Saba Saba ni sherehe ya nini?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Jana kwa wakazi wa Tanzania ilikuwa ni siku ya mapumziko/SIKUKUU. Japo mtu binafsi alikuwa na hiari ya kwenda anakotaka na kufanya shughuli anayotaka bila kubughudhiwa ilimradi havunji sheria.

Swali ninalo jiuliza tunasheherekea Saba Saba zama hizi kwa nini? Ikiwa kama mtu ataoanisha na kuzaliwa kwa TANU ajaribu kukumbuka kuwa mwaka 1992 tuliingia mfumo wa vyama vingi, ndipo pia tulipoua shereha zote za kichama kuhesabiwa kama shereha za kitaifa.

Mwaka jana niliuliza swali hilo nikapata majibu kadhaa, lakini bado mtima wangu haujaridhika. Watanzania wenzangu, kesho itakuwa siku ya mapumziko ya Sabasaba. Je! tunapumzika tukisherekea ninI?
 
ni maadhimisho ya siku ya maonyeso ya bidhaa na shughuli mbalimbali

Mbona ni wa Dar es salaam tu ndiyo wanaokwenda kwenye sherehe hizo wa Mbeya,Kigoma,Mwanza na Mara inawahusu nini?
MBONA NAO WANAPUMZIKA?
 
Ilianza kama sabasaba kweli kuadhimisha TANU ilipozaliwa tarehe 7/7/54.
Kinachoshangaza ni kwamba haya maonyesho ambayo sasa yanaitwa ya kimataifa ya biashara yanahudhuriwa na watoto na watu wenye kununua vitu kama ndoo za plastiki na masufuria!
Kwanini tusiende kazini sijaelewa!
 
Huwa huendi kazini? mhhhh siamini
 
Sikukuu ya Manyesho ya Biashara ya Kimataifa

imebadlishwa na kuwa

Siku ya kutembelea Wilaya ya Temeke na Kukesha tukinywa na Kula Viwanja vya Sabasaba
 
Ilianza kama sabasaba kweli kuadhimisha TANU ilipozaliwa tarehe 7/7/54.
Kinachoshangaza ni kwamba haya maonyesho ambayo sasa yanaitwa ya kimataifa ya biashara yanahudhuriwa na watoto na watu wenye kununua vitu kama ndoo za plastiki na masufuria!
Kwanini tusiende kazini sijaelewa!

Ni kweli wengi wanashangaa na wengi hatuelewi vizuri, hebu tusubiri majibu ya ndugu zetu.
 
Siku tanayotakiwa kwenda kuona au kununua bidhaa zinazopatikana nchini kwa kuwa hapo biashara nyingi huenda kujijulisha. nisiku muhimu kwa wafanyabiashara manake watuwengi huenda huko na kujionea vitu vipya vilivyoletwa. yalemakampuni mazembe ndo yanadoda huko lakini yale yanayowajibika huvutia sana kuona utenaji wake kazi.
 
Kwenda kwenye maonyesho ni kwa baadhi ya watu wa Dar tu. Baadhi kwa sababu ktk watu zaidi ya milioni 3, ule uwanja hauwezi chukua hata laki 3. Je! Wanaoishi mikoani wanakwenda wapi? Kama ni biashara na maonyesho ya huko kwanini isiwe kwa watu wa DAR tu?
 
Hayo maonesho siyo ya kwaajili ya Dar tuu watanzania wote wa pembezote wanaweza leta bizaazao zitambulike. Kuna makundi mengi tuu ya mikoani wanaojipangaga kama kikundi na kuleta bizaa zao hapo na wanafaidikaga sana kwa sababu ya ile idadi ya watu wanaoendaga huko. Nakushauri mkuu uende huko ujionee mwenyewe na usikie stories za wajasirimali na uone bizaa zao waweza jifunza mengi
 
Siku ya kuuza na kununua bidhaa za viwandani isipokuwa JKT tu pale kwenye bustani yao wameotesha mazao mazuri sana
 
Back
Top Bottom