Sababu za CCM kukataa midahalo hizi hapa

WANA JF nani anaelewa sababu za msingi hasa zilizopelekea wagombea wa CCM kukatazwa kushiriki midahalo inayoendeshwa na Televition ya CCM aaaah....samahani ya Taifa TBCI ni zipi?

Muheshimiwa Makamba alisema anataka ajue watu wataoshiriki mdahalo sio watu wenye njaa, na vile vile wanataka wajue ni maswali gani yataulizwa, kwa kifupi ccm wanataka kuchakachua hata maswali ya mdahalo.
 
Rev tuongee ukweli, inamaana CCM haiwatendei haki wapiga kura wake, kampeni kila siku unazisikia
CCM wamaebaini kuwa wapinzani wanasubiri tu mdahalo ili wawafikie watu kwakuwa unashirikisha CCM ,kama ndio hivyo siwafanye mdahalo bila CCM uone kamawatapata muitikio

midahalo uwa tunaangalia saana TBC tena bila ccm tatizo lipo wapi bwana tena mwiiitikio nimkubwa saaana!
 
Hamna kitu kama hicho, jamaa walitaka kutumia mgongo wa CCM sasa wameshtukiwa

Mkuu paulss

Ni kweli kabisa walitaka kutumia mgongo wa CCM kujitangaza. Ili kuthibitisha hilo wanahangaika huku na kule kubembeleza CCM wakubali lakini imeshindikana.

CCM inaona mdahalo si kitu cha mkakati kwa ajili ya ushindi, basi anaeona kuwa mdahalo utamsaidia kushinda hana haja ya kuwang'ang'ania CCM watumie fursa hiyo kupata nafuu ya ushindi.

Mwisho, ni wazi kabisa CCM ndiyo bidhaa inayouzika kwa sababu ni nzuri na bora, kwahiyo wanataka kuzichanganya na bidhaa zao hafifu na zisizouzika na zile za CCM wajaribu bahati yao.

Wameshtukiwa, sasa wanalalama.

Hatutaki mdahalo, tunataka kura tu!
 
THE CITIZEN
Capitation policy 'highly flawed'
Friday, 24 September 2010

By Florence Mugarula

The primary school students' capitation grant which was introduced under the capitation grant policy in 2002 has failed to serve its purpose, a survey conducted by Uwazi-Twaweza has established.

Addressing reporters yesterday, the Uwazi-Twaweza managing director, Mr Rakesh Rajani said that the primary school capitation grant needs serious changes to enable students benefit from the policy.

Uwazi is part of Twaweza, a new citizen-centered initiative, focusing on large-scale change in East Africa region.

Mr Rajan said this when revealing the report of a survey on capitation grant. He said the $10 (about Sh14,000) grant a year to each primary school pupil was not enough to buy books and other academic materials and that its value has declined by over 35 percent since it was established about nine years ago.

"It has been established that there was a need to make changes in the whole system so that there could be positive improvement in the education sector," said Mr Rajan.

The analysis report shows that the policy was introduced in order to replace the revenues lost to schools because of the abolition of fees and to improve the quality of education by making real resources available at the school level.

According to the report, at least Sh80 billion was allocated in 2009/10 fiscal year under the Primary Education Development Programme (PEDP) but still there were no enough improvement which reflect the allocated funds.

The report established that the allocation of Sh14,000 ($10) to each pupil has never been adhered and only Sh4,189 has been actually provided for each pupil.

The report reads also that the amount was not enough to the extent that even if it was released in full, it was too small to cover the cost of learning materials.

It added that the actual capitation grant disbursements were less than what was allocated in the budget, and thus it was so unpredictable for proper planning.

The report establishes that the amount allocated in the budget for capitation grants has systematically been lower than the amount stated in the PEDP policy adopted by cabinet.

According to the report, in 2007/08 the shortfall in capitation grant was Sh4,481 per pupil as government allocated Sh5,519 per pupil.

Mr Rajan said that there was a need to revise the policy and allocate more money to enable the implementation of different school programmes.
Commenting on the problems that hinder the development of primary school education in the country, Mr Rajan said the analysis has established also that the allocated money was not delivered on time thus delaying implementation of development programmes.

He added that there was no transparency among teachers, government officials and wananchi in general on the capitation grant.

But the PEDP coordinator from the ministry of Education and Vocation Training, Mr Benedict Mtui told The Citizen that the delay or timing of cash depend on the response of the donors.

According to Mr Mtui, the government always asks for cash from different areas and that it becomes difficult to allocate fund to a particular school if there is no response from the source.

"We fail to provide money on time, and sometimes we offer less amount because we are also receiving money from donors, so some give us on time and other delay or nothing at all therefore that is how this problem happen," said Mr Mtui.

Commenting on the transparency on allocating and using of the fund, Mr Mtui said the reports were published in the government gazette but currently all reports were exposed on the ministry of Finance and Economic Affairs website.

The Uwazi-Twaweza Research analyst, Ms Rose Aiko said the present price for the book was between Sh3,500 and Sh5,000 and that the 40 percent of Sh10,000 which is currently offered by the government was not even enough to buy a single book.

She said, in order to foster education sector, the government must increase the amount of capitation grants to primary school pupils.
According to Twaweza, at least sh 13,000 were needed to each pupil just for buying books alone.


WAKUBWA HII NDIO HALI HALISI YA UTEKELEZAJI ILANI YA CCM YA 2005 PAMOJA NA SERA ZILIZOTUNGWA NA SERIKALI YENYEWE YA CCM HUSUSAN KATIKA SEKTA YA ELIMU.

SERIKALI YA CCM ILIJIPANGIA SERA YAKE YA ELIMU KUWA KAMA IFUATAVYO:- The Education and Training Policy adopted in 1995 sets the policy for the education sector in Tanzania.
The Education sector has a vision for Tanzania to be:
"a nation with high level of education at all levels; a nation which produces the quality and quantity of educated people sufficiently equipped with the requisite knowledge to solve the society's problems, in order to meet the challenges of development and attain competitiveness at regional and global levels".

The mission of the Ministry of Education and Culture in this regard is over achingly to:
"Realise Universal Primary Education (UPE), eradicate illiteracy and attain a level of tertiary education and training commensurate with critical high quality human resources required to effectively respond to the development challenges at all levels".



WAKATI AMBAPO SERIKALI ILIAHIDI KATIKA SERA YA PRIMARY EDUCATION DEVELOPMENT PROGRAMME (PEDP) ILIYOPITISHWA NA BARAZA LA MAWAZIRI (2002) NA SERIKALI YA KIWETE KUAHIDI KUENDELEA KUTEKELEZA AHADI HIZO ILIPOINGIA MADARAKANI MWAKA 2005, KUWA KILA MWAKA SERIKALI ITAMTENGEA KILA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI HAPA TANZANIA DOLA $10 ZA KIMAREKANI SAWA NA SHILINGI 10,000 (2002) AU SHS 14,000 (2010) (KUTOKANA NA KUSHUKA KWA THAMANI YA FDHA YA KITANZANIA) KAMA MATUMIZI YA MWANAFUNZI HUYO KUPATA ELIMU YA MSINGI.

KATIKA YA BAJETI YA 2007/8 SERIKALI YA KIKWETE ILIMTENGEA KILA MWANAFAUNZI SHILINGI 5,519/= TU, KATI YA SHILINGI 10,000/=.FEDHA ILIYOTENGWA INATOSHA KUNUNUA KITABU KIMOJA CHA KUFUNDISHIA KWA BEI ZA MWAKA HUO.

KATIKA BAJETI YA 2009/10 SERIKALI YA KIKWETE ILITENGA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 80 TU KWA AJILI YA ELIMU YA MSINGI SAWA NA SHILINGI 4,189/= TU KWA KILA MWANAFUNZI BADALA YA SHILINGI 14,000/=. KIASI HICHO NI PUNGUFU NA KILE KILICHOTENGWA KATIKA BAJETI YA 2007/8 KWA SHILINGI 1,330/= KWA KILA MWANAFUNZI ILIHALI GHARAMA ZA KILA KITU KILICHATAKIWA KATIKA KUMUELIMISHA MWANAFUNZI ZILIONGEZEKA MARADUFU

NDUGU ZANGU JE HUKU NDIO JAKAYA KIWETE ANAKOITA UTEKELEZAJI WA SERA BORA ZA CCM NA AHADI NA ILANI YA CCM YA 2005?

NDIO MAANA CCM WANAKATAA KUINGIA KWENYE MIDAHALO KUKWEPA KUULIZWA MASWALI JINSI WALIVYOSHINDWA KUELEKEZA RASLIMALI ZA TAIFA KUWANUFAISHA WANANCHI WENGI NA BADALA KUNUFAISHA KIKUNDI KIDOGO CHAA WATEULE NDANI YA CCM.

BADALA YA WAGOMBEA WA UPINZANI NA WANANCHI KUCHEZA NGOMA ZA CCM NA KIKWETE ZA KUTOA NA KUPOKEA AHADI MPYA; NI VYEMA WAGOMBEA WA UPINZANI NA WANANCHI WAKAJIELEKEZA KATIKA SERA ZA CCM ZILIVYOTEKELEZWA KATI YA 2005 HADI 2010 KWA KUWA UTEKELZAJI HUO ULIFANYIKA KWA KUTUMIA RASLIMALI ZA TAIFA. HII ITATUSAIDIA KUPATA MAFUNZO MAZURI JUU YA UWEZO WA CCM NA VIONGOZI WAKE KUSIMAMIA UTEKELZAJI WA SERA, ILANI NA AHADI WANAZOTOA SASA.

KWA KUANZIA TUPITIE SERA ZA ELIMU ZA CCM KAMA ZINVYOONEKANA HAPO HAPO JUU NA TUTAFAKARI YALIYOJITOKEZA KATIKA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU SEKTA YA ELIMU KATIKA GAZETI LA CITIZEN; NA TAARIFA YA UTAFITI MWINGIONE KUWA ZAIDI YA 50% YA WANAFUNZI WANAOMALIZA DARASA LA SABA HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA KISWAHILI, HISABATI NA KIINGEREZA.

KWA HALI HII, JE NI KWELI KUWA CCM NA KIKWETE WANATEKELEZA AHADI, SERA ZAO, ILANI YA CCM YA 2005 KWA UFANISI WA KUTOSHA? AU WANANCHI TUNATAKIWA KUBORESHA USIAMAMIZI WA RASLI MALI ZA TAIFA HILI KWA KUONGEZA UFANISI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LENYE JUKUMU YA KUISIMAMIA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI JINISI INAVYOTUMIA RASLI MALI ZA TAIFA?

WANANCHI WANA MCHANGO MKUBWA SANA KATIKA UBORESHAJI WA USIMAMIZI WA RASLIMALI ZA TAIFA KWA KUPUNGUZA IDADI YA WABUNGE WA CHAMA TAWALA NDANI YA BUNGE NA KUONGEZA IDADI YA WABUNGE KUTOKA KAMBI YA UPINZANI KWA KUWAPIGIA KURA KWA WINGI ZAIDI TAREHE 31 OKOTOBA 2010 KATIKA KILA JIMBO LA UCHAGUZI.

UKO NDIO KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU WA 2010 ZINATAKIWA KUELEKEA ILI RASLIMALI NYINGI ZINAZOTUMIKA KATIKA MCHAKATO HUU ZIWEZE KUWA NA TIJA KWA WANANACHI NA TAIFA HILI, BADALA YA KUTUMIKA KUWAPATIA WANANCHI BURUDANI YA BONGO FLEVA NA AHADI MPYA ZISIZOTEKELEZWA.



maelezo meengi, hamna kitu mmeshtukiwa
 
Mkuu paulss

Ni kweli kabisa walitaka kutumia mgongo wa CCM kujitangaza. Ili kuthibitisha hilo wanahangaika huku na kule kubembeleza CCM wakubali lakini imeshindikana.

CCM inaona mdahalo si kitu cha mkakati kwa ajili ya ushindi, basi anaeona kuwa mdahalo utamsaidia kushinda hana haja ya kuwang'ang'ania CCM watumie fursa hiyo kupata nafuu ya ushindi.

Mwisho, ni wazi kabisa CCM ndiyo bidhaa inayouzika kwa sababu ni nzuri na bora, kwahiyo wanataka kuzichanganya na bidhaa zao hafifu na zisizouzika na zile za CCM wajaribu bahati yao.

Wameshtukiwa, sasa wanalalama.

Hatutaki mdahalo, tunataka kura tu!
Yuo make ma day
 
icon1.gif
Ccm kukimbia midahalo ni upom pompo au?


WANA JF nani anaelewa sababu za msingi hasa zilizopelekea wagombea wa CCM kukatazwa kushiriki midahalo inayoendeshwa na Televition ya CCM aaaah....samahani ya Taifa TBCI ni zipi?


Soma post no 1, utaelewa tu
 
Hata ningekuwa mimi kwenye mdahalo hamnipati, angalia list hii, RICHMOND, RADAR, MEREMETA, IPTL, NDEGE YA RAIS, EPA and the list goes on...
 
Nionavyo mimi kukimbia kwa ccm kwenye idahalo mbalimbali ni nafasi nyingine nzuri ya vyama vya wapinzani kupata ushindi mnene hapo 31 oct 2010.

Safi sana ccm kwa kumsikiliza role model a.k.a mentor wenu Yusufu Makamba kwamba msishiriki!
:tongue:
 



vijisenti.jpg

INGAWA midahalo baina ya wagombea ni jambo jema, kwa wengine, hasa wasio na kitu cha kuonyesha wapiga kura, ni jambo la hatari.

Kupitia midahalo, chama hata mgombea huweza kuwashawishi wapigakura kwa kujibu maswali yao makuu. Kupitia midahalo, mipango, vipaji, sera, historia, weledi, uoza na hata umahiri wa wagombea na vyama vyao, huwekwa wazi mbele ya wapiga kura.

Kwa mgombea au chama ambalo kiliishachafuka au kutopea kwenye shutuma lukuki, tena za kutisha na kuchusha, midahalo ni sawa na moto, huku wao wakiwa wamejipaka petroli.

Kwa kutambua hatari na hali hii, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewapiga marufuku wagombea wao kushiriki midahalo.

Hata hivyo, hii ni dhuluma na hujuma kwa demokrasia. Kwani kufanya hivyo ni kujiangalia binafsi na kuupuuzia umma ambao chama hicho kinadai kuupigania na kutaka kuuongoza.

Midahalo haijaanzia Tanzania. Hata nchi zinazotufadhili hutumia midahalo kuonyesha kufaa au kutofaa kwa wagombea wa nafasi za uongozi.

Hivyo kutoshiriki ni sawa na kuturejesha kwenye zama za kiza za chama kimoja. Ni aina fulani ya ubabaishaji na kushindwa kwa wazi.

Zuio hili lilianza baada ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuonyesha wazi kukacha midahalo kwa sababu anazozijua mwenyewe na chama chake.

Wengi hawakushangaa hili kutokana na kujua hali ambayo CCM na mgombea wake wanakabiliana nayo katika uchaguzi huu. Wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite.

Hata hivyo tukirejea historia ya ugombea wa Kikwete, hatutashangaa kukacha midahalo hadi sasa kuingiza hata wagombea wengine wa chama chake.

Alianza mchezo huu mwaka 2005 alipopitishwa kwa kishindo na ushabiki baada ya wengi waliompinga kuchafuliwa vibaya.

Kwa wanaojua uwezo wa Kikwete na hali inayokikabili chama chake, hasa tuhuma za ufisadi, ingekuwa sawa na kujinyonga kama wangeridhia kushiriki midahalo.

Wangeshiriki na lipi la maana ambalo CCM wangewasilisha kwa wapigakura? Je, ingetokea wakaulizwa maswali muhimu na chokonozi, wangejibu nini?

Kwa mfano, kama wananchi wangemuuliza juu ya yeye na chama chake kunufaika na fedha za umma zilizoibwa na kampuni ya Kagoda, Kikwete angejibu nini?

Au, kama baadhi ya vyama vingekuja katika mdahaho huo na nyaraka zinazoonyesha majina halisi ya wakwapuaji wakiwamo vigogo wa serikali, Kikwete na chama chake wangesemaje?

Angeelezwa kwamba fedha hizo zilizoibwa katika fuko la madeni ya nje (EPA) zilitumika kumuwezesha kuingia madarakani chini ya jinai ya takrima, angeeleza nini?

Hivi Kikwete angejibu nini kama angeulizwa chanzo cha fedha zinazomwezesha mke wake kumpigia kampeni, ukiachia mbali madai ya matumizi ya mali na fedha za umma katika kufanya hivyo?

Bila shaka Kikwete angeulizwa mantiki ya mkewe, kwa mfano, kuanzisha NGO baada ya yeye kuingia madarakani. Angeulizwa kwa nini mke wake anayelindwa na fedha za umma anatumikia chama kimoja?

Swali jingine ambalo lingempiga chini na kumuacha uchi bila shaka lingekuwa juu ya ahadi zake za kuwapeleka Watanzania Kanani ambazo alitoa mwaka 2005 asitekeleze hata moja.

Pia swali juu ya ni vipi atatekeleza ahadi nyingine mpya lukuki anazozidi kutoa lingemuacha hoi mbele ya wapigakura kiasi cha kupunguza kura zake.

Hapa halijaulizwa swali moto kabisa kutokana na tukio la hivi karibuni la Shehe Yahya Hussein kuahidi kumpa ulinzi wa majini, tena katika karne ya 21 ya sayansi na teknolojia, ilhali anao walinzi wanaolipwa mabilioni ya shilingi.

Pia wengi wangetaka aeleze ni vipi alichezewa hadi kuanguka kama alivyodai Hussein bila kusahau kumbana aeleze ni kwanini Hussein amegeuka msemaji wake.
Angeulizwa kwa nini Yahya anaingilia mambo yanayopaswa kutolewa maelezo na yeye Kikwete au daktari wake na asimkemee, kama kweli hajamtuma kujenga hofu kwa Watanzania?

Hivyo basi, CCM imekataa kuweka shingo lake kitanzini na kufa ikijiona, ingawa hili si jibu mujarabu. Kwani wengi wamefanikiwa kuona woga wa chama hiki kiasi cha kushindwa kuiamini CCM-mwoga kuendesha taifa lao.

Kuna maswali mengine ambayo yangemsumbua hata kumuumbua Kikwete.

Kwa mfano, kama angeulizwa mantiki ya mwanae Ridhiwan kuwa na nguvu katika chama; unadhani angejibu nini?

Najua wanaohoji wasingekuwa na ubavu wa kumuuliza maswali makali kama haya. Bali wagombea wenzake hasa Dk. Willibrod Slaa angeyachomeka ili yapate majibu kwenye kadamnasi.

Kwa vile kugoma kushiriki midahalo kwa CCM kumewanyima wananchi haki yao ya kuchambua sera na mipango yao, kuna haja ya kuiogopa CCM kama ukoma.

Hakika kama chama hicho kimekosa hata mawazo ya kuwaeleza wananchi, kitapata wapi msuli wa kuwa na matendo ya kuwafikisha watakako?

Leo, Kikwete anajitahidi kuwaaminisha Watanzania kuwa atawavusha wakati pesa ya umma, licha ya kutumika vibaya, inaibiwa kila uchao?

Rejea kugundulika kwa wizi wa Sh.1,700,000,000 (trilioni moja na milioni mia saba) uliofichuliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kuwa ulifanyika ndani ya mwaka jana tu.

Fedha hizi ni sawa na takriban moja ya tano ya bajeti ya Tanzania ambayo ni trilioni 11.

Kupitia midahalo, wengi wangetaka kusikia majibu ya Kikwete, hata wagombea wengine, juu ya mantiki, kwa mfano, ya kupitisha wagombea wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali, kama vile ufisadi na kughushi vyeti ukiachia kutoa rushwa ambayo inasemekana imetolewa na wagombea wengi, kama sio wote, wa CCM.

Aidha, wengi wangetaka kumsikia Kikwete akielezea mipango yake ya kuvunja urafiki na watuhumiwa wa ufisadi ambao wamekuwa wakijisifu kuwa urafiki wao hauwezi kuvunjwa na vyombo vya habari.

Wengi wangetaka kusikia tathmini binafsi ya Kikwete ya utawala wake ulioonyesha wazi kulegalega na kufumbia macho ufisadi kiasi cha imani kuanza kujengeka kuwa CCM inaendeshwa na mafisadi.

Kwa jumla, maswali ambayo yangemuweka Kikwete msalabani kama angeridhia kushiriki midahalo, ni gunia.

Hapa CCM imekiri wazi udhaifu na utupu wake. Hakika, imedhihirisha kuwa imeisha na kuishiwa, ukiachia mbali kuwa mshiriki wa jinai na kuendeshwa kwa mawazo mgando yanayopingana na mambo ya kisasa kama midahalo.

Je, kwa hili, hukumu ya wapiga kura itakuwa kali kiasi gani? Tungoje tushuhudie ambacho hatukutegemea. Kuna uwezekano watu wasiamini masikio na macho yao huko tuendako.
Chanzo: Mwanahalisi Septemba 15, 2010.

Free Thinking Unabii: Midahalo ya wazi itaiumbua CCM
 
Kuna swala la afya pia. Mtu anayeanduka hovyo hovyo bila pressure yoyote ataweza kustahimili presuure za midahalo? Anaweza kufa kabisa.
 
Kunaweza kutafsiriwa ifuatavyo.
1. Kulwepa mdahalo ni kutokujali hoja za watu na kung'ang'ania zako tu.
2. Ni kuonyesha kuwa hauko tayari kusikia maoni wala maswali ya wengine.

3. Ili kuweza kujua mgombea atakayetimiza matakwa ya wapiga kura, wajibu maswali na hoja anazopewa.
4. Mgombea anaponadi tu ilani ya Chama chake bila ya kuweza kueleza uwezo wa binafsi hawezi kuaminiwa na wananchi kwani hatujui kama anaamini ilani ambayo hakushiriki kuitunga.
5. Uwezo wa mtu na yaliyomo akilini na moyoni mwake hujulikana kwa kueleza msimamo wake wa binafsi juu ya hoja.
6. Kushindwa kuhudhuria midahalo ni kutaka kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
7. Hata kama mbuzi aliyeko kwenye gunia anafaa lakini kwa kuwa huna uhakika naye ni afadhali umchukie unayemuona.
NI AFADHALI KUJUA KUWA MBUZI WAKO ATATOA MAZIWA KIDOGO KULIKO ALIYE KWENYE GUNIA AMBAPO UNAWEZA KUKUTA NI BEBERU wakati unahitaji atakayezaa
MSINUNUE MBUZI KWENYE GUNIA.
 
Kunaweza kutafsiriwa ifuatavyo.
1. Kulwepa mdahalo ni kutokujali hoja za watu na kung'ang'ania zako tu.
2. Ni kuonyesha kuwa hauko tayari kusikia maoni wala maswali ya wengine.

3. Ili kuweza kujua mgombea atakayetimiza matakwa ya wapiga kura, wajibu maswali na hoja anazopewa.
4. Mgombea anaponadi tu ilani ya Chama chake bila ya kuweza kueleza uwezo wa binafsi hawezi kuaminiwa na wananchi kwani hatujui kama anaamini ilani ambayo hakushiriki kuitunga.
5. Uwezo wa mtu na yaliyomo akilini na moyoni mwake hujulikana kwa kueleza msimamo wake wa binafsi juu ya hoja.
6. Kushindwa kuhudhuria midahalo ni kutaka kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
7. Hata kama mbuzi aliyeko kwenye gunia anafaa lakini kwa kuwa huna uhakika naye ni afadhali umchukie unayemuona.
NI AFADHALI KUJUA KUWA MBUZI WAKO ATATOA MAZIWA KIDOGO KULIKO ALIYE KWENYE GUNIA AMBAPO UNAWEZA KUKUTA NI BEBERU wakati unahitaji atakayezaa
MSINUNUE MBUZI KWENYE GUNIA.

Wnaogopa JK kuanguka katikati ya makombora ya Slaa!
 
Kunaweza kutafsiriwa ifuatavyo.
1. Kulwepa mdahalo ni kutokujali hoja za watu na kung'ang'ania zako tu.
2. Ni kuonyesha kuwa hauko tayari kusikia maoni wala maswali ya wengine.

3. Ili kuweza kujua mgombea atakayetimiza matakwa ya wapiga kura, wajibu maswali na hoja anazopewa.
4. Mgombea anaponadi tu ilani ya Chama chake bila ya kuweza kueleza uwezo wa binafsi hawezi kuaminiwa na wananchi kwani hatujui kama anaamini ilani ambayo hakushiriki kuitunga.
5. Uwezo wa mtu na yaliyomo akilini na moyoni mwake hujulikana kwa kueleza msimamo wake wa binafsi juu ya hoja.
6. Kushindwa kuhudhuria midahalo ni kutaka kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
7. Hata kama mbuzi aliyeko kwenye gunia anafaa lakini kwa kuwa huna uhakika naye ni afadhali umchukie unayemuona.
NI AFADHALI KUJUA KUWA MBUZI WAKO ATATOA MAZIWA KIDOGO KULIKO ALIYE KWENYE GUNIA AMBAPO UNAWEZA KUKUTA NI BEBERU wakati unahitaji atakayezaa
MSINUNUE MBUZI KWENYE GUNIA.

Nimeipenda kweli hii sredi!!
 
MI NASHANGAA SANA KWA WALE NDUGU ZANGU AMBAO WANAMKUMBATIA BABA YAO CCM,MI HUA NAJIULIZA KIKWETE YUPO MADARAKANI KWA 5YRS KWAHIYO YUPO KWENYE SYSTEM ANAJUA VITU VYOTE VINAVYOENDELEA KAMA RAIS LAKINI HAJIAMINI KUTOKANA NA GENTLEMAN YAKE KUKAA KITI KIMOJA NA WASOMI WA JUU DR. SLAA NA LIPUMBA NA HIYO YOTE NI KWASABABU ANAJUA UCHAFU ALIOUFANYAIKIWEMO;
1.KUKUMBATIA MAFISADI AMBAO NI MASWAHIBA WAKE.
2.KWENDA KUBEMBEA CANADA NA MKE WAKE WAKATI AMEACHA WANANCHI WANAISHI CHINI YA DOLA MOJA NA WAZEE WANANYANYASIKA KILA SIKU.
3. ANAONGEA KWA MIPASHO SANA KIASI SHERIA ANATUNGA YEYE ALAFU ANAIKANYAGA MWENYEWE.
4. ANAJUA FIKRA AHADI NYINGI ALIZOZIHAIDI 2005 AJATEKELEZA.
Ni hayo tu na mengineo mengi
 
MI NASHANGAA SANA KWA WALE NDUGU ZANGU AMBAO WANAMKUMBATIA BABA YAO CCM,MI HUA NAJIULIZA KIKWETE YUPO MADARAKANI KWA 5YRS KWAHIYO YUPO KWENYE SYSTEM ANAJUA VITU VYOTE VINAVYOENDELEA KAMA RAIS LAKINI HAJIAMINI KUTOKANA NA GENTLEMAN YAKE KUKAA KITI KIMOJA NA WASOMI WA JUU DR. SLAA NA LIPUMBA NA HIYO YOTE NI KWASABABU ANAJUA UCHAFU ALIOUFANYAIKIWEMO;
1.KUKUMBATIA MAFISADI AMBAO NI MASWAHIBA WAKE.
2.KWENDA KUBEMBEA CANADA NA MKE WAKE WAKATI AMEACHA WANANCHI WANAISHI CHINI YA DOLA MOJA NA WAZEE WANANYANYASIKA KILA SIKU.
3. ANAONGEA KWA MIPASHO SANA KIASI SHERIA ANATUNGA YEYE ALAFU ANAIKANYAGA MWENYEWE.
4. ANAJUA FIKRA AHADI NYINGI ALIZOZIHAIDI 2005 AJATEKELEZA.
Ni hayo tu na mengineo mengi

Too Junior...Karibu Jamvini
 
Back
Top Bottom