Picha hii ni kielelezo kizuri cha taarifa.
Najiuliza; kwani polisi huwa na kawaida ya kuhakikisha ndugu wa marehemu wanaichukua miili na kuizika kwa wakati? Au hilo nalo ni jukumu jipya la kisheria kwa jesji la wahalifu (polisi)?
Kwa vyoyote vile, hakuna namna wala lugha ya kuspin unyama huu, ccm na serikali yake wanapaswa kujua hilo kabla mambo hayajazidi kuwa mabaya na hatari nchini Tz.
Hivyo napendekeza yafuatayo miongoni mwa mengine:-
1. Ufanyike uchunguzi huru na wa haraka juu ya mauji yote hapo Tarime.
2. Polisi na viongozi wote waliohusika wanajulikana (hata kama wamehamishwa au kustaafu), wakamatwe na kufunguliwe mashtaka ya mauaji mara moja.
3. Mahakama iwaachie huru wote waliokamatwa bila masharti yoyote na kufuta kesi hizo dhalili.
4. Shuguli katika eneo tata la mgodi zisimamishwe mara moja hadi hapo muafaka na haki itakapopatikana.
5. Serikali iombe radhi kwa umma wa Tarime na Tz kwa ujumla na pia ilipe fidia za madhila ya mauaji, hasara za kiuchumi, matibabu kwa walioathiriwa na sumu itokayo mgodini nk
6. Mikataba yote ya madini iandikwe upya, na iwe kwa lengo na maslahi ya MTz kwanza na pili Taifa kwa ujumla.