Sababu 5 CCM Kushinda Uchaguzi 2015

Sababu 5 CCM Kushinda Uchaguzi 2015

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Ndugu zangu ni vizuri kuambiana mambo ya msingi haswa linapokuja swala la hatma ya Taifa letu.
Tanzania ni nchi ya kipekee duniani na watu wake ni wa kipekee pia, utu wetu , utanzania wetu huwezi pata sehemu nyingine. Watanzania ni watu wenye upendo, amani na mshikamano huwezi linganisha na nchi yoyote ile. Tumekuwa tukiishi siku zote kwa amani, kupendana na kushirikiana kabla na hata baada ya kuasisiwa taifa letu. Lakini baada ya kuingia siasa za upinzani nchini mwetu , kumekuwa na fikra zenye kuhatarisha amani yetu. Hatukatai upinzani, ndio maana kumekuwa na vyama vingi vya siasa nchini Tanzania. lakini kamwe hatutaruhusu amani yetu kupotea na siasa za kutubagua. Hadi hapa, Amani na maendeleo yaliyopoTanzania yametokana na uongozi wa chama cha mapinduzi. Kuanzia kwa wazee wetu waasisi, na viongozi wetu wakiongozwa na Mwenyekiti wetu, Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa siasa safi na uongozi makini, Sina budi kuzitaja sababu 5 kwa nini chama cha mapinduzi kitashinda uchaguzi wa 2015.

Moja; CCM imeweza kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.
Muhimu kwa watanzania wote kukumbuka kwamba chama cha mapinduzi hakina udini wala ukabila kwa misingi hiyo kimeweza kudumisha amani na umoja wa nchi yetu.

Mbili; CCM imekuwa ya kwanza katika ushirikishwaji wa watanzania wote walio nje ya nchi katika kutoa mchango wao ili kuleta tija na maendeleo ya taifa letu.

Tatu; CCM imehakikisha kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia. Nchini Tanzania kuna demokrasia ya kutosha na hata kupitiliza. Mwananchi yoyote anao uhuru wa kuishi, kuabudu na kufanya maamuzi apendayo ili mradi sheria za nchi zinazingatiwa.

Nne; CCM haina ubaguzi, kila mtu anayo nafasi. Chama cha mapinduzi siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wanawake na wanaume bila kujali rangi, kabila, Dini, au hali ya mtu.

Tano; CCM iko mstari wa mbele katika kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM ambavyo kweli vinapinga Ukoloni, Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.

View attachment 70958
Source: Vijimambo
 
Sihasa za maji taka, ufisadi na makundi ndani ya magamba siyawezi!
 
Huwa napata shida mtu kutueleza maneno yale yale kwa NYAKATI MPYA..omba babu zako wafufuke uendelee kudumisha fikra za WAJINGA.

Fikra za baba wa taifa...
unasema fikra za wajinga!!
 
Bofloooo. Mwanachama mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Uenyekiti imara wa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. HONGERA
 
Bofloooo. Mwanachama mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Uenyekiti imara wa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. HONGERA

Hahaha Elizabeth Dominic , nawachemsha tu wana Jf, I hate politics, sina chama, na sikuwahi kupiga kura
toka nizaliwe, BTW how was Diwali?? Juzi nilidhani nchi imevamiwa, baruti zilipopigwa usiku,jirani zangu wengi ni Baniani
 
Hivi wewe Boflo ni nini leo umetuletea humu asubuhi?

Nina hofu na thread yako na ngoja nitakurudia!
 
Last edited by a moderator:
Tanzania hakuna chama cha Upinzani ila bali ni vyama vya kidini wewe Christian Democratic Movement aka Chadomo.Chini ya katibu wa baraza la Maaskofu padri mla vya watu Slaa.Mkishika hii nchi ujue yesu karudi
 
Tanzania hakuna chama cha Upinzani ila bali ni vyama vya kidini wewe Christian Democratic Movement aka Chadomo.Chini ya katibu wa baraza la Maaskofu padri mla vya watu Slaa.Mkishika hii nchi ujue yesu karudi
Mvaa matineti na gobazi bado unapromot UAMSHO chini ya gaidi Farida na pondwa
 
Ungekuwa shule, na umeulizwa swali kama hilo na mwalimu wako angekupa Ziro!

Udini tanzania haupo! ?

Democrasia gani iliyoimarishwa TZ kuwalipua kina mwangosi?
...

-Kinachotakiwa ni hatua za maendeleo huku mwanachi akiguswa mojakwa moja na maendeleo hayo, mfano kiwango cha vijana wanaopata ajira baada ya kumaliza masomo..
-Uwiano kati ya maliasiri zetu na maendeleo yanayodaiwa kuwepo ni ukoje?
-Ubora wa viongozi wanaotuongoza, je ni kweli ndio wato wenye akili kiliko watz wengi wenye nia ya kuongoza nchi hii? JK, Sophia Simba, Pinda, Mulugo, Kawambwa n.k Je wana akili kweli au wanatuongoza kwa sababu tu mfumo uliopo unatulazimisha tuongozwe nao?

Na mabo kama hayo ya kutumia ubongo kuyatafakari, sio ngonjera za kina Cha nazi!
 
Tanzania hakuna chama cha Upinzani ila bali ni vyama vya kidini wewe Christian Democratic Movement aka Chadomo.Chini ya katibu wa baraza la Maaskofu padri mla vya watu Slaa.Mkishika hii nchi ujue yesu karudi

Ndivyo mlivyo ninyi, hata muende shule vipi lakini ujinga hauwatoki!!
Siwalaumu, mmerithi.
 
Nimeiona hii Habari kwenye Blog ya Vijimambo kwa Dj Luke Joe.
Mwandishi ni Alex Kassuwi.
 
Hahaha Elizabeth Dominic , nawachemsha tu wana Jf, I hate politics, sina chama, na sikuwahi kupiga kura
toka nizaliwe, BTW how was Diwali?? Juzi nilidhani nchi imevamiwa, baruti zilipopigwa usiku,jirani zangu wengi ni Baniani

Divali was fine che. Wewe unawachemsha watu sisi tuna hasira zetu za kutosha na hao jamaa
 
Tanzania hakuna chama cha Upinzani ila bali ni vyama vya kidini wewe Christian Democratic Movement aka Chadomo.Chini ya katibu wa baraza la Maaskofu padri mla vya watu Slaa.Mkishika hii nchi ujue yesu karudi

Punguza jazba.
 
CCM ni baba wa vyama Tanzania hatahivyo inatakiwa itoe darasa kwa vyama vingine ambavyo vinaendeshwa kwa sura za kidini na kikanda wakiwa na lengo la kutugawa wananchi; vyama hivi vimejaa mapungufu:-

1. CUF - Uislam na Ukanda wa Pwani
2. Chadema - Ukristo na Ukanda wa Kaskazini na Uchaga
 
time will tel! kwa sasa wananchi tumeamka na m4c imetupa elimu ya uraia tupo tayari kulinda kura zetu hatuogopi kuuliwa na mabomu, jipangeni jinsi ya kuiba kura maana tumejipanga kulinda.
 
Mkuu Boflo,
Hapa nadhani utakuwa unakosea...unachanganya kati ya WAJIBU wa Serikali na "Siasa/mtazamo binafsi"

Hoja namba moja, tatu na nne (1,3,4) zinafanana tofauti ni kiuandishi TU!!Lakini bado katika hoja hiyo MOJA kuna mapungufu mengi.
-Ni uhuru gani unaouongelea? wa bendera?
-"Walio nje"..A great country utilize what she has, mkuu! Hebu tathmini ni watanzania wangapi walio ndani ya nchi na wale walio nje? Unataka kusema waliondani hawafai, au hawana mwamko na chachu ya maendeleo kuliko wale wa nje?..Sawa, "imewashirikisha walio nje", kina nani hao, kwa mfano? So, far wamefanya nini katika maendeleo ya Taifa(sio CCM)?


"CCM HAKINA UBAGUZI KILA MTU ANAYO NAFASI"
Mkuu katika hili utakuwa si mfatiliaji wa siasa au ni mfatiliaji uliyeanza hivyi karibuni(amateur) na kama siyo haya basi hutaki tu kwa sababu zako ingawa ukweli unaujua...Nikukumbushe, Hivi ni viongozi wa Chama gani waliokubuhu katika kutoa rushwa ili kupata nafasi ndani ya chama?..Kumbuka kule Dodoma, Pale Mwenyekiti wa CCM Taifa(Mh.JM Kikwete) kukubali kuna rushwa ndani ya chama hasa katika uongozi,tena BILA KUCHUKUA HATUA!!..zaidi ni pale aliposema wakiwapatia fedha/rushwa CHUKUENI!!Huyu ni kiongozi?

Something must be wrong with one's mind to convice kuwa CCM inafaa...it can be true, but not in this life time, mkuu.
 
Back
Top Bottom