sababu za Taifa stars kupoteza mechi ya leo-laana ya vifo huko arusha

Tunafungwa sababu tuna wachezaji andunje viazi na vilaza hata aje mourinho kuwafundisha hawaelewi siasa haipo hapa jaribu kutumia akili ya mwewe utaelewa tu
 
Tukio la kupigwa mabomu kwa watoto na kina mama huku arusha na vyombo vya serikali kutoonyesha empathy kwa waathirika ni laana kubwa ambayo itaitafuna timu yetu ya Taifa leo hii.

TBC ilishindwa kurusha live tukio la bomu lakini sasa hivi inatuonyesha mpira.

Naungana na ndugu wa marehemu na majeruhi kuilaani timu yetu ya taifa ili ipoteze mechi hii kwa kufungwa magoli matano na zaidi ili tujifunze kuheshimu utu wa wanadamu wenzetu.

RIP kwa marehemu wote!
Poleni majeruhi na wahanga wa bomu huko arusha!

naona ugonjwa umeacha kushambulia uti wa mgongo, sasa unashambulia ubongo !
 
naona ugonjwa umeacha kushambulia uti wa mgongo, sasa unashambulia ubongo !

hiki ni kipigo kwa ccm pia!ngoja tusubiri hayo mabilioni mliyoahidi kwa wizara ya utamaduni.mnatafuta pa kutokea lakini wapi!
 
taifa stars vs proffesional ivory coast??siasa zikae pemben,tutengeneze academy za soccer,tujipange kuandaa vijana wadogo frm now ili watusaidie 10,15 years time,kila kitu kamati,inaundwa kamati ya ushindi,utadhan ndo inaingia uwanjan,mabomu arusha utasikia kamati ya kuchunguza,tunaharibu nchi tuliyoijenga kwa muda kwa muda mfupi,hapa hakuna cha laana wala mikosi,siasa siasa tu kila kitu siasa,mpira kujipanga kwa muda mrefu.
 
By Mr Kombe
Poleni wana Arusha Poleni CHADEMA poleni wATANZANIA wote tulisikia aina ya umwagaji damu kwa mtindo wa kujitoa mhanga ktk nchi za wenzetu na sasa tumeshuhudia kwa macho yetu wenyewe damu ya ndugu zetu ikimwagwa kwa stahili hiyo hapa kwetu.Damu ya ndugu zetu hatamwjika bure kwasababu tunaye mtetezi wetu YESU.wauwaji si hewa kwmba hawaonekani,tunao na pengine ni ndugu zetu tuwafichue ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria. Ili nasi tubaki salama.Adui wa ndani ni mbaya kuliko adui wa nje.
 
Maisha mtailaani tbc lakini mkumbuke wakati nyinyi mnazunguana na siasa uchwara wapo ambao hata kuzisikia siasa hawataki bora waangalie mpira
 
Back
Top Bottom