Sababu zilizosaidia ndege ya Nkurunzinza isitunguliwe Bujumbura

Pierre Nkurunzinza janja janja sana huyu bwana,hata jana nchini mwake hakuondoka na ndege ya nchi yake...ili kuwapoteza maboya maadui wake alikodi ndege toka South Africa ikaja kumchukua Bujumbura - Dar es Salaam.Hata "Call Sign" yake haikuwa inaita kama "Burundi 001" ilikuwa inaita kwa Registration number yake ambayo ni ya South Africa,maana nasikia alipanda LearJet45(LJ45) yenye usajili wa ZS-OPR ambayo ni usajili wa Afrika Kusini

View attachment 251751
Sasa kama Rais alifikia kukodi ndege toka Afrika Kusini maanake alianza kunusa harufu za uasi toka kwa watu wake,ambao pengine angekuja na ndege ya Serikali kwayo Marubani wake ni Wanajeshi wangeweza kumuhujumu kwa namna yoyote ile.Hii kukodi ndege ya nchi nyingine na kuendeshwa na marubani ambao ni raia wa nchi nyingine ya Afrika kusini ndio imemuokoa jana Rais Pierre Nkurunzinza,laa sivyo kama angekuwa amekuja na ndege ya Serikali ya Burundi basi historia ya mwaka 1994 ingejirudia jana ktk uwanja wa ndege wa Bujumbura kwa Nkurunzinza kuripuliwa na ndio ingekuwa mwanzo wa machafuko kati ya wale wanaomuungu Nkurunzinza na wale wasio watiifu kwake

Kwenye usafiri wa anga kuna kitu wanaita "Call Sign",huu huwa ni muito wa ndege au utambulisho wake inapokuwa ktk safari zake,utambulisho huu unaweza kuwa ni namba ya usajili ya ndege,au jina la kampuni ya ndege au jina "mahalia" linaloambatana na "flight number"...kwa mfano wa jina "mahalia" kwa ndege za shirika la umma la Afrika Kusini ni "springbok",huyu ni mnyama mwenye sifa na heshima kwa S.Africa,British Airway wao ni "Speedbird",wakati mashirika kama Fly 540 hujiita kama "swift Tango" n.k

Kwa mfano Tanzania shirika la ndege la fast jet "call sign" yake hujiita kama "Greybird" kutokana na picha ya ndege wa kijivu kama alama ya ndege pale mkiani mwa ndege zao.Kwa hiyo hata watu mashuhuri duniani huwa na "call sign" zao wawapo angani au ardhini iwe tu ni ndani ya ndege,mfano Rais wa Marekani akiwa ndani ya ndege ya Rais "call sign" yake huwa ni "Air Force One", akiwa ndani ya meli ataitwa kama "Marine One";kwetu hapa Tanzania ndege ikiwa imebeba rais hujitambulisha kama "Tanzania One",akiwa makamu wa Rais "Tanzania Two" na akiwa Waziri mkuu rubani huita "Tanzania Three".

View attachment 251753View attachment 251756

Tukirudi kwenye mada ya Nkurunzinza Pierre,jana wakati akiondoka Bujumbura kuja Tanzania hakujitambulisha kama "Burundi One" bali marubani wa kukodiwa toka Afrika Kusini waliita kwa "Call sign" ya "ZS-OPR",kitu ambacho kilifanywa kuwa siri ya nani alikuwa ndani ya ndege hiyo,kwa aina ya usajili wa ndege maadui wa Nkurunzinza iliwawia vigumu kujua hasa ni nani yupo ndani ya ndege hiyo na wasingefanya lolote sababu usajili wa ndege ilikuwa ni Afrika Kusini.

Mara baada ya mkutano hapa DSM,Nkurunzinza alitaka kurudi kwa lazima Bujumbura ili akahutubie Taifa kupitia Radio na Tv za Serikali,kujiamini kwako kulikuwa na sababu ya aina ya ndege aliyotumia ili kutua ktk uwanja wa Bujumbura,kitu ambacho aliamini maadui zake hawawezi "kuitungua" kwa sababu zifuatazo:

(1)Ilikuwa ni ndege ya kiraia toka Afrika Kusini

(2)Ilikuwa ndege inayoongozwa na marubani raia wa S.Afrika.

Kuitungua ndege hii yenye marubani wa Afrika Kusini tena "raia" waliombeba "mteja" aliyeikodi,ingeamsha mgogoro mpya wa kidiplomasia ambao "maadui" zake wasingeweza kukubali mtego huo

Nkurunzinza aliondoka Dar es Salaam milango ya saa 1815hrs,lakini baada ya kama saa moja na nusu alirudi tena kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dsm,hii ni baada ya kujaribu kutua mara mbili katika uwanja wa Bujumbura kwa "Call sign" ya " ZS-OPR" badala ya "Burundi One".Hata baada ya rubani kuulizwa mara kadhaa "status of souls on board" alisisitiza kuwa ni "customers" waliomkodi toka Bujumbura-Dsm-Bujumbura.

Baadae Rubani wa ndege akaambiwa "Clear to land at your own risk"...hii ni baada ya chumba cha waongoza ndege kuwa tayari mikononi mwa wanajeshi wasio watiifu kwa Nkurunzinza,hali hii ilimfanya Rubani kugeuza na ku-opt Entebbe International Airport,ambapo Mseven hakuwa tayari,ndipo Pierre akaamua kurudi kwa "Baba" zake Tanzania,mpaka sasa hajulikani amefikia sehemu gani ktk jiji la Dsm,hata Waziri Membe alipooulizwa leo kuwa Nkurunzinza yupo Tz sehemu gani,hakutaka kusema mahali alipo

Hiki ndio kitu pekee kilichomuokoa Brother Nkurunzinza,vinginevyo maadau zake waliokuwa wamefunga mipaka na kutawala viwanja vya ndege wangefanya lolote endapo tu ndege aliyokuwa anatumia ingekuwa ni ile ya Rais ambayo huitumia mara kwa mara,maana kwa maadaui zake kurudi kwa Nkurunzinza toka Dsm na kuhutubia Taifa ingekuwa ni pigo kwani ingezuia vuguvugu na harakati za kumuondoa madarakani zilizokwisha anza.

Lakini mbadala mwingine kama Nkurunzinza angekuwa ametumia ndege ya Rais kurudi Bujumbura kwa kulazimisha ni ima maadui zake wangeitungua ndege yake au wangeruhusu itue na kumshikiria Pierre kwa nguvu,lakini kwa sababu ya "mbeleko" ya ndege ya "kiraia" yenye marubani " raia" toka nchi ya Afrika Kusini,Maadui zake walizingatia diplomasia ya kimataifa na kumsihi rubani asitue Bujumbura "if and only among the souls on board,the soul of Nkurunzinza was boarded"...hii ndio ilikuwa nafuu ya Bro Nkurunzinza na "ujanja" wa team yake ya kijasusi,vinginevyo leo tungekuwa tunaongea mengine na pengine kama yale ya mwaka 1994 ambapo baada ya mkutano wa Dsm,watu walipokuwa wanarudi Makwao wakatunguliwa.
**USHAURI MDOGO KWA WAZIRI WA UTUMISHI**
CC: PAUL MAKONDA
UKIKATA MISHAHARA WATUMISHI WANAOCHELEWA KUFIKA KAZINI, KUNA UWEZEKANO WA KUTENGENEZA MADAWATI 10,000 KILA MWEZI KWA NCHI NZIMA:

mheshimiwa waziri, kama kuna kitu kinachokwamisha utendaji kazi kwa ufanisi na uwajibikaji miongozi mwa watumishi wa umma katika ofisi nyingi za serikali kuu,halmashauri na wilaya ni uchelewaji wa kufika kazini na suala zima la kutozingatia muda na maadili ya kazi na hii huchangiwa na ukosefu wa kamera za CCTV katika ofisi karibia zote za serikali, ambazo uwepo wake utakusaidia wewe na uongozi wako kuweza ku-monitor mienendo ya wafanyakazi kwenye kila ofisi ya serikali, halmashauri na wilaya. Kama inawezekana kwa supermarkets na maduka madogo madogo hata kwa huku mtaani kwetu kuwa na kamera za ulinzi, inashindikana vipi katika ofisi za serikali kama watu wapo serious??? bado nipo ninaandaa dodosi kamili la namna gani unaweza kutekeleza utaratibu wa namna hii kama ushauri wangu binafsi na kuweza kuzaa matunda ambayo watanzania wahatakaa kukusahau, and mark my words,
utarudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi ofisi za serikalini for 80% na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaosoma kwa kukaa chini for the same percentage countrywide!!!!!
 
Duuuh....,Pilau na Mrenda
 
hongereni burundi kwa kukinukisha
Huko Arusha Mkapa wamemgomea kuwapatanisha...Vyama vilivyo katika mazungumzo havitaki baadhi ya watu kuwemo ndani ya mazungumzo
Kufumba na kufumbua,leo mbunge wa EACL ameuwawa...hivi kwanini wanamuacha huyu Nkurunzinza??
 
Kwani huyo Nkurunzinza ndio kamuua huyo mama, mbunge wa EACL?
 
Hali ya Burundi bado tata...naona Mkapa na M7 ndio wataanza mazungumzo upya! Watawala wa Africa wanaianzisha ili waje wakae mezani waendelee kutawala! Ila baada miaka 5 ataomba tena au itakuwaje? Mwisho wa siku atatoka tu maana katiba wametengeneza wenyewe kumbe haikuwa matakwa yao! Atatoka tu hataweza kukaa milele! Aanze kutafuta wapi pa kwenda kuishi baada ya muda wake kwisha
Hivi Mkuu Mkapa kaishia wapi na utatuzi wa mgogoro wa Burundi?Maana kule watu bado wanaendelea kuuwana na EAC ipo kimya.Yaani Viongozi wa Afrika kwa madaraka ni uji na mgonjwa!!Hivi kwani toka atake kupinduliwa,Nkurunzinza amewahi kutoka nje ya nchi?
 
Mkapa ni mwanadiplomasia hana analoweza kufanya kwa mtu anaeng'ang'ania madaraka....africa uikomaa hakuna wa kukutoa zaidi ya waasi wa nchi yako ka Burundi kana njaa na nchi mwisho duniani kwa umasikini! Waasi wasipowezeshwa na nchi jirani hakuna kitu! Naona Rwanda nae mambo yake sio mazuri au hana kundi linam support kule burundi! Amekauka! Mkapa wanamuonea bure hana la kufanya! Zaidi kuwaita na kuwaita meza mazungumzo.....wakubali muda uende yaishe! Na hao waasi wana njaa pia hizi hela za usuluhishi nao wanaishi!!! Sikia tu njaa kiboko
Hivi Mkuu Mkapa kaishia wapi na utatuzi wa mgogoro wa Burundi?Maana kule watu bado wanaendelea kuuwana na EAC ipo kimya.Yaani Viongozi wa Afrika kwa madaraka ni uji na mgonjwa!!Hivi kwani toka atake kupinduliwa,Nkurunzinza amewahi kutoka nje ya nchi?
 
Kwani huyo Nkurunzinza ndio kamuua huyo mama, mbunge wa EACL?
Nkurunzinza kwa sasa anaishi kama kunguru!!Hajulikani analala kwenye mti gani...Huku kwenye mwembe mara huku kwenye mkwaju..Wamuige mwenzao wa Gambia
 
Hivi Mkuu Mkapa kaishia wapi na utatuzi wa mgogoro wa Burundi?Maana kule watu bado wanaendelea kuuwana na EAC ipo kimya.Yaani Viongozi wa Afrika kwa madaraka ni uji na mgonjwa!!Hivi kwani toka atake kupinduliwa,Nkurunzinza amewahi kutoka nje ya nchi?
Tuwaulize Warundi
 
Huko Arusha Mkapa wamemgomea kuwapatanisha...Vyama vilivyo katika mazungumzo havitaki baadhi ya watu kuwemo ndani ya mazungumzo
Kufumba na kufumbua,leo mbunge wa EACL ameuwawa...hivi kwanini wanamuacha huyu Nkurunzinza??
Kama unaifahamu historia ya Burundi utakubaliana na mimi kuwa Nkurunzinza ndiye Rais pekee aliyefanikiwa "walau" kuituliza nchi, na hii ndiyo sababu kubwa ya baadhi ya watu waliokuwa wananufaika na machafuko kushinikiza aachie madaraka!
Nimewahi kuishi bujumbura kwa miezi mitano, wananchi wanamkubali na kukubali kazi yake japo wapo wachache (Wapinzani) ambao wanaendelea na harakati zao za kusaka madaraka (nao pia wana wafuasi) pamoja na yote bado haiondoi ukweli kuwa Rais Nkuru amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutuliza ghasia na kuijenga Burundi mpya.
Zamani (kabla ya Nkurunzinza) hakuna ambaye angefikiria kwenda kutembea Burundi kutokana na machafuko, hali mbaya ya uchumi na nchi kutotawalika lkn leo hii hali ni shwari kwa kiasi kikubwa, biashara zinafanyika, watalii wanaingia na usalama ni wa uhakika pamoja na changamoto kidogo za waasi ambao kwa kiasi kikubwa wamepoteza nguvu na ushawishi.
Ukweli mchungu "Baada ya Nkurunzinza Burundi haitatawalika"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jasusi mahiri kabisa kutoka Tanzania UMEMALIZA KILA KITU ASANTE
Huyu jamaa Nkurunzina alifanya tathmini kama raia wanataka aendelee au hapana na alimtuma mkuu wa usalama Godefroid huyu aliyempindua sasa. Tatizo hakupenda jibu aliloaambiwa kuwa hutakiwi ndo akaamua kumfukuza kazi mkuu wa usalama
 
imeripotiwa tayari Rais yupo Burundi wanamtafuta aliyekuwa anajinasibu kupindua serikali ya nkurunzinza.
Bahati mbaya,Sasa sio tu kapinduliwa ila amekufa kabisa!Ndio mwisho wa ubinadamu wetu...Miaka mitano iliyopita alikwepa mapinduzi...sasa amekwenda na kifo
 
Back
Top Bottom