Sababu za kuhitaji muungano wa mkataba Tanzania

Afroshirazy

Member
Oct 19, 2012
6
0
MFUMOMPYA WA MUUNGANO WA MKATABA:
Kamanilivyotangulia kueleza, tumedumu na Muungano wa Katiba kwa miaka 49 ambaopamoja na mafanikio ya kuziweka nchi zetu mbili pamoja katika kipindi chote hicho,bado umeshindwa kutujengea kuaminiana kwa dhati na zaidi umeshindwa kuyatatuamatatizo ya msingi yanayotokana na maumbile ya mfumo huo.
Ulimwenguwa sasa umeshuhudia aina mpya ya mahusiano kati ya nchi huru ambao hutoa nafasiya mashirikiano kwa maeneo yanakayokubaliwa na nchi husika huku kila nchiikibaki na mamlaka yake kama nchi kamili (sovereign status). Mfumo huu kisheriaunaitwa ‘CONFEDERATION’ ambao kimsingi ni Muungano wa Mkataba (Treaty basedUnion). Katika mfumo huu, yale maeneo ya ushirikiano huwekwa katika mkataba aumikataba baina ya nchi zilizoamua kushirikiana na hutoa fursa ya kurekebishwakila mahitaji yanapojitokeza kwa kadiri na kwa mujibu wa makubaliano yaliyomokwenye mkataba au mikataba hiyo.
Umojawa Ulaya (European Union – EU) ni mfano mzuri wa muungano wa aina hii ambaponchi wanachama zinashirikiana katika maeneo mengi yaliyomo katika Mikatabatofauti lakini kila nchi mwanachama imebaki kuwa na hadhi yake kama nchi nakubaki na uanachama wake katika Umoja wa Mataifa (UN) na hata katika mashirikamengine ya kimataifa. Katika Umoja wa Ulaya (EU), miongoni mwa maeneowanayoshirikiana ni pamoja na:
(a) Sarafu moja;
(b) Uhamiaji;
(c) Uratibu wa sera za mambo ya nje za nchi wanachama;
(d) Ulinzi;
(e) Soko la pamoja la bidhaa, ajira na huduma;
(f)Uratibu wa sera za uchumi na fedha za nchi wanachama;
(g) Hifadhi ya mazingira;
(h) Viwango vya usalama na afya (health and safety standards).
Mfanomwengine wa ushirikiano kwa nchi za Ulaya nje ya EU ni ule unaohusu kuwa navisa ya pamoja kwa wageni wanaoingia katika nchi zilizo katika Mkataba waSchengen ambao hutoa visa inayoitwa ‘SCHENGEN VISA’. Baadhi ya nchi wanachamawa EU na wasio wanachama wa EU (kwa mfano Norway) ni wanachama wa utaratibuhuu.
Kwaupande mwengine, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mfano mwengine mzuri waushirikiano wa aina hii. Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East AfricanCommunity Treaty) unatambua maeneo 17 ya ushirikiano miongoni mwa nchiwanachama. Maeneo hayo ni:
(a) Ushirikiano katika Masuala ya Sarafu na Fedha;
(b) Ushirikiano katika Biashara Huria na Maendeleo ya Biashara;
(c) Ushirikiano katika Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda;
(d) Ushirikiano katika Uwekaji Viwango, Kuhakikisha Ubora wa Bidhaa, Utabiri waHali ya Hewa na Vipimo;
(e) Ushirikiano katika Mahusiano na Jumuiya nyengine za Kikanda na za Kimataifapamoja na ushirikiano na nchi washirika wa maendeleo;
(f)Ushirikiano katika Miundombinu na Huduma;
(g) Ushirikiano katika Kukuza Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia;
(h) Ushirikiano katika Kilimo na Uhakika wa Chakula;
(i)Ushirikiano katika Utunzaji Mazingira na Usimamizi wa Maliasili;
(j)Ushirikiano katika Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori;
(k) Ushirikiano katika Afya, Ustawi wa Jamii na Utamaduni;
(l)Ushirikiano katika Kukuza Ushiriki wa Wanawake katika Maendeleo ya Kijamii naKiuchumi;
(m) Ushirikiano katika Masuala ya Sheria na Mahkama;
(n) Ushirikiano katika Mambo ya Kisiasa;
(o) Ushirikiano katika Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia;
(p) Ushirikiano katika Uhuru wa Watu kwenda watakapo, Huduma za Kazi, Haki yaKuishi na Ukaazi; na
(q) Ushirikiano katika Maeneo Mengine.
Lililodhahiri katika miungano ya mikataba ya aina zilizotajwa hapo juu ni kuwamisuguano kwa kiasi kikubwa hupungua kwani kila nchi hubaki na mamlaka yake nauhuru wa kujiamulia na wakati huo huo kujenga misingi mizuri ya ushirikiano nanchi wanachama.
MUUNGANOWA MKATABA KATI YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA:

  1. Kutokana na hoja nilizozieleza hapo juu, mimi ninapendekeza kuwa baada ya uzoefu wa miaka 49 wa Muungano wa Katiba (Constitutional Union) kati ya Zanzibar na Tanganyika ambao baadhi ya matatizo yake ya kimaumbile yameelezwa na kufafanuliwa hapo juu, sasa Zanzibar na Tanganyika ziingie katika mfumo wa “CONFEDERATION” kupitia Muungano wa Mkataba (Treaty based Union).

  1. Katika mfumo huo wa Muungano wa Mkataba, kutakuwa na Serikali mbili ambapo Jamhuri ya Tanganyika itakuwa na Serikali yake na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar itakuwa na Serikali yake, zote mbili zikiwa na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa, na kisha Serikali hizo mbili zitafunga mkataba wa mashirikiano baina yao ambao unaweza ukapewa jina la ‘Tanzanian Union Treaty’. Yale maeneo yatakayokubaliwa kuwa chini ya ushirikiano wa nchi mbili huru yatasimamiwa na Kamisheni ya Muungano (Tanzanian Commission) kama ilivyo kwa Kamisheni ya Ulaya (European Commission) au jina jengine lolote litakalokubaliwa na nchi mbili hizi.

  1. Kila nchi kati ya Zanzibar na Tanganyika zitakuwa na hadhi ya nchi kamili (sovereign states) na zitakuwa na uanachama wake katika Umoja wa Mataifa (UN) na pia katika jumuiya, mashirika na taasisi nyengine za kimataifa lakini kwa kuzingatia msingi wa mashirikiano zinaweza kukubaliana kuratibu sera zake za mambo ya nje kadiri zitakavyoona inafaa.

  1. Maeneo ya kuingia katika Mkataba au Mikataba ya Ushirikiano kati ya Zanzibar na Tanganyika yataamuliwa na serikali mbili zitakazokuwa na mamlaka kamili kila moja katika eneo lake. Mambo yanayoweza kufikiriwa ni pamoja na:
(i) Ushirikiano katika Ulinzi na Usalama;
(ii) Ushirikiano katika Uwekaji Viwango, Kuhakikisha Uborawa Bidhaa, Utabiri wa Hali ya Hewa na Vipimo;
(iii) Ushirikiano katika Mahusiano na Jumuiya nyengine za Kikanda na za Kimataifapamoja na ushirikiano na nchi washirika wa maendeleo;
(iv) Ushirkiano katika Kukuza Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia;

  1. Kwa kufuata mfumo wa sheria za nchi za Jumuiya ya Madola (common law system) inapendekezwa kuwa Mkataba wa Ushirikiano kati ya Zanzibar na Tanganyika utiwe saini na Rais wa Jamhuri ya Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika baada ya mazungumzo yatakayohusisha wawakilishi watakaoteuliwa kuunda timu za mashauriano na majadiliano za Serikali za nchi mbili hizi. Kabla ya kutiwa saini na Marais wa nchi mbili hizi, Rasimu ya Mkataba huu baada ya kukubaliwa ifikishwe mbele ya Bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maoni na kisha Rasimu hiyo ipelekwe kwa wananchi wa Zanzibar na wa Tanganyika kupitia njia ya kura ya maoni kwa ajili ya kuidhinishwa kufuatana na Sheria ya Kura ya Maoni ya kila nchi.
NIZIPI FAIDA ZA MUUNGANO WA MKATABA:


  1. Hakuna khofu ya nchi moja kuimeza au kuitawala nchi nyengine.
    1. Kila nchi inabaki na uhuru na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kuamua mambo yake.
    2. Kila nchi mwanachama ina uhuru wa kujitoa katika jambo lolote ililoamua mwanzo kushirikiana pale inapoona hakuna maslahi au faida kuendelea nalo.
    3. Huvutia nchi nyingi kuingia katika Muungano wa aina hiyo kwa sababu hakuna khofu ya kupoteza mamlaka au kupunguziwa madaraka au mambo yake kuamuliwa na nchi nyengine.
    4. Mahusiano huwa ni ya kirafiki na ya ujirani mwema yanayopelekea kuaminiana na kuondoa kutiliana shaka kusikokwisha.
KAMANI MKATABA, KWA NINI ISIWE KUPITIA EAC TU?
Wapobaadhi ya watu wakiwemo Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba waliohojikwamba iwapo Zanzibar inaona hakuna haja tena ya kuendelea na mfumo uliopo wa Muunganona badala yake inataka kuwa na mashirikiano kupitia Muungano wa Mkataba kwamambo yatakayokubaliwa, kwa nini mashirikiano hayo yasiwe kwa kupitia Jumuiyaya Afrika Mashariki (EAC) ambayo pia ni aina ya Muungano wa Mkataba? Wenye hojahiyo wanasema basi wacha Zanzibar na Tanganyika zikutane Afrika Mashariki.
Hojahii ni nzuri lakini haizingatii uhalisia wa mambo. Pamoja na kuundwa upya kwaJumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kupitia Mkataba ambao unahusisha maeneo mengikati ya yale niliyoyataja hapa kwamba yanaweza kufikiriwa kuwa ya ushirikianokati ya Zanzibar na Tanganyika, ukweli unabaki kuwa utekelezaji wake katikaeneo la Afrika Mashariki umekuwa ni mdogo mno.
Nchitano zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki – Tanzania, Kenya, Uganda, Rwandana Burundi – hazionekani kuwa zimejenga kuaminiana kwa dhati licha ya matamshiya hamasa za kisiasa yanayotolewa na viongozi wake. Ndiyo maana maeneo mengiyamebaki katika makaratasi lakini hakuna utekelezaji. Hata hatua zilizotangazwakuwa zinapaswa kufikiwa kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki hazionekanikutekelezwa kwa dhati na badala yake kumekuwa na kutegana na hata kuogopana.
Baadaya miaka 49 ya kuwa pamoja katika Muungano (pamoja na matatizo yake yote),Zanzibar na Tanganyika angalau zimekuwa na uzoefu wa kufanya kazi pamoja.Kubadili aina ya mahusiano na mashirikiano yake kutoka kwenye Muungano waKikatiba kwenda kwenye Muungano wa Mkataba kunaweza kuwa jambo linalowezekanazaidi katika utekelezaji kuliko nchi hizi tano na pengine kunaweza kutoa mfanowa vipi utekelezaji wa maeneo hayo ya mashirikiano unavyopaswa kuendeshwa nakusimamiwa.
Isitosheunaweza tukawa mwanachama wa EAC na bado kukawepo ushirikiano wa Zanzibar naTanganyika kupitia mkataba baina yao peke yao. Duniani iko mifano ya nchi ambazopamoja na kuwa ni wanachama wa pamoja wa miungano au jumuiya za ushirikianozenye kushirikisha nchi nyingi zaidi, bado kunakuwa na nchi mbili ambazokutokana na historia ya ushirikiano wake zinabaki kuwa na ushirikiano waomwengine unaozihusisha nchi hizo tu. Mfano katika suala la ushirikiano waulinzi, pamoja na kwamba Marekani na Uingereza zote mbili ni wanachama wa NATOlakini bado nchi mbili hizo zina mikataba ya peke yao kuhusiana na ushirikianowa ulinzi kati yao. Katika Ulaya, kuna mashirikiano kupitia mkataba baina yanchi tatu – Belgium, The Netherlands and Luxembourg (BENELUX) – lakinibado zote ni wanachama wa Umoja wa Ulaya (European Union).
KIPINDICHA MPITO:
Haliya kubadilisha msingi wa mahusiano ya Zanzibar na Tanganyika kutoka kwenye Muunganowa Katiba (Constitutional Union) kwenda kwenye Mfumo wa kisasa waMuungano wa Mkataba (Treaty based Union) bila shaka utahusishamabadiliko makubwa ambayo yanahitaji kipindi cha mpito (transitional period)na kuwepo kwa utaratibu wa mpito (transitional process) kutoka mfumouliopo sasa kwenda kwenye mfumo mpya.
Katikakipindi hicho cha mpito, maoni ya watu wa Tanganyika kuhusu Katibayaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yanaweza kutumika kuandaa rasimuya Katiba ya Tanganyika na baada ya kupitisha Katiba ya Tanganyika, Serikali zanchi mbili (Zanzibar na Tanganyika) zikae pamoja kuchagua maeneo yakushirikiana na kisha kuandaa Mkataba wa Mashirikiano yao.
Kutahitajikakuundwe timu ya watalaamu wa masuala ya kisheria na kiutawala kutoka Zanzibarna Tanganyika na pia kuhusisha kuomba wataalamu waliobobea wa fani hizo nawaliosimamia vipindi vya mpito kama hivi katika nchi nyengine kuja kusaidiakuweka utaratibu maridhawa utakaohakikisha kuendelea kuwepo kwa mahusiano yakidugu ya nchi hizi katika mfumo mpya. Jumuiya za kimataifa kama Umoja waMataifa (UN), Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Afrika (AU), Umojawa Ulaya (EU) na nchi jirani na nchi za nje zenye kufuata mfumo wa sheria zakiingereza kama Uingereza, Malaysia, Singapore, Kenya, Uganda na Afrika Kusinizinaweza kuombwa kusaidia kutoa wataalamu watakaokuwa kama washauri waelekezi(consultants) kwa nchi zetu wakati wa maandalizi ya utaratibu wa mpito(transitional process) kuelekea Muungano wa kisasa wa Mkataba wa Zanzibar naTanganyika chini ya misingi ya uhuru, usawa, udugu na ukweli.
MUUNGANOWA MKATABA NI SAWA NA KUVUNJA MUUNGANO?
Wasioitakiamema Zanzibar au wang’ang’anizi wa mfumo uliopo wa Muungano waliouzoea (penginekwa sababu unawanufaisha wao) wanaweza kudai kwamba hatua hizi zinazopendekezwahaziashirii nia njema ya kuendeleza na kuimarisha Muungano. Mimi binafsi nawenzangu tunaoamini katika Muungano wa Mkataba hatuamini hivyo. Tunaaminikatika kuwa wakweli na wawazi, kwamba hivyo ndivyo mahitaji ya wakati huu na zamahizi yanavyodai.
Ulimwenguunabadilika kwa kasi. Zama za kuendesha mambo kwa ubabe na ukichwa ngumuzimepitwa na wakati. Tuache ile tabia ya kuyaona mapendekezo ya kubadili mfumowa Muungano kuwa yana nia ya kuuvunja Muungano huo. Muungano ili udumu unahitajiridhaa ya walioungana. Muasisi wa Muungano huu, Mwalimu Nyerere mwenyewe,aliwahi kueleza umuhimu wa ridhaa katika masuala haya na kuonyesha kwambaridhaa ya mshirika mmojawapo ikiondoka, Muungano hauwezi kusimama. Alisemamwaka 1968:
“Ifthe mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, andfor some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to theirexistence, I could not bomb them into submission … The Union would have ceasedto exist when the consent of its constituent members was withdrawn.” [11]
“Iwapowananchi walio wengi wa Zanzibar wataamua, bila ya msukumo wa kutoka nje, nakwa sababu zao wenyewe, kwamba Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao, siwezikuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu … Muungano utasita kuendelea pale ridhaa yawashirika wake itakapoondolewa.”
Wazanzibarini watu wenye historia ya maingiliano ya jamii za watu mbali mbali na hivyohawawezi kukataa umoja, alimradi tu umoja huo uwe na maslahi na faida kwao.Mfumo uliopo sasa hauinufaishi Zanzibar na hivyo haukubaliki kwa Wazanzibari.Koti la Muungano kama lilivyo sasa linabana sana. Wakati umefika tushone kotijipya kwa mujibu wa mahitaji ya zama hizi.
Hakunamabadiliko yasiyowezekana kufanyika na kusimamiwa vyema iwapo tutatumia njia yamazungumzo. Mazungumzo makini, ya kina na yenye kuambatana na nia njema kwawahusika wote ndiyo njia pekee ya matumaini katika kuyapatia ufumbuzi matatizoyanayolikabili Taifa letu. Hakuna mbadala wa mazungumzo. Nje ya mazungumzo nifujo.
 
Back
Top Bottom