Haiingii akilini kwamba wageni wanaokuja Tanzania wanapita kenya, kwanza wanapita hko kufanya nini? Ni kwa nini serikali yetu wanashindwa kujenga na kuimarisha viwanja vyetu vya ndenge KIA, JKNIA etc ili viwe na viwango vya ndege kutua moja kwa moja toka Ulaya?
Nawaunga mkono Kenya, waendelee kufunga mipaka yao na kuweka vizuizi vizito kwenye viwanja vyao ili na sisi akili zitukae sawasawa tuwajibike na kutengeneza mazingira mazuri ndani ya nchi yetu.
Nchi kubwa hii ya Tanzania, tumeshindwa kuendesha shirika letu la ndege sasa tunaendelea kutegemea kenya airways, huu si ni ujinga? mabilioni uswiss yamefichwa ni swala la sisi kuyafuata na kuyarudisha ili tujenge nchi yetu!!