Saad Gaddaf akamatwa Nigeria.

Saad Gaddaf akamatwa Nigeria.

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
2,411
Reaction score
1,153
Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, kanali Muammar Gaddaf, Saad amekamatwa na maofisa usalama huko nchini Nigeria, habari nilizozipata hivi punde kupitia redio RFA zinasema kwamba, Saad amekamatwa pamoja na baadhi ya maofisa waliokuwa katika serikali ya baba yake, kati ya maofisa hao ni aliyekuwa mkuu wa televisheni ya nchi hiyo. Saad alikimbilia nchini Niger ambako alihifadhiwa huku serikali ya nchi hiyo ikikataa kumkabidhi Tripol. Utawala wa Tripol umetuma ujumbe wake nchini Nigeria ili kuzungumza na serikali ya nchi hiyo ili wakabidhiwe watu hao.
 
kijana pole sana unahukumiwa kwa sababu ya marehemu baba yako.libya imechafuka sasa hakuna maisha tuliyozoea kuyaona.
 
kijana pole sana unahukumiwa kwa sababu ya marehemu baba yako.libya imechafuka sasa hakuna maisha tuliyozoea kuyaona.

Hakika anastahili kupewa pole kwani yanampata majanga sababu yeye ni mtoto Gaddaf, pia inasikitisha sana kuona jinsi viongozi wa kiafrika wasivyokuwa na ushirikiano wa ukweli baina yao zaidi ya unafiki tu. Huyu ni mtoto wa kiongozi mkubwa barani Afrika ambaye enzi za uhai wake alijitahidi kustawisha nchi yake na pia bara la Afrika hasa katika kuleta umoja kwa waafrika. Amefanya mengi tu ikiwemo kuwa mmoja wa waasisi wa Umoja wa Afrika (AU). Tumeona pia ni jinsi gani Marekani ilivyowasaidia waasi bega kwa bega mpaka wakaiangusha serikali yake na mbaya zaidi kumuuwa yeye mwenyewe, lakini wakati wote hayo yakitokea hakuna hata kiongozi mmoja wa Afrika aliyeinua mdomo wake na kuipinga Marekani. Haya sasa na leo taifa la kiafrika linamkamata mtoto wake tena kwenye ardhi ya Afrika!!!
 
Kwanini na sisi huku tusianze kuwatafuta watoto na wajukuu wa akina Ian Smith aliyekuwa kiongozi wa kikoloni wa S. Rhodesia (Zimbabwe) na kuua maelfu ya wapigania uhuru wakiafrika? Vile vile wakamatwe watoto mpaka njukuri za akina Pieter Botha wa Afrika kusini aliyeua si tu waafrika wazalendo wa nchi 'yake' bali alivuka mipaka kwa helikopta za kijeshi na kuua wale waliokimbilia Msumbiji Zambia n.k. bila kuzingatia sheria za kimataifa wala utu?!?! :angry:
 
Mkuu Mike Scofield hayo usemayo ni sahihi kabisa, viongozi wengi wa kiafrika hawana uchungu kabisa na watu wao, ukiona kiongozi wa kiafrika anashadadia kuhukumiwa kukamatwa kiongozi fulani basi ujue mambo hayo yameanzishwa na wazungu ambao wana sababu zao mbalimbali hasa za kimaslahi zaid lakini viongozi wetu hilo hawalioni wakati wazungu hao ndiyo walikuwa vinara wakubwa wa ukatili kwa wazee wetu wa kiafrika, nakubaliana na wewe kwa asilimia mia ila Marehemu Mzee Madiba amewasamehe hao watu!
 
Last edited by a moderator:
kijana pole sana unahukumiwa kwa sababu ya marehemu baba yako.libya imechafuka sasa hakuna maisha tuliyozoea kuyaona.

Maisha yake akirudi Tripoli yatakuwa mashakani sana. Wamevurugukiwa akili ni kuuana tu
 
Back
Top Bottom