Nakuunga mkono mkuu. Kama wanaogopa kuongea na wananchi wanaotegemea kuwaongoza tutategemeaje uongozi shirikishi kutoka kwa maendeleo ya taifa letu.
Ni jambo moja Makamba kurupoka kama kawaida yake, lakini ni jambo lingine kama hao wagombea wa ccm wako tayari kushiriki midahalo hata kama wasingekatazwa. Nadhani ccm sio ya makamba, inapaswa kuwa na washauri ili katika jambo jema kama hilo huyo mropokaji asisikilizwe.
Any way, nadhani ni wakati sasa wa watanzania kufungua macho na kutoa kura kwa wagombea ambao watatoa sera zao katika midahalo hiyo, pamoja na katika kampeni. Hao ambao wanatawaliwa na huyo mropokaji wao na kukubali kujificha nyuma ya pazia, na wabakie huko huko, hawatafaa kuleta maendeleo katika nchi yetu. Na hawakuweza kuleta kwa sababu daima walijificha nyumba ya pazia. Labda wataweza kuongoza kutoka nyuma ya pazia kwa kutumia 'kitawalambali'. Hata wakichaguliwa hawatakuwa viongozi bora. Makamba akikohoa, watafyata mikia yao. Kama wanachaguliwa kwa maslahi ya makamba na sio ya watanzania, shauri yao hao wanaowapa kura zao.
Mimi na nyumba yangu tutatoa kura zetu kwa wagombea wa chama ambacho kimeonesha tayari mwelekeo wa kutuletea ukombozi watanzania. Nacho sio kingine bali CHADEMA.