Sababu ya CCM kuja na “Surprises” katika teuzi zake mbalimbali ni hii hapa

Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
450
424
Mara nyingi tumeshuhudia CCM ikiwashangaza wengi katika teuzi zake mbalimbali, hasa pale ambapo watu ambao hawapewi kipaumbele au kufirikiwa kabisa; wanapoibuka kidedea.

Tukikumbuka mwaka 2015 katika harakati za kumtamfuta mtu ambaye angepeperusha bendera ya CCM katika mbio za Urais, wakati vyama vingi vya upinzani walikuwa hata hawajui ni nani hasa angepeperusha bendera zao; CCM ilikuwa na watia nia zaidi ya 40. Hata hivyo Lowassa na Membe walipewa nafasi kubwa sana kiasi kwamba hata wale tunaowaita “Political Analysts” walituelekeza mawazo na fikra zetu kwa watu hao wawili. Katika hali iliyowashangaza wengi John Pombe Magufuli aliibuka kidedea na hatimaye akachaguliwa kuwa Raisi wa JMT.

Tumeshuhudia pia katika uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM hapo jana tarehe 29/05/2018. Kuna majina mengi sana yalitajwa na wachambuzi kwa kuyatolea sababu kibao, lakini Bashiru Ali Kakurwa akaibuka kidedea na kuwashangaza wengi tena.

Sababu kubwa ni kuwa CCM ina “Hazina Kubwa ya Wanachama” wenye uadilifu na sifa za kuwa viongozi. Mbali na mambo mengine, CCM pia hujikita katika kuwaandaa wanachama wake kuwa na uwezo wa kukiongoza chama hicho pale itakapobidi. Kwa hali hiyo, CCM imeweza kuja na sura tofauti kila kukicha, na pale wananchi wanapokosa imani na sura kadhaa basi CCM huleta sura mpya na hivyo kuwajengea wananchi imani upya.

Ni wakati muafaka sasa kwa upinzani kuiga mfano huu mzuri wa CCM na kuwa na mpango mkakati wa kuwaandaa viongozi. Tabia ya kuwa na “For life leaders” au kupatikana kwa viongozi based on undugu, urafiki na rushwa haitawafikisha mbali. Ni vema sasa tukashuhudia sura mpya katika chaguzi zenu zijazo kama kweli mnataka kudumu katika uwanda huu wa siasa.
 
Sio km ccm INA hazina ya wanachama nadhani ni sababu ya kimaslahi zaidi kila ataepewa cheo na ccm lzm akubali.
Wengi wa waliopewa vyeo sasa HV ccm walikuwa wanaipinga mwanzo lkn kutokana na njaa iliopo upinzani MTU akipewa cheo anajua maisha yashanyooka.
Mfano ni polepole,kabudi na katibu wa w/maji.
 
Sky Eclat ingawa tumefurahia Bashiru kuwa SG sasa kazi ndiyo inaanza. Kumbuka anaingia kama Mkama ambaye aliandaa waraka wa kujivua gamba na yeye hakupiga round akawa gamba. Sasa huyu SG mpya ameigia na Gia ya kupambana na mafisadi ndani ya chama. Hii vita ni kali kuliko na ujue huyu si mwenzao alikuwa Nje sijui khali itakuweje ingawa wanyonge tunasuuzika ila ELITES ambao ndiyo walioshika usukani CCM wamechafuka mikono kiasi hata uwe na acid haisaidii njia ni moja tu kuikata! Let’s as usual wait and see
 
Ndugu hii ni CCM mpya, CCM.ya JPM
mnakumbuka mlisema JPM kuchaguliwa kuwa rais asingeweza kupambana na ufisadi kwa sababu ya "mfumo"?
 
Sky Eclat ingawa tumefurahia Bashiru kuwa SG sasa kazi ndiyo inaanza. Kumbuka anaingia kama Mkama ambaye aliandaa waraka wa kujivua gamba na yeye hakupiga round akawa gamba. Sasa huyu SG mpya ameigia na Gia ya kupambana na mafisadi ndani ya chama. Hii vita ni kali kuliko na ujue huyu si mwenzao alikuwa Nje sijui khali itakuweje ingawa wanyonge tunasuuzika ila ELITES ambao ndiyo walioshika usukani CCM wamechafuka mikono kiasi hata uwe na acid haisaidii njia ni moja tu kuikata! Let’s as usual wait and see
Mukama alishindwa cz hakupata support ya mwenyeki, any reforms have to be supported by the status quo in place! Je magufuli atampa support ya kufanya reforms? Ofcourse,!!
 
Sio km ccm INA hazina ya wanachama nadhani ni sababu ya kimaslahi zaidi kila ataepewa cheo na ccm lzm akubali.
Wengi wa waliopewa vyeo sasa HV ccm walikuwa wanaipinga mwanzo lkn kutokana na njaa iliopo upinzani MTU akipewa cheo anajua maisha yashanyooka.
Mfano ni polepole,kabudi na katibu wa w/maji.
Polepole hajawahi kuwa mpinzani japokuwa alikuwa akipinga msimamo wa Serikali mbili.
 
Back
Top Bottom