Sababu wanaume kuwaua wake zao

Sababu wanaume kuwaua wake zao

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
Kunakuwa na mijadala mingi Sana tena iliyokinzani pale ambapo inatokea mume amemuua mke wake wa ndoa.

Sababu ambayo hukimbiliwa na wengi pasipo hata kuwaza sababu nyingine ni hii ya wivu wa mapenzi.

sababu hii haitoshi kuwekwa kwenye kila tukio la mume kumuua mke wake.

Kuna sababu kadhaa zimeabinishwa na watafiti mbalimbali wa mambo ya kijinsia na masuala ya ndoa.

Sababu kuu 4 zinapewa kipaumbele kuwa chanzo cha mauaji kwa wanawake.

Sababu ya kwanza na inayotokea mara kwa mara inatajwa kuwa ni hasira ambapo Wanaume wengi hushindwa kuzuia hasira zao pindi wanapokwazwa na wake zao.

Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wengi huweka moyoni mzigo wa mawazo yanayo tokea kwenye familia na ndoa zao hivyo 'hujilipua' kipindi ambacho wamechoka huamua kuua.

Pia Kuna wale ambao hupata hasira wakiwa nje ya nyumba zao mfano maeneo ya kazi na pindi wanaporejea nyumbani wakikutana na mapokezi mabaya kutoka kwa wake zao huwaua.

Sababu ya pili ni hofu ya kuachika, au kuachwa ambapo baadhi ya Wanaume huwa hawajiamini na uhofia kuachwa na wake zao na huona kitendo hiki kitakuwa aibu na hatari kwao huamua kuwaua wake zao ili wasiaibike.

Utafiti unaonyesha kuwa kundi hili la Wanaume wenye hofu hutokana na Udhaifu binafsi wa kihisia na kutokuwa imara kimtazamo "borderline type".

Pia sababu nyingine inatajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Hii inahusisha mtazamo,hisia na maumivu ya kimawazo na ufahamu ambayo mwanaume anayabeba kwa mke wake.

Hapa mwanaume humuona mwanamke kama chombo chake hivyo akiona dalili za huyo mwanamke kuwa na Uhusiano na mwanaume mwingine huamua kumuua ili wote wakose.

Sababu ya nne iliyofanyiwa utafiti ni Kujiua, ambapo mwanaume humuua mke wake kisha hujiua mwenyewe hivyo hakuna anaebaki wote hufa.

Utafiti unaonyesha kuwa Sababu hizi nne ndizo sababu kuu zinazojibu swali kwanini Wanaume huwaua wake zao.

Na sababu nyingine zote ambazo hujitokeza mara nyingi huzaliwa ndani ya sababu hizi kuu nne.

Sababu zingine ndogo ndogo zilizofanyiwa utafiti ni Ugonjwa wa akili, upweke, uhitaji wa kubadilisha mke.

Na kuna wanaume ambao huwaua wake zao wakijua kuwa ndio suluhisho la matatizo kama vile fumanizi na kutoaminiana.

Sababu nyingine kama ulevi, matumizi ya madawa ya kulevya zinatajwa kuwa husababisha matukio ya mauaji kwa kiasi kidogo sana.

Peter Mwaihola

1653923180265.jpg
 
Na sisi walokole na wahafidhina tunasema, kila nafsi itaonja umauti, "mapenzi ya Mungu", kwamba siku zako zimehesabiwa.

Waswahili tunatamatisha kwa kusema, "kila lenye mwanzo, lina mwisho"

Wanasayansi, wanasubiri autopsy iseme kama baada ya risasi kuzama kichwani, ubongo ulikufa instantly au ulianza kukosa oksijeni, n.k

Itoshe tu kusema, kifo ni uhai kwa lugha tofauti.
 
Yote ya nini ayo mpk kupelekea kutoana roho wakati wote mmekutana vitovu vyenu vilikwishakauka mambo yakibuma kila mtu achukue hamsini zake
 
Kunakuwa na mijadala mingi Sana tena iliyokinzani pale ambapo inatokea mume amemuua mke wake wa ndoa.

Sababu ambayo hukimbiliwa na wengi pasipo hata kuwaza sababu nyingine ni hii ya wivu wa mapenzi. Sababu hii haitoshi kuwekwa kwenye kila tukio la mume kumuua mke wake.

Kuna sababu kadhaa zimeabinishwa na watafiti mbalimbali wa mambo ya kijinsia na masuala ya ndoa. Sababu kuu 4 zinapewa kipaumbele kuwa chanzo cha mauaji kwa wanawake.

Sababu ya kwanza na inayotokea mara kwa mara inatajwa kuwa ni hasira ambapo wanaume wengi hushindwa kuzuia hasira zao pindi wanapokwazwa na wake zao.

Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wengi huweka moyoni mzigo wa mawazo yanayo tokea kwenye familia na ndoa zao hivyo 'hujilipua' kipindi ambacho wamechoka huamua kuua.

Pia Kuna wale ambao hupata hasira wakiwa nje ya nyumba zao mfano maeneo ya kazi na pindi wanaporejea nyumbani wakikutana na mapokezi mabaya kutoka kwa wake zao huwaua.

Sababu ya pili ni hofu ya kuachika, au kuachwa ambapo baadhi ya Wanaume huwa hawajiamini na uhofia kuachwa na wake zao na huona kitendo hiki kitakuwa aibu na hatari kwao huamua kuwaua wake zao ili wasiaibike.

Utafiti unaonyesha kuwa kundi hili la Wanaume wenye hofu hutokana na Udhaifu binafsi wa kihisia na kutokuwa imara kimtazamo "borderline type".

Pia sababu nyingine inatajwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Hii inahusisha mtazamo, hisia na maumivu ya kimawazo na ufahamu ambayo mwanaume anayabeba kwa mke wake.

Hapa mwanaume humuona mwanamke kama chombo chake hivyo akiona dalili za huyo mwanamke kuwa na Uhusiano na mwanaume mwingine huamua kumuua ili wote wakose.

Sababu ya nne iliyofanyiwa utafiti ni Kujiua, ambapo mwanaume humuua mke wake kisha hujiua mwenyewe hivyo hakuna anaebaki wote hufa.

Utafiti unaonyesha kuwa Sababu hizi nne ndizo sababu kuu zinazojibu swali kwanini Wanaume huwaua wake zao. Na sababu nyingine zote ambazo hujitokeza mara nyingi huzaliwa ndani ya sababu hizi kuu nne.

Sababu zingine zilizofanyiwa utafiti ni Ugonjwa wa akili, upweke, uhitaji wa kubadilisha mke.

Na kuna wanaume ambao huwaua wake zao wakijua kuwa ndio suluhisho la matatizo kama vile fumanizi na kutoaminiana.

Sababu nyingine kama ulevi, matumizi ya madawa ya kulevya zinatajwa kuwa husababisha matukio ya mauaji kwa kiasi kidogo sana.

Peter Mwaihola

1669949752229.jpg
 
Kundi linaloongoza kuua wenza wao katika ndoa ni wanawake, wanaume wengi sana wamekufa katika ndoa zao kwa kigezo tu cha 'kulea' watoto kwenye ndoa ambazo zilishavunjika mioyoni, hao wanaochukua sheria mkononi ni wachache sana. Ukitaka kuthibitisha hili tazama idadi ya wajane vs. Wagane
 
Bila shaka tafiti hii ni ya huko nje.

Hapa ndani hatuna tafiti za hivi, hizi hapa taasisi zinaweza toa taarifa za kina;

1.Ustawi wa jamii, wana kumbukumbu nyingi za usurushishi wa ndoa, nk.

2.Dawati la jinsia, wana kumbukumbu nyingi za matukio yaliyolipotiwa kwao, na walioweza kuyatatua.

3.Jeshi la polisi, wakikaa na watu walio ua wake zao wakayasikiliza ya upande wa pili.kuna taarifa nyingi tungepata na zingeweza saidia kuepusha mauaji mengine kutokea.

4. Mhakama, watoe taarifa za kina chanzo cha talaka nyingi, sbb zake zinazo ongoza ni zipi.
 
Back
Top Bottom