Sababu 6 kwanini sitoenda kuhudhuria mazishi ya mbunge wangu Captain Komba

Marehemu huyu kazi anayo...

Akiwa hai aliandamwa, sasa ni marehemu bado anaandamwa...

Kazi kweli kweli...
 
Shukrani A. Ngonyani

Attention Seeker... Cheap Popularity.. Low Thoughts...
Usitafute umaarufu wa kijinga wewe... Pamoja na yote binadamu atabaki kuwa binadamu tu... Huna haja ya kumuhukumu Komba... Wewe ukiwa kama nani katika mamlaka ya roho... Wewe umetenda mangapi ya kuwaudhi na kuwaharibia maisha toka uzaliwe mpaka hapo ulipo??? Unadhani una utakatifu wa kumuita Komba alikuwa mchafu...

Kama wewe ni Chadema (am inn as well) unadhani mtoto wa marehemu ambae ni Chadema mwenzio akisoma hapa atajisikiaje?? Kuna wakati mwingine tusitafute umaarufu wa kwenye mitandao huku nafsi zikitusuta...

Think before you act!!!!

Mwenzako was bold enough to call a spade a SPADE. You may ask yourself Makinda anaomba msamaha kwa ajili yake kwa LIPI? Surely ni katika hizo sababu alizotoa mleta mada.


cc Shukrani A. Ngonyani,
 
Last edited by a moderator:
jamani Ishu ya msiba na kumzika marehemu si ya kuijadili kabisa yani,..Katika sehemu moja wapo ambayo unatakiwa kuonesha Utu wako kama mwanadamu ni kushiriki katika misiba na maziko!
sasa Usijaribu kumsema mtu hujui kesho yako itakuwaje Jamani!!

Imagine wewe ni kibaka mzoefu, mtaani kwenu kila mtu umemjeruhi kwa kumuibia au kumpiga. Sasa umekufa. Unataka mtaa wote walie kwamba marehemu alikuwa mtu mwema? Eti wasiseme kuwa angalau SASA tutapumua na vipigo?

Kama umeboronga katika mahusiano na wenzako UKIWA HAI kwanini utegemee hisani ukiwa MFU?
 
Imagine wewe ni kibaka mzoefu, mtaani kwenu kila mtu umemjeruhi kwa kumuibia au kumpiga. Sasa umekufa. Unataka mtaa wote walie kwamba marehemu alikuwa mtu mwema? Eti wasiseme kuwa angalau SASA tutapumua na vipigo?

Kama umeboronga katika mahusiano na wenzako UKIWA HAI kwanini utegemee hisani ukiwa MFU?

Hata kama Marehemu alikosea vipi?Ila kuwa japo na chembe ya utu sio suala la kufundishwa.,Ila ninachokiona sasa ubinadamu umetutoka.
 
Yote tisa, Kumi ni ile kauli ya kumkejeli Mzee wetu Jaji Warioba. kweli kifo huwa ni siri kubwa - kama angepata walau dakika moja tu kabla ya mauti kumkuta basi angemwita mzee wa watu na kumwambia Sorry!!

Si tu kwa sababu alichosema Jaji ilikuwa ni sauti ya watanzania walio wengi lakini pia ki-umri alimzidi - kweli alimkosema heshima.

Lakini ki-maadili hawa si vizuri kumsema mtu aliyetangulia mbele ya haki - Cha msingi Jaji amsamehe na sisi watanzania wote aliotukwanza tusamehe kisha maisha yasonge mbele - hicho ndiyo Mwenyezi Mungu amekiweka duniani - KUSAMEHEANA.

Hata wewe Ngonyani yote hayo ungeyasamehe na ukajumuika nasi kumpumzisha mwenzetu kwenye nyumba yake ya milele huku kijijini kwake.
 
1. Ni mtu ambaye ameifikisha nchi hapa ilipo kwa kusaidia kurubuni maskini wasio na elimu kwa vinyimbo vyake ili waichague CCM na kuwapiga vijembe wapinzani.

1. Ni mtu aliyehamia Dar badala ya kuishi Liuli au hata Nyasa, huku akijua kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi. Tena huko Dar hadi mtaa anaoishi ukapewa jina lake kwa umaarufu wake.

3. Ni mtu aliyetaka kulitumbukiza taifa ktk machafuko kwa kauli yake ya kuwa iwapo rasimu ya katiba ya jaji warioba ingepita "angeingia msituni kupigana".

4. Ni mtu ambaye hakupenda demokrasia hata kidogo na alitusi mara kadhaa vyama visivyo madarakani na kutoa lugha ya kejeli.

5. Ni mtu aliyemtukana sana jaji Warioba kuliko watu wote nchi hii. Alitoa matusi, kejeli na dharau dhidi ya jaji Warioba huku akiwa anajua/hajui kuwa mzee Warioba alikuwa "mjumbe" tu wa kile walichosema watanzania.

6. Mwanae Komba, Fred alijiunga na chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) punde tu alipomaliza kuchukua shahada yake pale SAUT na akamwelezea tabia ya baba yake kuwa ni "MBAYA" na miongoni mwa watu walioichukia demokrasia ni huyu marehemu

kwa lipi nipange safari kwenda nyumbani kumzika huyu jamaa? Sina wivu wala inda kwa ndugu yangu, mbunge wangu wa kule nyumbani wala chuki nae. "Ila ukweli hastahili kupata pole ya kifo wala faraja ya kifo kutoka kwa wazalendo na wapinga ukoloni weusi"

Shukrani a. Ngonyani
Machi 03, 2015
Dar Es Salaam
Ngonyani@naij.com/sirngonyani@gmail.com
+255 784 37 97 99
___________________________________________________________________________________________

NO PERFECT RELATIONSHIP IN THIS WORLD, AND FORGIVENESS IS SPECIAL WORD TO FILL THE GAP, WHY NI KWA SABABU KILA MTU ANA MTAZAMO WAKE BUT AT LAST WE MUST UNDERSTAND KAMA UNAPENDA KUHUKUMU THIS IS YOUR MESSAGE 'HERI WAPATANISHI MAANA HAO WATAMWONA MUNGU'

KATIKA MAISHA THIS IS THE TRUTH HUTAONDOA CHUKI KWA CHUKI, CHUKI HUONDOLEWA KWA UPENDO.

Give critics according to your professional level!!! Otherwise declare your level!!!
 
Back
Top Bottom