Ni kweli kabisa Kamanda!Yaani huwa yanakuwa rafiki yako unapokuwa na kitu tu...Aisee hii micapitalist....Ni zaidi ya ukimwi!
Raslimali bora na yenye thamani kuu ni WATU. Tuanze kwa kuwajenga watu wetu kuwa
-wazalendo,
-wenye mtazamo wa mbali (Vision),
-wanaojitegemea na si wale wanaosubiri serikali iwafanyie vitu
-wenye mipango ya mda mrefu inayooana na mahitaji ya nchi
-wenye elimu bora na ya kisasa inayoendana na mahitaji ya mazingira yaliyowazunguka na si KKK tu.
-watafiti na wagunduzi
-wenyekuthubutu na kupenda kuona matokeo na si kuridhika na maneno matupu
Tukimudu apo basi mengine yanayohusu raslimali kama miundombinuni, usimamizi, uongozi na uwekezaji yatafuata.
mi ningependa afanye summary!Aisee! Ebu kuza kwanza hayo maandishi ili isomeke vizuri!
Sasa nini kifanyike baada ya kuchambua vizuri?Hongera sana mkuu kwa uchambuzi wako mzuri!
Liganga, nakubaliana na wewe mkuu. Pia tunatakiwa kuondoa mawazo mgando ya baadhi ya watu kuamini kila jambo ni lazima lifanywe na serikali, wakisahau kua mimi na wewe ndio serikali na tunaweza kuleta maendeleo tukiwa na UZALENDO
Kwani Tz kuna nini cha ajabu mpaka uhisi unaibiwa? watanzania tuna roho nyembamba sana inayofanana kabisa na hali yetu ya umaskini kiasi cha kuhisi umaskini wetu ni kwa sababu ya watu fulani wanatuibia, jambo ambalo ni ushezi na ni kutokana na uwezo mdogo tulionao wa kufikiria.
Duh hongera kaka kwa uchambuzi wa kitafiti kweli Tanzania sasa tumegeuka uwanja wa mapambano wa Mataifa haya yenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi duniani.
Kwanini mwalimu Nyerere alivyotutoka tu, Tanzania imekuwa kimbilio la wawekezaji kwa kasi ya ajabu? Mimi najiulizaga sipati jibu.
Mheshimiwa umefanya uchambuzi wa kisayansi.
Historia hujirudia yenyewe. Sababu kubwa ya utumwa, ukoloni na hata utandawazi ni manufaa ya kiuchumi kwa mbinu mbali mbali.
Tanzania tupo loosers siku zote. Nchi zote kubwa zinawekeza kwenye tafiti katika nyanja zote, lakini nitolee mfano wa watafiti tunaowadharau sana, yaani anthropologists, hawa hujifunza mila na desturi ya jami, mara nyingi hawa watafiti huishi miongoni mwa watu wanao wajufunza na hasa vijijini. Utafiti huu hutumika kupata wanachotaka kwa jamii kwa kutumia mila na desturi zao. Enzi za Livingstone wa sasa. Inaaminika kila anthropologist ni agenti wa shirika la kijasusi la nchi yake.
Tafiti nyingine ambayo zinafanywa na hawa watu ni Ethnography, hapa mtafiti humjifunza mtu binafsi, kitugani anakipenda, asichopenda, namna nzuri ya kumshawishi nk. labda ili mnielewe ni vizuri niweke mfano wa rais Mkapa. Mkapa kabla ya kuingia kwenye madaraka alikuwa inocent, kwa kweli hakuwa mla rushwa na labda hata yeye anashangaa aliingiaje humo. lakini kwa wanaomfahamu Mkapa ni mtu mwenye kupenda kusifiwa, kutambuliwa na kuthaminiwa. Ni mtu ambaye akikuamini hatasikia ya wenginena hapendi kuwa critisied. Lakini pia ni mtu wa kupenda sana maendeleo na aaonekane amefanya kazi nzuri inayopimika. Sasa angalia jinsi gani walivyoweza kutumia weakness na strength zake ili kufanikisha malengo yao. Makamu mwenyekiti wa globalisation! Misaada waliyo mimina na yeye alivyofunguka. ------,wanamsaidia sana kwa kwendana na interest zake hawa ndio wanatumia mbinu za Carl petro wa leo kwa mangungo wetu Ze mkapa na Mr fast jet
we lazma ni mwana ccmKwani Tz kuna nini cha ajabu mpaka uhisi unaibiwa? watanzania tuna roho nyembamba sana inayofanana kabisa na hali yetu ya umaskini kiasi cha kuhisi umaskini wetu ni kwa sababu ya watu fulani wanatuibia, jambo ambalo ni ushezi na ni kutokana na uwezo mdogo tulionao wa kufikiria.
. Ningependa kidogo muelewe
na ntaweka baadhi yavithibitisho kutoka vyanzoa mbalimbali
nini hasa ni sababu ya safari hii.
KWANZA:.
.Hapa chini
nimeweka linki ya dokumentari ya Aljazeera ambayo inaongelea uporaji ardhi mkubwa na pia naweka
na video ya taarifa za kiintelijensi za mikakati ya mataifa makubwa:
Uporaji ardhi: Our Man in Sudan - Witness - Al Jazeera English
Intelijensia: imeambatanishwa
HITIMISHO:
Kwa waliomudu kutazama taarifa ya habari juu ya mkutano wa Obama na Xi, utaona jinsi Obama
alivyojawa na wasiwasi hata sauti yake ilikuwa kama inatetemeka. Pili mkutano ule haukuwa pale
Washington kama vile viongozi wengine wanapokuwa wameenda USA kukutana na raisi wa Marekani,
mkutano huu unafanyika California, eneo lilipendekezwa na Xi na watu wake. Obama na timu yake
wameitwa kukutana na Xi, na si vinginevyo, Tazama Aljazeera na utaona hata maelezo ya habari hiyo
leo yanaandikwa tofauti. Nimeambatanisha screenshot. China sasa ndio SUPER POWER!!!
View attachment 96829
TAFAKARI:
Kwa kutumia mfano wa timu za mpira (wengi wetu ni wadau)
China = Barcelona (Young, inteligent players, financially sound and ambitious)
USA = Real Madrid (Ageing giant, talented players, financially fit, has lost bearings)
Tanzania = Taifa Stars (Rookie, money-hungry players,ambitious coach -> JK and highly hopeful fans)
.
Pili mkutano ule haukuwa pale
Washington kama vile viongozi wengine wanapokuwa wameenda USA kukutana na raisi wa Marekani,
mkutano huu unafanyika California, eneo lilipendekezwa na Xi na watu wake. Obama na timu yake
wameitwa kukutana na Xi, na si vinginevyo,
Liganga Nimefurahishwa na uchambuzi wako.Isipokuwa nataka nikuulize kuwa mbona sasa ni zaidi ya miaka 55 miongo mingi sana , Tangu wakoloni waanze kuondoka kwenye hili bara la africa na kuwaacha waafrica wajitawale na kujiendeshea mambo yao wenyewe, kwa masikitiko makubwa hakuna walichokibadilisha, hata ile miondo mbinu kidogo waliyotuachia, na baadhi ya viwanda na pamoja na rasilimali nyingi walizotubakishia havijatuongezea kasi yeyote ya maendeleo kwa kasi ukilinganisha na walivyokuwepo wakoloni.(sio kwamba naunga mkono ukoloni).
Kama Tanzania walishindwa kujiendeleza wenyewe takriban miaka zaidi ya 50 tangu uhuru 1961, itawezekana lini kujitambua na kujiendeleza yenyewe bila kutumia haya mataifa makubwa ya nje? Tanzania ya leo yenye watu milioni 46 wanashindwa kujitosheleza chakula kwa mwaka mmoja, achilia mbali kuwa na uwezo wa technolojia kubwa ya kuchimba mafuta, madini na gesi..?