#
Izz,
mwenye kuanzisha thread hii amesahau kitu kimoja ambacho tunakisoma na kukiskiliza kila siku kwenye tvs na radio, kuwa HISTORIA INATABIA YA KUJIRUDIA!, Siku zoote na miaka yote, tokea empire over 2000 yrs ago,
Taifa llt lililoko juu hofu yake kubwa ni ! lisitokee taifa lingine ambalo kwa namna moja au nyingine linaonekana kulishinda lingine,
wakati huo (romans and abisinians and pershians almost 2000 yrs ago) kesi zao zilikuwa hazina tofauti saana na hizi za leo baina ya hawa super powers,
Ukiangalia american na china, wote ni nyuklia power nation{ hapa sio nyuklia ya kutengeneza umeme, LA HASHA, HII NI YA KUUA KWA WINGI INAPOTUMIKA!} KWA HIVO hata mabishano yao hayawi makali kama vile america na cuba, au venezuela inapokuja kwenye threat,
Sasa taifa dogo linapoonekana kuwa tishio basi hawa mabeperiri kama americans and europeans huibana hiyo nchi kuanzia kwenye uchumi na biashara na ikishindikana huitafutia sababu yyt na kuitishia hata kuiingilia kivita, mifano ni mingi tu, north korea, iraq, iran n.k huutangazia ulimwengu ubaya wa kubumba ili kuinyamazisha ,
Lakini kwa nchi km china mbinu hizi haziwezi kufanya kazi, hata fujo inayotokea ndani ya china wamerekani hata comment hawatoi,
Sisi wanyonge ni watazamaji tu, tunaangalia nani atakae endelea kuelea kwenye ulimwengu huu wa ushindani??
Tamaa imeponza mataifa mengi mmno! sisi yetu macho na maji yakizidi unga Mi baba narudi kijijini nikaanze ufugaji tena,