Saa ya Ukombozi ni sasa! Tutamkumbuka Rev. Mtikila

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Kuna vitu vinaanza kutokea sasa na immediately unamkumbuka mtanzania mmoja tu, aliyekuwa na uwezo wa kuzuia mambo bila ya kuumizana! None other than the one and only the late Rev. Mtikila!

Sijui hadi leo tungekuwa na kesi ngapi mahakamani dhidi ya Jamhuri!

Sidhani kama angekaa kimya hasa ktk hili la kukopa technolojia toka Rwanda!

Anyway bado tunazo chembe za matumaini na nia njema, ila hili la kutumia wataalam wa Rwanda nadhani linapaswa lizue mjadala wa kitaifa ili Tanzania iridhie! Kama kuna vitu vya referendum basi hili la kuimport wanyarwanda linahitaji mjadala kuliko hata ile mijadala ya bei za mafuta by ewura au nauli elekezi!

Kuna bunge, kama eneo muhimu kwa ajili ya mjadala, Ila pia kuna mahakama (hapa ndipo tunapomkumbuka Mtikila) vinaweza kuwa sehemu sahihi ya kuweka zuio kwa jamhuri isije kufanya makosa!
 
Tatizo nchi inaendeshwa kwa staili ya ONE MAN SHOW.

Mkuu amejipa madaraka ya 'Mungu mtu' ambapo kila analoliagiza yeye litekelezwe bila kutaka kukosolewa.

Ndiyo matokeo ya upigaji marufuku ya uagizaji sukari nje ya nchi, ambapo imesababisha hadi leo bei ya sukari haijastabilize, ambapo baadhi ya maeneo nchini yananua sukari hadi zaidi ya shilingi 5,000 kwa kilo.

Tumeshuhudia janga lingine lililotokana na watendaji wakubwa kufanya kazi kwa HOFU KUBWA ili wampendezeshe Mfalme, hali iliyointroduce VAT kwenye miamala ya mabenki na simu, ambapo imesababisha mtafaruku mkubwa ndani ya jamii.

Hofu hiyo hiyo ya watendaji ndiyo iliyosababisha pia kuintroduce VAT kwa huduma zote za utalii, jambo kitakalosababisha anguko kubwa sana la biashara ya utalii ambayo ndiyo sekta inayoongoza nchini kwa kuliingizia Taifa letu pesa nyingi za kigeni.
 
Back
Top Bottom