Sababu ya wengi "kuwapotezea" wana baada ya kufanikiwa

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Hali gani ndugu zangu?

Malalamiko na vilio vimekuwa vingi sana. Wengi waliofanikiwa wamewa ditch yaani wamewasahau na "kuwapotezea" kabisa wale waliokuwa nao hali moja wakati wa mapambano.

Wale waliokuwa masikini wenzao hawataki tena mazoea nao baada ya kufanikiwa kwao. Hali ni tete.

Ni kama wakati wapo low walikuwa beneti ila baada ya mmoja kati yao au wachache kuchomoka, basi anakata mawasiliano na wenzake.

Sababu kubwa ya haya ni ROHO MBAYA. Huyu don aliyetoboa anakumbuka namna yeye na wenzake wakati wakiwa low profile, namna walivyokuwa wakiwajadili na kuwafanyia husuda, majungu, na fitina wale waliofanikiwa kuliko wao.

Kumbu kumbu hizi zinamfanya ahitimishe kuwa kwa roho mbaya za masikini, hata yeye akirudi kuwa nao beneti watamfanyia majungu na fitina na hata kumshusha kabisa. Hivyo anawakacha wenzake mazima.

Rejea mifano kama ya Fid Q kwa Rado, Diamond na wengineo wengi. Hawataki mazoea na masikini. Masikini wana husuda, wana roho mbaya hatari, mbaya zaidi bila sababu na hawahitaji uwachokoze, wewe ukiishi vema na kunawiri basi tayari umeshawachokoza.

Hata kwenye kuomba kazi kwa nyie vijana, msiende kutega connection vitongoji vya mabosi walala hoi. Vaa pendeza, nenda Posta, nenda Masaki, nenda Mikocheni, nenda maeneo ya Feri hutojutia.

Usitafute connection kwa walalahoi, nao wenyewe wanahitaji misaada kama wewe.

Masikini wana ROHO MBAYA sana.
 
Masikini wanaroho mbaya, we tajiri wawapi, Forbes nafasi yako ya ngapi, kupata Ela za kununua Dona kosa mjini, kuwa na kibanda Cha kukaa na gari a.k.a jeneza tayari ooh masikini wanaroho mbaya, acha kujifariji na kumbuka ulipo toka, ishi na Wana Kama zamani tu.
 
Ni Kama amekugusa Mana haya Ni maumivu yanatoka ndani ya kichwa chako. Ila alichokisema Ni sahihi kabisa Wala sio uwongo. Why mtu ukipata tatizo watu wanafurahia. Mie shuleni nimeshuhudia mtu anachukiwa kisa anafaulu kumzidi jamani.yaani huwa najiuliza why mtu anapopata majanga wengine ndio wanashukuru Muumbaji wao kuwaona,
Pia ukipata mafanikio watu wanatumia na wanamuomba Muumbaji wao awaone ili akushushe wafanane wote. Wakati huyu anacho kigari akiumia ama anaweza akakimbizwa hospital fasta kuliko wote msipokuwa naa gari
 
Masikini wanaroho mbaya, we tajiri wawapi, Forbes nafasi yako ya ngapi, kupata Ela za kununua Dona kosa mjini, kuwa na kibanda Cha kukaa na gari a.k.a jeneza tayari ooh masikini wanaroho mbaya, acha kujifariji na kumbuka ulipo toka, ishi na Wana Kama zamani tu.
Kwa hiyo gari ni jeneza
 
Labda nyie roho zenu na yategemea na mtu na roho yake, kwa hiyo nyie matajiri wa jf mmewapotezea wenzenu ambao Maisha bado Kama kweli endeleeni na mwenendo huo.
 
Hali gani ndugu zangu?

Malalamiko na vilio vimekuwa vingi sana. Wengi waliofanikiwa wamewa ditch yaani wamewasahau na "kuwapotezea" kabisa wale waliokuwa nao hali moja wakati wa mapambano.

Wale waliokuwa masikini wenzao hawataki tena mazoea nao baada ya kufanikiwa kwao. Hali ni tete.

Ni kama wakati wapo low walikuwa beneti ila baada ya mmoja kati yao au wachache kuchomoka, basi anakata mawasiliano na wenzake.

Sababu kubwa ya haya ni ROHO MBAYA. Huyu don aliyetoboa anakumbuka namna yeye na wenzake wakati wakiwa low profile, namna walivyokuwa wakiwajadili na kuwafanyia husuda, majungu, na fitina wale waliofanikiwa kuliko wao.

Kumbu kumbu hizi zinamfanya ahitimishe kuwa kwa roho mbaya za masikini, hata yeye akirudi kuwa nao beneti watamfanyia majungu na fitina na hata kumshusha kabisa. Hivyo anawakacha wenzake mazima.

Rejea mifano kama ya Fid Q kwa Rado, Diamond na wengineo wengi. Hawataki mazoea na masikini. Masikini wana husuda, wana roho mbaya hatari, mbaya zaidi bila sababu na hawahitaji uwachokoze, wewe ukiishi vema na kunawiri basi tayari umeshawachokoza.

Hata kwenye kuomba kazi kwa nyie vijana, msiende kutega connection vitongoji vya mabosi walala hoi. Vaa pendeza, nenda Posta, nenda Masaki, nenda Mikocheni, nenda maeneo ya Feri hutojutia.

Usitafute connection kwa walalahoi, nao wenyewe wanahitaji misaada kama wewe.

Masikini wana ROHO MBAYA sana.
Maisha yakibadilika unakuta watu unaokuwa nao sana ni wale walio kwenye circle yako.
Mimi nawaelewa watu. Ni sawa na wale jamaa zake hashim thabiti waliokuwa wanalalamika eti akija tz haendi kijiweni kwao.
Kuna jamaa yetu ni naibu waziri. Watu wanamlalamikia sana mbona siku hizi hata simu hapokei wala haji kitaa.
Mimi nawambia kuwa maisha yamebadilika sasa hivi anazungumza na mawaziri wenzake na watu wa level hizo hata simu zetu muda mwingine anaona kero tu maana watu wanataka tu michongo utadhani yeye hana familia na watoto wa ndugu zake.
 
Kwa hiyo hako ka sevant kota na ka ist ndio unajiona tajiri sio.

Nikueleze sasa sababu ya kweli kwa nini watu wakifanikiwa wanakuwa mbali na waliokuwa nao nyuma, sababu kuu ni kuwa kila mmoja wakati wa utafutaji anakuwa na ndoto yake na support kwa wakati husika sasa akishatoboa ndoto zake zinasogea mbele hawazi tena alipo ambako wale wa nyuma hawajafika, atatumia mazingira haya mapya na marafiki na support ya wakati huu kufika huko alikopanga so obvious wale wa nyuma hawezi kuwa nao tena beneti.

Au unasemaje tajiri wa mchongo.
 
Back
Top Bottom