Sababu ya CCM kuja na “Surprises” katika teuzi zake mbalimbali ni hii hapa

narumuk

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
1,944
2,000
Ndugu hii ni CCM mpya, CCM.ya JPM
mnakumbuka mlisema JPM kuchaguliwa kuwa rais asingeweza kupambana na ufisadi kwa sababu ya "mfumo"?
Ukweli wa mambo kubali kuwa huijui CCM haswa. Naombea kwa mungu JPM afanikiwe na akifanikiwa upinzani utafutika wenyewe Tanzania. Naona dhamira yake safi ila waliomo ndiyo shida wanaishi kwa kuhujumu chama nikuhakikishie kuwa nimefurahi kumpata SG mpya ambaye mikono yake si michafu.
 
narumuk

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
1,944
2,000
Mukama alishindwa cz hakupata support ya mwenyeki, any reforms have to be supported by the status quo in place! Je magufuli atampa support ya kufanya reforms? Ofcourse,!!
You are pretty right kibarua chao Chairperson and SG ni kizito 80percent ni mikono michafu na remaining 20 percent ni wanafiki
 
zous

JF-Expert Member
Sep 25, 2017
475
1,000
kweli ccm yafanya mambo yake ki sayansi ...na upinzani ukiiga huenda mambo ya kawa mazuri ila wakiendelea na mwendo wao hakuna ataeeza itoa ccm madarakani kwa kwel
 
Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,729
2,000
4C212596-7832-42C8-9317-D956127EFA5B.jpeg
Sina shaka na ulichoandika hapo juu ila hapa mwisho kwenye of course sina uhakika kama ni jibu kwa kingereza changu cha kuungaunga kuna of course yes na of course no.
Usikalili mambo ya yes or no!
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,084
2,000
Mara nyingi tumeshuhudia CCM ikiwashangaza wengi katika teuzi zake mbalimbali, hasa pale ambapo watu ambao hawapewi kipaumbele au kufirikiwa kabisa; wanapoibuka kidedea.

Tukikumbuka mwaka 2015 katika harakati za kumtamfuta mtu ambaye angepeperusha bendera ya CCM katika mbio za Urais, wakati vyama vingi vya upinzani walikuwa hata hawajui ni nani hasa angepeperusha bendera zao; CCM ilikuwa na watia nia zaidi ya 40. Hata hivyo Lowassa na Membe walipewa nafasi kubwa sana kiasi kwamba hata wale tunaowaita “Political Analysts” walituelekeza mawazo na fikra zetu kwa watu hao wawili. Katika hali iliyowashangaza wengi John Pombe Magufuli aliibuka kidedea na hatimaye akachaguliwa kuwa Raisi wa JMT.

Tumeshuhudia pia katika uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM hapo jana tarehe 29/05/2018. Kuna majina mengi sana yalitajwa na wachambuzi kwa kuyatolea sababu kibao, lakini Bashiru Ali Kakurwa akaibuka kidedea na kuwashangaza wengi tena.

Sababu kubwa ni kuwa CCM ina “Hazina Kubwa ya Wanachama” wenye uadilifu na sifa za kuwa viongozi. Mbali na mambo mengine, CCM pia hujikita katika kuwaandaa wanachama wake kuwa na uwezo wa kukiongoza chama hicho pale itakapobidi. Kwa hali hiyo, CCM imeweza kuja na sura tofauti kila kukicha, na pale wananchi wanapokosa imani na sura kadhaa basi CCM huleta sura mpya na hivyo kuwajengea wananchi imani upya.

Ni wakati muafaka sasa kwa upinzani kuiga mfano huu mzuri wa CCM na kuwa na mpango mkakati wa kuwaandaa viongozi. Tabia ya kuwa na “For life leaders” au kupatikana kwa viongozi based on undugu, urafiki na rushwa haitawafikisha mbali. Ni vema sasa tukashuhudia sura mpya katika chaguzi zenu zijazo kama kweli mnataka kudumu katika uwanda huu wa siasa.
Kutukuza kitu au jambo ambalo unajua kwamba halistahili ni utumwa wa kiakili.
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,110
2,000
...Sababu kubwa ni kuwa CCM ina “Hazina Kubwa ya Wanachama” wenye uadilifu na sifa za kuwa viongozi. CCM pia hujikita katika kuwaandaa wanachama wake kuwa na uwezo wa kukiongoza chama..
So Dr. Bashiru Ali Kakurwa amekuwa akiandaliwa na CCM kwa muda mrefu sana ili "aje akiongoze chama pale inapobidi"?
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,219
2,000
Ndugu hii ni CCM mpya, CCM.ya JPM
mnakumbuka mlisema JPM kuchaguliwa kuwa rais asingeweza kupambana na ufisadi kwa sababu ya "mfumo"?
Kabisa, Ndiyo yalikua maneno yao, sasa hivi wamebadilika kuwa JPM anataka kuiuwa CCM
 
Asiye na Chama

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
1,269
2,000
Mara nyingi tumeshuhudia CCM ikiwashangaza wengi katika teuzi zake mbalimbali, hasa pale ambapo watu ambao hawapewi kipaumbele au kufirikiwa kabisa; wanapoibuka kidedea.

Tukikumbuka mwaka 2015 katika harakati za kumtamfuta mtu ambaye angepeperusha bendera ya CCM katika mbio za Urais, wakati vyama vingi vya upinzani walikuwa hata hawajui ni nani hasa angepeperusha bendera zao; CCM ilikuwa na watia nia zaidi ya 40. Hata hivyo Lowassa na Membe walipewa nafasi kubwa sana kiasi kwamba hata wale tunaowaita “Political Analysts” walituelekeza mawazo na fikra zetu kwa watu hao wawili. Katika hali iliyowashangaza wengi John Pombe Magufuli aliibuka kidedea na hatimaye akachaguliwa kuwa Raisi wa JMT.

Tumeshuhudia pia katika uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM hapo jana tarehe 29/05/2018. Kuna majina mengi sana yalitajwa na wachambuzi kwa kuyatolea sababu kibao, lakini Bashiru Ali Kakurwa akaibuka kidedea na kuwashangaza wengi tena.

Sababu kubwa ni kuwa CCM ina “Hazina Kubwa ya Wanachama” wenye uadilifu na sifa za kuwa viongozi. Mbali na mambo mengine, CCM pia hujikita katika kuwaandaa wanachama wake kuwa na uwezo wa kukiongoza chama hicho pale itakapobidi. Kwa hali hiyo, CCM imeweza kuja na sura tofauti kila kukicha, na pale wananchi wanapokosa imani na sura kadhaa basi CCM huleta sura mpya na hivyo kuwajengea wananchi imani upya.

Ni wakati muafaka sasa kwa upinzani kuiga mfano huu mzuri wa CCM na kuwa na mpango mkakati wa kuwaandaa viongozi. Tabia ya kuwa na “For life leaders” au kupatikana kwa viongozi based on undugu, urafiki na rushwa haitawafikisha mbali. Ni vema sasa tukashuhudia sura mpya katika chaguzi zenu zijazo kama kweli mnataka kudumu katika uwanda huu wa siasa.
Mtoa mada naona umekaa kiushabiki wa kivyama badala ya kukita kwenye ukweli ambao ungefanya mada yako ikawa na mvuto zaidi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom