwa mwanzilishi wa EAC iliovunjika (?) na iliendelea kuwa hivyo ndani ya muungano na kulikuwa hakuna tatizo lolote.Iweje leo iwe tatizo? mbona Zanzibar inabaki kuwa mwanachama anayojitegemea wa "EA Challenge Cup ( Kagame)"

Zanzibar ilidai haki hiyo kutokana na ukweli kuwa mambo mengi yasiokuwa ya muungano yana jadiliwa ndani ya EAC, hivyo haipati uwakilishi stahiki. Kumbe kubanwa kule ni sawa na Somali na kwa sababu ambazo zinalingana?

Kwa vile South Sudan imeshindwa kabisa kutimiza masharti ya kuwa mwanachama, hatuoni sasa umefika wakati muafaka wa kuisimamisha uanachama mpaka hapo itakapoweza kutimiza masharti kikamilifu.

Tanzania ina nafasi kubwa ya kuzishawishi wanachama wengine, hasa tukitilia maanani kuwa Mwenyekiti wa EAC wakati huu ni Tanzania.
 
Hey dude you are boring. Udini udini udini you always act as victims. The only good thing about you folks YOU LIKE TO KILL AND HATE EACH OTHER IN THE NAME OF YOUR god AND YOU JUSTIFY IT.

Na utawasikia oh ISIS ni mmarekan bas marekan noma yani anamtumia dini na mungu wenu hadi mnchinjana na mungu wenu karidhia na kufyata. PATHETIC. PEOPLE. PATHETIC. FAITH
 
Hey dude you are boring. Udini udini udini you always act as victims. The only good thing about you folks YOU LIKE TO KILL AND HATE EACH OTHER IN THE NAME OF YOUR god AND YOU JUSTIFY IT.

Na utawasikia oh ISIS ni mmarekan bas marekan noma yani anamtumia dini na mungu wenu hadi mnchinjana na mungu wenu karidhia na kufyata. PATHETIC. PEOPLE. PATHETIC. FAITH
Na kuhurumia hujui usemalo. Mimi sijataja jina la dini yeyote, kama wewe unafikiria hivyo basi wewe ndio mdini tena sana kufikia hatua hata ya kutukana, lakini hata hivyo, YOU ARE LESS BORING.
LET ME TELLING YOU, KILLING IS KILLING, IT DOESN'T MATTER YOU KILL IN THE NAME OF YOUR THEOLOGICAL GOD OR LIVING GOD
 
Matukio ya mauaji na kukandamiza haki ya kuishi na uongozi bora uliotokea jana wakati Taifa hilo changa Duniani likijiandaa kusheherekea miaka mitano toka kuzaliwa limezidi kuipaka matope meusi nchi hiyo inayonuka damu ya binadamu.

Tayari nchi hiyo inatajwa kuwa nchi hatari zaidi kuishi duniani baada ya Syria. Kinchonigusa ni kuwa nchi hii ni mwanachama hai wa EAC na hivyo harufu ya matendo yake kihalifu na isiothamini uhai wa mtu imetapakaa na kulitia doa eneo zima la Afrika ya Mashariki.

Tanzania ndio Mwenyekiti wa EAC wakati huu ina kila wajibu wakuitisha mkutano wa dharura kujadili hali ya kisiasa nchini na usalama Sudan Kusini na kuangalia uwezekano wa kuisimamisha uwanachama . Ni aibu na fedheha kuikumbatia nchi hii isiojali uhai na usalama wa raia wake kuwa moja wa sahibu wao.

Kwa kuufumbia macho ukiukwaji mkubwa wa mkataba wa na masharti ya uanachama wa EAC, nchi nyengine wanachama watafuta nyao hizo na kutojali umuhimu wa kuziangalia haki hizo kutenedeka ipasavyo.

Nchi zitaamua kuvunja Katiba ya nchi zao, kuipinda demokrasia, kuvunja haki za binadamu, kutoheshimu maamuzi ya raiana kupora haki wapendavyo. HAPA KAZI TU inawezekana
 
Zanzibar ilikuwa mwanachama mzuri tu as EAC. Worst tragedy that has befallen Zanzibar ni Muungano wa kinafiki na Tanganyika.
 
Back
Top Bottom