Labda nitoe kisa cha kuipenda na kuanza kuijua SEIKO 5 kuwa sio saa ya kimchezo mchezo.
Hii stori niliisikia kwa baba yangu, kuna baba aliachana na mkewe mjini Bagamoyo, na kuamua kuoa mke mwengine, hiki ni kisa cha kweli kabisa.... Huyo mwanamke aliyemuacha alishazaa naye... Alikuwa na asili ya kiarabu.
Huyo aliyemuoa mara ya pili alikuwa ni mzaramo... Na hawakubahatika kupata mtoto... Walihangaika sana... Lakini Mungu hakuwajaalia mtoto.... Kwa kuwa yule baba alikuwa na mali nyingi.... Yule mwanamke roho ya wivu ikamuingia.... Akajua yule baba atakapokufa atakuwa hana chake.... Akaona ni bora amuue.
Kwa kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba yenye fensi... Alichukua mchi wa kutwangia na kumpiga mumewe kichwani.... Mumewe alipoanguka akamburuza mpaka kwenye kisima na kumtia... Akakata miti iliyoko uwani na kuifunika kwa juu.
Asubuhi kulipopambambazuka... Akawaita vijana waweke zege kwenye kisima kwa madai kumeingia mbwa na amefia huko.
Muda mrefu ukapita... Majirani kila walipomuuliza kuhusu mumewe... Kwa kuwa alikuwa mtu wa kusafiri... Mfanyabiashara... Aliwajibu tokea asafiri ni muda mrefu hajarudi.
Miaka ikakatika bila kutokea wa kuitambua hiyo siri.... Ndipo mtoto wake wa kiume kutoka uarabuni alipokuja kumtembelea baba yake... Alipofika nyumbani kwa mama yake wa kufikia hakumkuta baba yake... Akawa kila wakati anamuuliza.... Baba yangu yuko wapi?... Yule mwanamke anamjibu... Usinisumbue baba yako tokea asafiri hatuna mawasiliano na ni miaka mingi.
Baada ya kuona kero inazidi... Yule mwanamke akaamua kwenda kwa mganga ili amtie kichaa yule kijana... Na akafanikiwa... Kijana akawa kichaa cha kufungwa kamba.
Familia yake walipoona mtoto wao amekuwa kichaa wakaazimia wamrudishe uarabuni... Alipopelekwa huko ndipo siri ilipovuja huko... Alitibiwa akapona... Akaelezwa unajua sababu ya kichaa chako.... Akajibu sijui... Akaambiwa mdomo wako umekuponza kumuulizia baba yako kila wakati.
Yule mtabibu akamwambia baba yako ameuliwa miaka mingi imepita... Yupo uwani mwa nyumba anayoishi... Na amefukiwa chini ya kisima.
Yule mtoto baada ya kuipata hiyo habari akasema sikubali... Narudi tena Tanzania nikahakikishe aliyehusika na kifo cha baba yangu anapata haki yake.
Ndipo aliporudi tena Tanzania... Mama yake wa kufikia hakuyaamini macho yake alipomuona tena... Ikawa ugomvi patashika... Mama unahusika na kifo cha baba yangu... Mama akawa mkali kama mbogo.... Mtoto akaenda kutoa taarifa polisi... Polisi wakaja na wafungwa na kuanza kazi ya kukifumua kisima.
Kwa kuwa zege lililowekwa lilikuwa ni kubwa... Haikuwa kazi rahisi... Iliwachukua takribani siku tatu... Huku yule mama akisema mnajisumbua bure kafa mbwa ndio aliyefukiwa humo hamtopata kitu.
Askari wakiwa naye yule mama chini ya kizuizi... Siku ya tatu jioni wanamalizia kutoa zege... Inaanza kutolewa mifupa ya miguu na mikono na fuvu la kichwa.... Lilipoonekana fuvu la kichwa cha binadamu... Hapo ndipo taharuki ilipoanza... Wakazi wa Bagamoyo walikuwa wengi kuangalia huo mkasa.... Askari haraka wakaamua kuondoka naye yule mama ili kulinda usalama wake.
Pamoja na mifupa na skeleton ya kichwa... Ilitolewa saa ya SEIKO 5 akakabidhiwa yule kijana... Na yule kijana alipoitikisa tu saa ilikuwa inatembea kama kawaida... Akaichukua na kuivaa.... Baadhi ya vitu vingi vya baba yake alivitoa sadaka.... Lakini saa ya baba yake aliivaa.
Yule mwanamke alifungwa kifungo cha maisha.
Hapo ndipo nilipoitambua saa ya SEIKO 5... Na pia nikaja kukutana nayo kwenye kitabu cha mtunzi mahiri.... Kitabu cha NJAMA... Willy Gamba... Akiwa amevaa saa yake matata aina ya SEIKO 5... Ukitaka kujua kakisome kitabu cha WILLY GAMBA... NJAMA.
Msifananishe saa nyengine na SEIKO 5.
Sent using
Jamii Forums mobile app