Sababu za ccm -kushindwa arumeru mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za ccm -kushindwa arumeru mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by OMEGA, Apr 3, 2012.

 1. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Wakuu,kwanza naomba nijiwakilishe kuwa mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa japo siasa ninaipenda.Pia naomba nieleweke kuwa nachukia ufisadi,unafiki wa kisiasa na umaifa wa kisiasa unaofanywa na CCM,mfano wizi wa kura,ktumia green guards,etc.Kwa izi siku mbili nimevutiwa sana na kauli za busra za Nape,mwanzoni hakuwa ananivutia lakini matamshi yake yote aliyoyatoa baada ya uchguzi ni ya kiungwana na ya busara sana,ingawaje always,i wish I knew comes last.Kazungumzia kuwa watakaa kama chama kutathmini uchaguzi na kuangalia sababu ya kushindwa kwa kishindo,assume na mimi ni mmoja wa wajumbe kwenye kikao icho,huu ndio mchango wangu wa sababu za kufeli.
  1.Utumiaji wa siasa za adaa za mwaka 47:Sasa hivi watanzania wengi wana upeo na ni wafuatiliaji wa siasa za kila siku,vyonmbo vya habari vimetapakaa kila kona tofauti na enzi za Mwalimu.Kutumia siasa za ghiliba ni kujizika kisiasa.Watu wana hali mbaya kiuchumi na wanajua hali hii sio kwa sababu ya mapenzi ya Mungu bali ni kwasababu ya sera mbovu za chama tawala.Wanafahamu nchi zilizokuwa nyuma yetu,zilizokuwa na vita na machafuko na ambazo azina rasilimali nyingi kama sisi,lakini baada ya kuchukua hatua madhubuti uchumi wao umeimalika.
  2.Kutumia watu wasio na mvuto au waliopoteza mvuto kuendesha Kampeni:CCM ina watu wenye convincing power mfano Magufuli,Rose Asha Migiro,Anna Tibaijuka,Mizengo Pinda.Vijana wakina Nape,January na wengineo.CCM imeacha watu wenye busara zao na mvuto na badala yake wanatumia watu kama Wasila,Lusinde,Vicky kamata na wengineo ambao si tu hawana mvuto lakini baadhi yao hata busara yao ya kuchagua maneno ya kuongea jukwaani ni questionable.
  3.Militarization of politics and politicization of the military.Kutumia green guards na vitisho vya vyombo vya dola hata kabla ya uchaguzi wenyewe ni kosa.Baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola kujidhiirisha kama wanasiasa kwa kauli zao na misimamo yao ilikuwa ni hatari kwa CCM.When it comes to use of force,kawaida watu wanaji identify na yule mtu ambaye wanadhani vyombo vya dola vinamnyanyasa.
  4.Kitendo cha Nassari kujinyenyekeza kwa watu kuwa yeye ni maskini mwenzao ambaye mama yake anaishi kwa uchuuzi wa mbogamboga na anashindana na tajiri asiye na shida kilimfanya apate kura za huruma na hasa za akina mama ambao inmost case ndio wanaoisaidia CCM kwenye chaguzi,CCM haikugundua kuwa Nassari anatafuta sympathy ya maskini na kusapoti hiyo rhitoric kuwa kweli ni maskini wa kutupwa,mfano ni matamshi ya wapiga kampeni wa CCM kuwa Nassari anafanya kazi ya kuosha mbwa wa wazungu,au hana viatu etc.Yeye hakukanusha tuhuma izo na hivyo kupata support ya vijana na watu wa kawaida ambao wanaishi kwa kubangaiza.
  5.Kutumia muda mwingi wa Kampeni kutoa maneno ya kashfa kwa mgombea na Chama chake badala ya ku addrees key issues ambazo ni matatizo ya watanzania.Pale CCM ilipojaribu kutoa majibu yaliacha utata mwingi,mfano mdogo ni pale Raisi mstaafu aliyetawala kwa miaka kumi na kushindwa kutatua tatizo la ardhi Arumeru anaposimama jukwaani na kuwaambia wananchi kuwa atamshawishi Raisi aliyebakiza miaka miwili na nusu kumaliza kipindi chake heti atatue matatizo ya ardhi Arumeru.Mgombea mwenyewe anatoa ahadi kama hiyo wakati baba yake aliyekuwa mbunge kwa miaka saba hakutatua ilo tatizo.Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi campaingn ilivyokuwa ya ubabaishaji,pia kila mpiga debe aliyekuwa anasimama alikuwa anatoa ahadi zake tofauti na aliyemtangulia,campaing ilikuwa disorganised,un coordinated na ilikosa generalised TOR.
  6.Matusi yaliyokithiri ya Lusinde-Sina haja ya kuyarudia kwani kila mmoja anajua athari za hayo matusi katika kampeni ile.
  7.Kujaribu kutumia mbinu chafu na zilizopitwa na wakati-mfano kununua kura,kuonga etc.
  8.Mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi,
  9.Kutochukulia hatua mafisadi-Kutojivua gamba:Wananchi wanasubiri CCM ijivue gamba.sasa ni takriban mwaka hatuoni ikijivua magamba.
  10.Umahiri wa mgombea wa CHADEMA katika kuelezea hisia zake kwa mvuto tofauti na mgombea wa CCM ambaye alipoa sana katika hotuba zake,hazikuwa na mvuto wala ushawishi wa kumfanya mtu ahamini anachokisema,nadhani sio natural politician tofauti na mwenzake ambaye I believe ni charismatic.CCM walikuwa sahii kuchagua mgombea kijana kwani kwa Tanzania ya leo vijana wanaona wanasiasa wazee kama walaghai na wasio na uchungu na nchi wala vision,tatizo ni haiba ya mgombea mwenyewe,hakuwa mchangamfu tofauti na mgombea wa CHADEMA.
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  I support ila sikio la kufa kila dawa inadunda..
   
 3. y

  yplus Senior Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ile ya mwalimu si ya sasa,CCM ya sasa sijui niifananishe na nini!
  Lakini walio ona ya mbele walitabiri kuwa imepoteza dira na mwelekeo,matokeo yake wakawa Genocide.
  Nawasilsha.
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Omega,

  Sikubaliani na hoja yako ya pili. Sasa hivi ndani ya CCM hakuna ambaye ana mvuto kwa kuwa chama kimeshindwa kutekeleza mambo mengi ambayo kiliahidi kuwafanyia wananchi.

  Kama una kumbukumbu nzuri, Nape alienda Arumeru na pia Januari Makamba alikuwa huko, na umewataja kwamba wana mvuto.

  Hata kama Migiro angeenda, angewaambia nini kipya? Ana mvuto gani? Prof. Tibaijuka angewaambia nini na ilihali yeye ni Waziri wa Ardhi na wananchi wameporwa ardhi na wawekezaji? Magufuli angewaambia nini na ili hali kuna nyumba zilivunjwa tangu 2006 ili kupisha ujenzi wa barabara ambayo mpaka leo ujenzi wake haujaanza? Mizengo Pinda ana mvuto gani? Huyu aliyejinasibu kwamba ni "mtoto wa mkulima" na kumbe kichaka cha kuhifadhi mafisadi. Kila akipelekewa hoja za mafisadi anazifunika.

  Kwa kifupi ni kwamba mtu individually anaweza kuwa na mvuto, lakini akibanwa na maswali ya utendaji wa serikali ya chama tawala, sidhani kama anaweza kutoa majibu ya kuridhisha na ndio maana unakuta akina Mkapa wanakimbilia kusema CCM ilileta Uhuru na kuondoa ukoloni na ubaguzi wa rangi huku Kusini mwa Afrika. Hivi leo hii kuna haja ya kuambizana hizo historia? Miaka 50 baada ya uhuru, as if nyingine hazikupigania uhuru. Nilishasahau hata orodha ya nchi tano ambazo zilikuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi za Kusini.

  Ugumu wa maisha ndio unaimaliza CCM. Mwananchi hana uhakika wa mlo halafu anamuona Wassira yuko V8 la serikali full kiyoyozi, bado utamwambia kwamba CCM ni nzuri na ilihali akienda kuuza sokoni ushuru kibao, mara mgambo wamsumbue mara bado huyo mtu ataipenda CCM?

  Siku ya Uchaguzi Masako alisema kwamba walijitokeza wazee wengi na akina mama. Hili kundi ndio tegemeo la CCM na ndio maana Tume iligoma kuboresha daftari la wapiga kura. Hili lilikuwa ni kundi la wapiga kura watiifu kwa chama tawala. Ndio maana wiki ya mwisho ya kuelekea uchaguzi Mama wa mipasho Sofia Simba alitua Arumeru akisaidiana na Mama Nagu na kuanza kuwahadaa akina mama kwamba wangepewa mikopo. Bado hazikutosha!
   
 5. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  mkuu ccm hakuna jipya,mtaji wao wa wanawake na wazee unazidi kupoloka kila kukcha!kofia na khanga yalikuwa nimatusi makubwa kwa watz. 2015 utakuwa mwaka waukombozi.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  There is only ONE Reason

  CCM IMECHOKWA, INACHUKIWA NA HAIPENDEKI TENA
   
 7. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umesema meeengi, lakini sababu ya kushindwa ccm either unaikwepa au huijui. Angalia michango ya siku kwa siku hapa JF ndio utajua kwamba sababu ya kushindwa kwa ccm Arumeru si Sioi wala Mkapa wala Nchemba wala bwana Mitusi. Watanzania wengi hawaitaki tena ccm, basi! Wewe angalia, Arumeru kwa wapiga kura wale wale wa 2010 ambapo ccm ilishinda, ni wangapi hawakuipigia kura ccm wameipigia CDM? Halafu jiulize kile kizazi kipya ambacho hakikuwa na sifa kiumri kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na walikosa nafasi ya kupiga kura juzi, katika marekebisho yatakayokuja kabla ya 2015 watakuwa wameandikishwa ambao kama 80% hawataki kuisikia ccm, je kwenye general election ya 2015 ccm itakuwa na hali gani? Watz wameamka si wale wakudanganywa tena kwa T-shirt na kofia na khanga. Watakula ccm na kulala CDM. Wait and see.
   
Loading...