Sababu 6 kwanini sitoenda kuhudhuria mazishi ya mbunge wangu Captain Komba

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,179
2,004
1. Ni mtu ambaye ameifikisha nchi hapa ilipo kwa kusaidia kurubuni maskini wasio na elimu kwa vinyimbo vyake ili waichague CCM na kuwapiga vijembe wapinzani.

1. Ni mtu aliyehamia Dar badala ya kuishi Liuli au hata Nyasa, huku akijua kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi. Tena huko Dar hadi mtaa anaoishi ukapewa jina lake kwa umaarufu wake.

3. Ni mtu aliyetaka kulitumbukiza taifa ktk machafuko kwa kauli yake ya kuwa iwapo rasimu ya katiba ya jaji warioba ingepita "angeingia msituni kupigana".

4. Ni mtu ambaye hakupenda demokrasia hata kidogo na alitusi mara kadhaa vyama visivyo madarakani na kutoa lugha ya kejeli.

5. Ni mtu aliyemtukana sana jaji Warioba kuliko watu wote nchi hii. Alitoa matusi, kejeli na dharau dhidi ya jaji Warioba huku akiwa anajua/hajui kuwa mzee Warioba alikuwa "mjumbe" tu wa kile walichosema watanzania.

6. Mwanae Komba, Fred alijiunga na chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) punde tu alipomaliza kuchukua shahada yake pale SAUT na akamwelezea tabia ya baba yake kuwa ni "MBAYA" na miongoni mwa watu walioichukia demokrasia ni huyu marehemu

kwa lipi nipange safari kwenda nyumbani kumzika huyu jamaa? Sina wivu wala inda kwa ndugu yangu, mbunge wangu wa kule nyumbani wala chuki nae. "Ila ukweli hastahili kupata pole ya kifo wala faraja ya kifo kutoka kwa wazalendo na wapinga ukoloni weusi"

Shukrani a. Ngonyani

Machi 03, 2015

Dar Es Salaam

Ngonyani@naij.com/sirngonyani@gmail.com

+255 784 37 97 99
 
Tatizo hujui kwa nini watu huenda kuzika.Kuhudhuria Mazishi kwa mtu uliyemchukia sana ni muhimu.Uende ukashuhudie anavyozikwa utupie na udongo urudi umefurahi kuwa uliyemchukia kafa kweli na wewe umeshuhudia na kurusha udongo kwa hasira kwenye kaburi lake.

Halafu kafa kwani anakuona kuwa hujaenda kuzika? Wewe utakuwa na ugonjwa wa akili.Naomba yeyote mwenye namba za hospitali ya vichaa mirembe ampe huyu ngonyani amtumie kwenye simu yake ambayo kaiweka wazi.
 
Ngonyani wewe ni mjinga wa kutupwa,Komba kuish Dar na kupeleka huduma kwa wananchi wake haramu,wewe kuishi Dar na kuwatelekeza wazazi wako hapa kijijini halali?. Rudi huku mazazi wako ombaomba sasa hivi, kwanza tulikukuwa hutujui uko wapi asante kwa kufahamisha kuna siku tutawaleta wazazi wako Dar.
 
Shukrani A. Ngonyani

Attention Seeker... Cheap Popularity.. Low Thoughts...
Usitafute umaarufu wa kijinga wewe... Pamoja na yote binadamu atabaki kuwa binadamu tu... Huna haja ya kumuhukumu Komba... Wewe ukiwa kama nani katika mamlaka ya roho... Wewe umetenda mangapi ya kuwaudhi na kuwaharibia maisha toka uzaliwe mpaka hapo ulipo??? Unadhani una utakatifu wa kumuita Komba alikuwa mchafu...

Kama wewe ni Chadema (am inn as well) unadhani mtoto wa marehemu ambae ni Chadema mwenzio akisoma hapa atajisikiaje?? Kuna wakati mwingine tusitafute umaarufu wa kwenye mitandao huku nafsi zikitusuta...

Think before you act!!!!
 
Last edited by a moderator:
Shukrani A. Ngonyani

Lakini Yote Kwa Yote Marehemu Husamehewa Na Hakuna Binadamu Ambaye Ni Malaika Na Hili Kulidhihirisha Hilo Hata Waliokwenda Jana Kumuaga Pale Karimjee Wapo Wengi Tu Aliotuudhi Ila Ki Imani Unatakiwa Kumsamehe Yote Na Tumwombee Tu Akapumzike Kwa Amani. Naamini Hata Wewe Pia Una Mauzauza Yako Kama Binadamu Je Na Wewe Ukiresti Ini Pisi Mimi GENTAMYCINE Nisije Kubeba Jeneza Lako, Kukutupia Udongo Na Kukusindikiza Na Shada La Maua? Tupunguze Chuki Za Ki Palestina Na Za Ki Mujahidin!
 
Last edited by a moderator:
Katika yote, hili namba tano la kumtukana Jaji Warioba na kutoa kejeli na dharau dhidi ya Jaji Warioba huku akiwa anajua/hajui kuwa mzee Warioba alikuwa "mjumbe" tu wa kile walichosema Watanzania linatia hasira sana.
 
mama makinda amemuombea MSAMAHA JANA

Kama alikuwa anajua kwamba alichokuwa anafanya ni makosa, mbona hakumkemea kipindi kile wakati marehemu akipotoka? Au alimwacha tu aendelee kuharisha kwa faida ya chama? Huyu mama ni mnafiki.
 
Lakini Yote Kwa Yote Marehemu Husamehewa Na Hakuna Binadamu Ambaye Ni Malaika Na Hili Kulidhihirisha Hilo Hata Waliokwenda Jana Kumuaga Pale Karimjee Wapo Wengi Tu Aliotuudhi Ila Ki Imani Unatakiwa Kumsamehe Yote Na Tumwombee Tu Akapumzike Kwa Amani. Naamini Hata Wewe Pia Una Mauzauza Yako Kama Binadamu Je Na Wewe Ukiresti Ini Pisi Mimi GENTAMYCINE Nisije Kubeba Jeneza Lako, Kukutupia Udongo Na Kukusindikiza Na Shada La Maua? Tupunguze Chuki Za Ki Palestina Na Za Ki Mujahidin!
Kama marehem husamehewa,mbona tunagubiriwa kuna adhabu kwa Mungu?watu waish kwa adabu,na liwe fundisho kwa wenginw,Kifo ni Mawaidha
 
Duh! Mkuu unagonga kunako. Yale majitu ya maji ya bendera yatakuja kuhara hapa eti oooh marehemu asijadiliwe. Hatumjadili marehemu tunajadili mawazo yake.
 
Kama alikuwa anajua kwamba alichokuwa anafanya ni makosa, mbona hakumkemea kipindi kile wakati marehemu akipotoka? Au alimwacha tu aendelee kuharisha kwa faida ya chama? Huyu mama ni mnafiki.
Aaaah,sasa ataanza kuwakemea wapuuz wote
 
Ebu naomba na wewe ututajie sababu ambayo kila mtu wa itikadi tofauti ataikubali, ni kwa nini na wewe ukifa watu tuje tukuzike?

Acha fikra mgando na kujionesha hadharani ulimbukeni wako. Hata mimi pia kiitikadi nipo tofauti kabisa na marehemu, lakini sio hivyo
 
Back
Top Bottom