Renegade
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 7,126
- 6,764
Hata kama CCM hao hao walikosea wanapojirekebisha kuna ubaya gani? Yaani tuwachukie kwa kuwa wameamua kujirekebisha? Ni jambo zuri kukubali makosa na kurekebisha, haiondoi nafasi ya wapinzani wapiga kelele..
Wacha niseme kwanza mimi sina chama na wala sina mrengo wowote kisiasa. Ila, nachukia ufisadi!
Hili suala la CCM walifanya hivi au vile nafikiri tunaliongelea kijumla jumla sana.
CCM ni moja lakini ndani yake kuna makundi. Kuna CCM ya Azimio la Arusha na kuna CCM ya Azimio la Zanzibar.
Hapa naongelea wanachama, siyo chama!
Wale wanaoamini Azimio la Zanzibar, walisaini hiyo mikataba lakini kuna wengi wanaoamini katika utu na miiko ya uongozi ambao walipinga jitihada zile za kusaini mikataba ya kitapeli. Kwa hiyo ni vizuri tuwe waangalifu tunapo zungumzia hili suala bila kusahau kiini cha tatizo.
Nitaishia hapa.