Sababu za polisi kuiba maiti usiku mochwari na kukamatwa Lissu Tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za polisi kuiba maiti usiku mochwari na kukamatwa Lissu Tarime

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, May 24, 2011.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Picha jeneza barabarani huko Tarime.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa vulugu hizo mpaka kukamatwa wa wabunge hao zilianza jana usiku majira ya saa 1: 30 usiku baada ya ndugu na jamaa za wafiwa kueleza kuwa wameona askari Polisi wakinunua majeneza manne na kupakia katika gari hali ambayo iliashiria kuwa kulikuwa na mpangop wa polisi kuchukua maiti waliouawa kwa risasi mgodini kwa lengo la kuvuluga mpango wa kuendesha maziko ya pamoja ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika katika uwanja wa sabasaba chini ya uratibu wa Chadema.

  Kufuatia taarifa hiyo Tundu Lissu, Waitara na makada wengine wa Chadema pamoja na wananchi walifika katiki eneo la Mochwari ambako muda mfupi wananchi wengi walikuwa wamefika pia kuzuia Polisi kubeba miili hiyo usiku.

  Lakini polisi walipofika majira ya saa 2:00 usiku na kukuta timu kubwa ya watu ambao wallikuwa wamejitolea kulinda maiti hao wasichukuliwe, walianza kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu na ndipo walipowakamata wakina Tundu na wengine.

  Baada ya kuwasambaratisha watu hao na akina Lissu kukamatwa, Polisi waliingia na majeneza yao usiku huo na kuanza kuchukua miili hiyo ambayo waliiondoa Mochwari na kuanza kuisambaza asubuhi katika nyumba za wafiwa nako wakizitelekeza barabarani leo asubuhi.

  Familia waliyagomea masanduku hayo, kwa vile hawakujua kama ilikuwa na ndugu zao ama maiti wengine kwamba hawakushiriki kuitayarisha toka Mochwari hatua ambayo iliifanya mmili hiyo kukaa barabarani hadi majira ya saa 4 ambapo katika kijiji cha Nyakunguru waandishi walipokuwa wakipiga picha walikamatwa wakisingiziwa kuchochea ndugu kuzika.

  Utetezi wa Polisi juu ya kitendo hicho:
  Akizungumza kwa njia ya simu name Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Tarime Constantine Masawe, alikiri kukamatwa kwa watu hao na kueleza kuwa walikamatwa kutokana na jeshi lake kupata taarifa za baadhi ya ngudu wa marehemu kushindwa kuchukua miili ya ndugu zao jana usiku kwa ajili ya maziko.

  "Unajua jana baada ya kufanyika Postmortem kama walivyotaka miili yote ilikuwa chini ya familia, sasa uamuzi wa kuzika ulikuwa juu yao, lakini majira ya saa 2 usiku tulipata taarifa kuwa kuna watu wako Mochwari wamewazuia ndugu wanaotaka kuzika wasichukue miili ya jamaa zao, tulipofika tulikuna wapo watu na tulifanikiwa kuwakamata wanane ambao wanne walikuwa ni wakazi wa Singida na wengine wane wakiwa ni wakazi wa Tarime," alieleza Kamanda Masawe.

  Alisema kuwa baada ya kuwakamata watu hao na kuwatimua wengine waliokuwa wakilinda Mochwari, polisi walisimamia ndugu na jamaa ambao walitaka kuchukua miili hiyo kwa maziko (Usiku) na kuwapa ulinzi.

  "Tuliwasaidia kuchukua miili hiyo Mochwari hapo na kuwapelekea nyumbani kwao, hapo unaposema barabarani ni kwamba ndugu walikuwa wakifika na kusema amefika tuliwashusha na jeneza lao, sasa hii habari ya majeneza kuwa barabarani tumegundua kuwa inachochewa na kundi la watu ambao wamekuwa wakiwatisha wasizike," alieleza Kamanda Masawe.

  Sababu za kuzuiwa Ibada ya Maziko:
  Aidha mpango wa awali ambao ulikuwa umeandaliwa na Chadema ulikuwa ni kuendesha ibada ya maziko katika uwanja wa Saba Saba leo kuanzia saa 2 asubuhi kabla ya kupelekwa katika vijiji vyao kwa ajili ya mazishi ya kifamilia.

  Kwa mujibu wa Tundu Lissu (akizungumza jana kabla ya kukamatwa) alisema licha ya kuwa kulikuwa na makubaliano baina ya familia, Chadema na jeshi la polisi lilowakilishwa na Kamishina wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja, jeshi la polisi lilibatilisha kibari hicho baadaye kwa madai kuwa walikuwa wamepewa maelekezo toka juu.

  "Tumekuwa katika maandalizi ya mazishi hayo tangu jana jioni. Hata hivyo, jioni hii tumeletewa barua ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tarime kututaarifu kwamba haturuhusiwi tena kuwaaga marehemu wetu kama ilivyokubaliwa jana,' alieleza Lissu huku akibainisha kuwa mpango huu uliratibiwa mahususi kwa lengo la kukwamisha jitihada za Ibada hiyo ya maziko ya pamoja kufanyika.

  Polisi walivamia Mochwari kuchukua miili hiyo ili kuharibu mpango wa Chadema wa kuendesha Ibada ya maziko ya pamoja, walitambua kuwa iwapo wangetoa nafasi ya kukucha asubuhi hali ingekuwa kama Arusha kwa vile wananchi walikuwa wakiwaunga mkono Chadema kuaga miili hiyo uwanjwa wa Sabasaba leo saa 2 asubuhi.

  Hivyo sambamba na mkakati huo polisi walichoamua ni kuhakikisha Tundu Lissu na wenzake hawapati dhamana ili usiku wa leo waratibu wau kuzika kwa nguvu na kukamatwa kwa waandishi kuna nia ya kuwatisha, kuwazuia pia kutoa taarifa zao za kuiba maiti ikiwa ni pamoja na picha walizopiga jeneza ambalo limetelekezwa barabarani na polisi zisitoke katika vyombo vya habari kesho.

  Hayo ndiyo ya Tarime;
   
 2. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hiyo haitawasaidia polisi vibaraka wa CCM wanadhani hao ni wasukuma!
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kuna siku watatakiwa kuwajibika kwa haya wanayoyafanya.
   
 4. D

  DENYO JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Polisi vibaraka wakubwa kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  polisi kwa kugeuza kibao.hivi inaruhusiwa kuchukua maiti mortuary wakati wa usiku?
   
 6. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii sasa ndiyo habari, manake ina pande zote zinazohusika. asante sana mkuu.

  sasa fanyeni ufukunyuku wenu mtutundikie hizo picha za majeneza zilizotelekezwa barabarani ili tupandishe hasira sawasawa tayari kuing'oa ccm madarakani
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Si ubabe tu wanatumia...
  Natamani kweli ifike siku ambayo hawa wahusika wote katika kuharibu maisha ya Mtanzania na kunyanyasa raia watahukumiwa na kuwajibishwa ipasavyo!
   
 8. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Picha jeneza la Polisi barabarani hilo.

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 9. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kaka asante kwa kutuwekea picha hii, sasa kama polisi walisaidia ndugu wa marehemu kubeba maiti na walishusha nyumbani kwa waliofiwa je, hapo ndipo nyumbani ama barabarani? Wameumbuka safi sana waandishi mmekamatwa lakini mmefanikiwa kutuonyesha ukweli kwa picha hiii
   
 10. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Yaliyotokea Tarime in mambo ya kusikitisha.

  Huu ni ushahidi kwamba idara za serikali likiwemo jeshi la polisi linaongozwa na watu ambao hawakustahili hata uongozi wa darasa (class monitor). Kwa kiongozi kusema uongo ni aibu na kujivunjia heshima(maelezo ya RPC Masawe). Hivi mazishi yapomoja yangefanyika kungekua na athari gani kwa watawala? Hivi mkusanyiko wa amani kama ulioudhuria mazishi yalofanyika Arusha baada ya polisi kuua raia zaidi ya kutoa ishara juu ya hali ya kutoridhika kwa wananchi ulitishia vipi utawala wa nchi?

  Watawala wasio na upeo wa kuelewa ndio wanaotegemea kupigiwa makofi kila siku. Kwenye hili la Polisi kuua raia hata kama imeshakua mazoea na hakuna wa kuwagusa wananchi wanatambua kwamba ni kosa na niuonevu.

  Kuwepo au kusiwepo mazishi ya pamoja wananchi wameshatambua kwamba wale tuliowapa dhamana wamejichukulia mamlaka tofauti na dhamana yao na mwisho wao unakuja. Hakuna jeshi katika historia ya dunia ambalo limeshinda nguvu ya umma sio hata la Hitler kule Urusi. Hali hii inaumiza mioyo ya watanzania na inasikitisha kwa kila aliyejaliwa uwezo wa kufikiri na kutambua mambo kadri yanavyotokea katika mazingira yake.
   
 11. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Uongozi jeshi la Polisi Tarime ni hovyo kabisa (sorry imenibidi kutumia lugha kali mniwie radhi).

  Toka lini na wapi ndugu wanachukua maiti saa nane za usiku kwa ajili ya maziko? Ni wapi? To the best of my knowledge hakuna hiyo tabia kwa mkoa wa Mara haipo na pia sina hakika kama kwa kina Masawe kuna tabia hiyo.

  Nimwambie Masawe kuwa anaweza kuwa na uwezo wa juu sana wa kufanya na kusema mambo ya kipuuzi afahamu kuwa si wote watakaonunua huo upuuzi.

  Shame on jeshi la polisi Tarime for shooting dead civilians and disrespecting their bodies.
   
 12. b

  baraka boki Senior Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  hali hii itaendelea mpaka lini
   
 13. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tanzania hakuna kiongozi mwenye akili katika Jeshi la Polisi.
   
 14. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Siku zote muuaji lazima aache alama (kwa kutokujua au kwa kujua). Vivyo hivyo shahidi wa uongo atoaye uongo kutetea mauaji haachi kujichanganya.

  Polisi,eti, wanakwenda kuwasaidia wananchi kutoa maiti "mortuary" usiku. Kana kwamba hawajui kuwa saa 12:00 jioni ndiyo mwisho wa kuchukua maiti kwenye chumba cha maiti na kuwa nje ya eneo la hospitali.

  Walianza kukana hawajaua, wakaja kusena walikuwa ni majambazi waliovamia mgodi, wakaja na kutoa rambirambi, now the story goes on in unknown direction of lies.
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Duh! Ninapata shida ku comment hapa maana nikijaribu ku imagine ingekuwa ndio maiti ya marehemu baba yangu, pangechimbika hapo mochuari!
  Mwema ule mpango wako wa police jamii unakufa taratibu kutokana na siasa za ccm. Wanapandikiza chuki kati yetu na police na muda c mrefu utasikia vituo vya police vinachomwa moto!
   
 16. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hawa Polisi wataendelea kutuonea na kutuongopea mpaka lini?
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  akili wazitoe wapi IGP ndo linaonea kama zezeta hivi....
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Fred, naomba uzungushe satellite dish lako ili utupatie habari za waliowekwa ndani. Wamepigwa kweli, na kama ndivyo wana hali gani?
   
 19. Sailor Boy

  Sailor Boy Senior Member

  #19
  May 24, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh hawapolisi tatizo wote lasaba
   
 20. W

  Wings Member

  #20
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Polisi wanasema waliwasaidia wafiwa kupeleka miili nyumbani, mbona hapo bararani hakuna hata nyumba ya jirani? Wangesema wamewatelekeza porini maana hapo naona kama kuna vichaka vifupi.
   
Loading...