Sababu za kiintelijensia zimebadilika tayari

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,604
4,259
1. Nakumbuka mara baada ya kwisha uchaguzi mkuu, mikutano ya kisiasa ilikatazwa kwa sababu hali ya amani ilikuwa tete, nchi ilikuwa haija-stabilize kutokana na tension ya uchaguzi. Sijui uhalisia wake lakini hiyo ndiyo sababu iliyotolewa.

2. Baadaye mikusanyiko hata ya ndani ilipigwa marufuku kwa kisingizio cha ugonjwa wa ajabu uliotokea Dodoma, japo sababu hiyo ililazimika kubadilishwa baada ya mikusanyiko ya namna hiyo kutawanywa Kilimanjaro, ilhali ile ya CCM ikiendelea, hata Dodoma huko huko kwenye "ugonjwa huo wa ajabu"

3. Kilichofuata ni kuruhusu kidogo mikutano ya ndani, na kisha tukapewa sababu nyingine ya kuzuia shughuli za kisiasa kwamba "Uchaguzi umepita, huu ni muda wa kazi! Kila siku mikutano...kila siku mikutano, sasa watu watafanya kazi saa ngapi?" Wakati huo tukaambiwa kuwa masuala ya kisiasa yanamchlewesha mheshimiwa Rais kuwaletea maendeleo wananchi wake

4. Hivi karibuni mikutano yote ya ndani imepigwa marufuku kwa kisingizio kuwa inatumika kuwachochea wananchi kupambana na jeshi la polisi. Sijapata reference ya matukio ya namna hiyo, ila bado natafuta.

5. Sasa hivi nimesikia kwamba mikutano na maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika Septemba mosi yamekatazwa "kwa sababu jeshi la polisi litakuwa busy elsewhere likishirikiana na JWTZ katika maadhimisho yao" Hii taarifa sijui kama imetungwa au ni ya kweli...but nayo pia ni sababu.

Swali ninalojiuliza hapa: Hivi sababu ya ukweli hasa ya kuzuia shughuli za kisiasa nchi hii ya Tanzania ni ipi?
 
Back
Top Bottom