Sababu za polisi kuiba maiti usiku mochwari na kukamatwa Lissu Tarime

Hivi mkuu wa nchi hii yupo au yuko kwenye bembea nchi zatu?,mbona vibalaka wake wanawamaliza watanzania? Tutafika 2015 au tutaisha kabla ya hapo? Mabadiliko yanaitajika by any means!!
 
Hiyo miili iliyoporwa na hao majambazi wa Mwema ifanyiwe uchunguzi tena kwani inawezekana hao vibaka wamenyofoa baadhi ya viungo vya hao marehemu kwa mambo ya kishirikina kwani tukio hili la kuiba maiti usiku limekaa kichawi zaidi.
 
Utatuzi wa mifarakano kama hii inahitaji kutatuliwa kwa uangalifu na utaalam wa hali ya juu. Polisi/serikali kukurupuka na kuweka watu ndani siyo suluhu bali ni kumwangia petrol kwenye moto tayari umepamba. Kwani kuna ubaya gani chadema kushirikiana na wananchi huwa kuwazika wapendwa wao. Mimi nilizani huu ni msaada mkubwa kwa Polisi.
 
Chadema ndio wanasababisha hizo maiti zisizikwe, sifa walizo zifata huko bado hawajazipata. huyu lissu hana dini huyu?
 
Mkuu wa Polisi alisikika akisema walishangaa kuona watu wa mikoa mingine (Singida) wanafanya nini huko Tarime. Ningependa kuuliza kuwa yeye anafanya nini huko? Ninaelewa anatokea Kilimanjaro.

Mpuuzi huyu! Alijuaje wametoka Singida? Je kuna mipaka ya kuzika au kuomboleza kimikoa? Tuelezane labda ukifiwa Mwana na uko Arusha unatakiwa kibali cha polisi kusafiri
 
Serikali ya kishikaji itatucost jamani, yaani washikaji zangu wote wa kijiweni nimewapa maisha, wakifika kwenye familia zao wanajisifia wameula, sasa wanatukula, kweli wameula hapo Raisi hutomsikia kabisa akinena jambo kuhusu haya, kweli waliopigana kutafuta amani kwa kumwaga damu viongozi wao wana disciplines ya hali ya Juu watanzania wanateseka tu sasa hivi Serikali ipo chamani tu na sio kwa wananchi hapa tumeliwa, IGP anazungukuka tu na cruiser V8 kipupwe utafikiri anafanya kazi katika NGO flani ambayo yeye ndo mmiliki. Poleni wakazi wa huko, maana uchungu wa msiba na hivyo watu wanavyoitriti miili ya hao jamaa kama wanyama haiko pouwa kabisa, imeniuma sana, hata siku moja maiti haitoki usiku wa manane, EEh Mungu waaangalie na hawa maana hawajui walitendelo, SIASA MCHEZO MCHAFU.
 
Chadema ndio wanasababisha hizo maiti zisizikwe, sifa walizo zifata huko bado hawajazipata. huyu lissu hana dini huyu?

Tumekuzoea upuuzi wako, wewe mwenyewehuku unajulikana mdini mkubwa! Lissu siyo size ya yeyote ccm pamoja nawewe
 
JK hana uchungu kwa sababu waliokufa si waislam

Nimekusoma mara nyingi nadhani unahitaji msaada, jaribu kumuona mchungaji wako wa kiroho akusaidie, you real need some kind of therapy, something wrong with your brain, we are not joking here, innocent peoples have been murdered, please be serious.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Viongozi wa nchi hii ni vema mkajiuliza hali hii mpaka lini? Waswahili husema "bandu bandu humaliza gogo"
 
MAssawe niliamini wewe ni mpiganaji wa kweli kumbe ni upuuzi mtupu huna lolote tena biala haya unatumia vyombo vyetu vya habari kuwadanganya wananchi, ninachoweza kukuarifu kuwa umujishushia heshima sana, Ulipokuwa Arusha tuliheshimu kazi zako lakini umekuwa hopeless kabisa, wachaga hawapo hivyo, wanasiasa wamekudanganya na ukaingia kwenye mtego kwa manufaa yao.
 
Uongozi jeshi la Polisi Tarime ni hovyo kabisa (sorry imenibidi kutumia lugha kali mniwie radhi).

Toka lini na wapi ndugu wanachukua maiti saa nane za usiku kwa ajili ya maziko? Ni wapi? To the best of my knowledge hakuna hiyo tabia kwa mkoa wa Mara haipo na pia sina hakika kama kwa kina Masawe kuna tabia hiyo.

Nimwambie Masawe kuwa anaweza kuwa na uwezo wa juu sana wa kufanya na kusema mambo ya kipuuzi afahamu kuwa si wote watakaonunua huo upuuzi.

Shame on jeshi la polisi Tarime for shooting dead civilians and disrespecting their bodies.

attachment.php

What a shame, it sounds like witchcraft. It is very sad to the Police Force being used in political grounds. dumping human bodies on the road? It doesnont sound like a work of rational Police man. what is going on in Tanganyika?:mod:
 
INAHUZUNISHA SANA,poleni wafiwa.hatuna jeshi hapa tuna makatili inatbidi tuanze na nguvu ya uma kwa kila polisi tunayemfahamu au kumuona na vituo vyote vya polisi na ccm kwa ujumla.
 
Jeshi la polisi wako very cheap, nilikuwa najua ni watu wasio na utashi lakini sikuweza kufikiria kama kuna siku wanaweza kufanya upumbavu wa namna hii.........this is TOOOOO MUCH. Na massawe anakuja na majibu mepesi kabisa ati "watu wa singida na tarime wapi na wapi" Shame on him and shame on everyone involved.

Ninaisubiri kwa hamu siku watakayo wajibika kwa haya wanayoyafanya.
 
Maisha ya watanzania hayatakiwi kuchezewa namna hii. Tusichanganye mambo haya na siasa, tutawavuruga watu. Watanzania tusipende kusikiliza upande mmoja. Naamini kila upande unaweza kuwa na matatizo. Sasa tukae pamoja kwa muafaka. Hili suala siyo la chadema wala ccm bali ni maisha ya watanzania
 
asante.....
Hii sasa ndiyo habari, manake ina pande zote zinazohusika. asante sana mkuu.

sasa fanyeni ufukunyuku wenu mtutundikie hizo picha za majeneza zilizotelekezwa barabarani ili tupandishe hasira sawasawa tayari kuing'oa ccm madarakani
 
Back
Top Bottom