Sababu za Wanaume wengi kuwa WAPO WAPO KWANZA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za Wanaume wengi kuwa WAPO WAPO KWANZA...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kula kwa tindo, Jul 11, 2012.

 1. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hi!
  Kuna thread moja inahusu michango ya harusi imenikumbusha mbali. Hivi
  jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali
  ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo
  haya:

  1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo
  mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi
  Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia
  shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo
  atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
  2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa
  umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio
  kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na
  gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
  3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane
  Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha
  ubishi, tenga 800,000 tu.
  4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda
  Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna
  imejensi.
  5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye
  hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe
  2,000,000.
  6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida
  kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita
  marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
  7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko
  wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa
  500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.
  8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu
  kuna cheka time)
  9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya
  kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa
  10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
  11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!
  12
  . "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..."
  700,000!
  13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za
  harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000
  maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala
  hutarudishiwa.
  14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili
  watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la
  bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000
  uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi
  watakaoibuka ghafla!
  15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
  16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
  17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila
  utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
  18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa
  uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
  19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar
  ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
  20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa
  wakapambwe saluni. 200,000
  21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black
  kibishi 40,000
  22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana
  akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so
  utalipa malazi ya siku mbili 200,000
  23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini
  ya 800,000 kwa angalau siku 5.
  24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae
  hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote
  iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za
  nani?? 500,000!
  25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer
   
 2. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hili nalo neno!
   
 3. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umeona Mkuu eeeeeh?!!!! Kwa hali hii ya uchumi,ma Single tutakua wengi....
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Trilion times same thing over and over again
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Haha, hujaongelea habari ya michango ya harusi kutokutosha, na unatakiwa u top up
   
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135

  You are becoming too expensive madam.....
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mimi, I just thought its boring now duuh
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kwani sherehe lazima?
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Si lazima but ni muhimu...after all kabla hata ya iyo sherehe makoro koro kiiibao....ah..we are not purchasing you bana!
   
 10. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  piga mimba,weka ndani....huo ni mtaji mkubwa sana wa biashara...
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  yote ya nini hayo wakati mnaweza kuchukuana na kuanza maisha bila gharama yoyote,sana sana ni kulipia pick up ikachukue vyombo vyake na kuhamishia kwako,thats all
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  umuhimu wake nini sifa tu za kijinga...kama huna uwezo si utulie?
   
 13. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Jamani hii thread inarudiwa kila mwezi?muwe mnajaribu kuiedit basi ili iwe mpya khaa!
   
 14. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kana ukweli.. but its so far....
   
 15. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  kazi ipo hapo kaka na hii thread imenitisha
   
 16. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sana mzee.. Kama KALE Mkuu....
   
 17. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Umeua.. duh
   
 18. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,895
  Likes Received: 4,749
  Trophy Points: 280
  90% ya girls bila sherehe utakua unatafuta ugomvi
   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nyie si ndo huwa mnashoboka kutangaza harusi huwa mnaombwa?
   
 20. mjombo's

  mjombo's JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  so expensive mbaya zaidi unaoa uchagani ndio utakoma
   
Loading...