Sababu za mzozo wa gaza kwa ufupi

Sababu za mzozo wa gaza kwa ufupi

Status
Not open for further replies.

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,345
Reaction score
15,850

10517959_462766157194185_8021672139384734713_n.jpg

Ukanda wa Gaza, ni kipande cha ardhi kilichopo katikati ya Israel na Misri, na eneo hilo limekuwa kitovu cha mzozo kati ya Israel na Palestina kwa miaka na miaka.

Israel iliikalia na kuidhibiti Gaza wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967, na iliachilia eneo hilo kwa kuondoa majeshi yake na walowezi mwaka 2005.
Israel iliona hatua hiyo kama kumaliza kuikalia kimabavu Gaza, lakini bado inaendelea kudhibiti mipaka ya Gaza, inaendelea kudhibiti mfumo wake wa maji, na pia inadhibiti anga ya Gaza. Misri inadhibiti mpaka wa Gaza upande wa kusini.
Israel iliweka sheria kali kwa watu na bidhaa kuingia na kutoka Gaza, hatua ambayo Israel inasema ni muhimu kwa usalama wake.
Hata hivyo Wapalestina wanahisi kubanwa na kufungwa, na wanaathirika na matatizo na kijamii na kiuchumi. Makundi makuu ya wanaharakati ya Palestina, likiwemo kundi la Hamas wanasema hali ya udhibiti haivumiliki.
Msimamo mkali wa Hamas ni kuiteketeza Israel, ingawa katika miaka ya hivi karibuni imesema inafikiria kuwa na makubaliano ya amani na Israel ya muda mrefu. Hamas inasema Israel kuendelea kukalia kimabavu maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki ndio sababu ya kufanya mashambulio dhidi ya Israel, kabla na baada ya 2005.
Inasema inafanya hivyo kujikinga dhidi ya mashambulio ya anga, uvamizi na mashambulio mengine ya kijeshi.
Kwa historia, uchambuzi na mengine mengi kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati tembelea: BBC News - Gaza-Israel conflict: Why are civilians on the front lines?
 
Hawa watu sijui kama kuna siku watakuja kupatana
 
Ukanda wa Gaza, ni kipande cha ardhi kilichopo katikati ya Israel na Misri, na eneo hilo limekuwa kitovu cha mzozo kati ya Israel na Palestina kwa miaka na mikaka.
Israel iliikalia na kuidhibiti Gaza wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967, na iliachilia eneo hilo kwa kuondoa majeshi yake na walowezi mwaka 2005.
Israel iliona hatua hiyo kama kumaliza kuikalia kimabavu Gaza, lakini bado inaendelea kudhibiti mipaka ya Gaza, inaendelea kudhibiti mfumo wake wa maji, na pia inadhibiti anga ya Gaza. Misri inadhibiti mpaka wa Gaza upande wa kusini.
Israel iliweka sheria kali kwa watu na bidhaa kuingia na kutoka Gaza, hatua ambayo Israel inasema ni muhimu kwa usalama wake.
Hata hivyo Wapalestina wanahisi kubanwa na kufungwa, na wanaathirika na matatizo na kijamii na kiuchumi. Makundi makuu ya wanaharakati ya Palestina, likiwemo kundi la Hamas wanasema hali ya udhibiti haivumiliki.
Msimamo mkali wa Hamas ni kuiteketeza Israel, ingawa katika miaka ya hivi karibuni imesema inafikiria kuwa na makubaliano ya amani na Israel ya muda mrefu. Hamas inasema Israel kuendelea kukalia kimabavu maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki ndio sababu ya kufanya mashambulio dhidi ya Israel, kabla na baada ya 2005.
Inasema inafanya hivyo kujikinga dhidi ya mashambulio ya anga, uvamizi na mashambulio mengine ya kijeshi.
 
Ni kweli wapalestina wanateseka, lakini hata waisrael waliteseka kipindi walipofukuzwa nchi yao kipindi cha Mohammad katika harakati za kusambaza dini kwa upanga

Huu ni ushahidi

Sura 5;51

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

Sura 2:191
Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom