S2kizzy sio producer bora bali ni producer maarufu

S2kizzy sio producer bora bali ni producer maarufu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Dunia ya muziki wa Tanzania imekuwa ikipitia mageuzi makubwa kwa miongo kadhaa. Kila zama imezaa nyota zake – kuanzia wasanii, watunzi, waimbaji, hadi watayarishaji muziki (producers). Katika zama hizi za mitandao ya kijamii, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kujianika hadharani na kujinadi kuwa wao ndio number one kwenye sekta fulani.
images (65).jpeg

Hivi karibuni, jina la Salmin Kasimu Maengo maarufu kama S2KIZZY limekuwa gumzo baada ya kujinasibu hadharani kuwa ndiye producer namba moja wa muda wote ndani ya muziki wa Tanzania, akifanya hivyo kwenye vituo kadhaa vya habari.
TTouch1.jpg

Kauli hii imeibua mjadala mzito, ikizingatiwa kuwa Tanzania imewahi na bado ina watayarishaji waliopiga hatua kubwa, wakatengeneza alama zisizofutika kwenye historia ya muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava).
PF.jpg

Kabla S2kizzy hujazaliwa, Paul Matthysse maarufu kama P Funk Majani alikuwa akitikisa anga ya muziki. Huyu ndiye aliyebatizwa jina Mkono wa Mungu, kutokana na uwezo wake wa kutoa kazi bora ambazo hadi leo zinasalia kuwa alama za muziki.
images (70).jpeg

Majani ndiye aliyekuwa nyuma ya nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family, Juma Nature, Gangwe Mobb, na Dogo Janja wa miaka ile. Fikiria wimbo "Mzee wa Busara" wa Juma Nature au "Msela" – nyimbo zilizoweka msingi wa Bongo Flava na kubaki kwenye kumbukumbu za kila mpenzi wa muziki.
mika.JPG

Kwa upande mwingine, Miika Mwamba lilikuwa jina linalotikisa sana katika miaka ya 2000. Alisifika kwa ubunifu na ubora wa utayarishaji uliosababisha nyimbo kadhaa kukua kimataifa. Wimbo kama "Darubini Kali" wa Afande Sele si tu ulikuwa wa kijamii, bali pia ulikuwa na ubora wa kipekee wa production.
images (69).jpeg

Hii ilikuwa kazi ya producer mwenye upeo mkubwa, aliyeweka uzito kwenye sound na ujumbe wa nyimbo. Mzungu ambaye hakutaka umaarufu kabsa ndio maana kuna picha zake chache sana mitandaoni, kazi zake zinaishi mpaka kesho.
Tudd.jpg

Producer bora huwa hafanyi kazi kwa kutafuta sifa, bali kazi zake hujieleza zenyewe. Fikiria nyimbo hizi:

  • "Barua" – Daz Nundaz, production ya Miika Mwamba, nyimbo ambayo ilimwinua kundi la Daz Nundaz kuwa kundi lililopendwa sana ndani ya Tanzania.
  • "Nikusaidiaje" – TID, production ya P Funk, nyimbo ambayo ilimwinua TID kuwa superstar.
  • "Eno Maiki" – Ziggy Dee, production ya Miika Mwamba, nyimbo ambayo ilimwinua na kumfanya Ziggy kuwa superstar ndani ya Tanzania.
  • "Ndio Mzee" – Professor Jay ft. Juma Nature, production bora sana ambayo ilitengeneza anthem ya vijana wa Tanzania miaka ya 2000.
  • "Kamanda" – Daz Nundaz, kazi nyingine ya Miika Mwmba.
  • "Chuki" – Gangwe Mobb, mojawapo ya nyimbo za kwanza kupeleka street rap mainstream.
  • "Tamala" – Hardmad, mojawapo ya nyimbo bora sana ya mapenzi, wimbo ambao mdundo wake tu ni unique.
facts-pc.jpg

Nyimbo hizi ni mifano hai kuwa Tanzania imebarikiwa na producers wenye vipaji vikubwa ambao walitengeneza miziki ya thamani isiyopimika.
s2kizzy-828x628.jpg

Bwana mkubwa S2kizzy pasipo shaka ana mchango mkubwa sana, kwani amekuwa nyuma ya hits kama "Tetema" na "Amaboko" za wasanii Rayvanny na Diamond Platnumz, nyimbo zilizoitikisa Afrika na dunia.
images (67).jpeg

Lakini je, kufanikisha nyimbo mbili tatu kubwa kunatosha kumfanya awe producer bora wa muda wote? Historia ya muziki wa Tanzania ni ndefu, na majina kama P Funk Majani, Mesen Selekta, Lamar, Maroza, Tudd Thomas na wengineo yameshafanya kazi ambazo zinaishi vizazi baada ya vizazi.
images (66).jpeg

Producer bora hahitaji kujisifu. Ni jamii na historia ndizo zinazomvika taji. Sauti za muziki zinazodumu vizazi ndivyo ushahidi wa ubora wa kweli. Ubora wa kazi husika na heshima ya kazi yake vitaongea.
images (68).jpeg

Kwa hiyo, badala ya kuanzisha majigambo na mabishano yasiyokuwa na faida, S2kizzy anapaswa kuacha kazi zake ziongee. Historia ya muziki wa Tanzania imeshaandikwa kwa wino usiofutika – na huenda siku moja, kama ataendelea kwa ubunifu na nidhamu, jina lake litaunganishwa rasmi na orodha ya vigogo.
PF.jpg

Lakini kwa sasa, kofia ya dhahabu ya producer namba moja wa muda wote bado inabaki mikononi mwa wale waliopanda mlima huu mapema na kusimamisha bendera ya muziki wa Tanzania. Kama haujasikia majigambo kutoka kwa watu kama Tudd Thomas na wahenga wengine, kaa kwa kutulia brother.
 
Darubini kali hivi katengeneza Mika??? Sio Soggy?

Mzungu ni producer bora ila hajawapa wenzake credits nyingi saana.....mmoja akiwa Soggy.

Hongera kwa S2kizzy anamchango mkubwa saana wa kuupeleka Muziki wa wasanii wa Tanzania nje.

Laiti kama Singeli ingepewa nguvu....
 
Ni kweli mkuu, Darubini walikuwa pamoja na Soggy
 
Vita ambayo ipo ni Zest kumchana S2kizzy kuwa hana chochote!
Kwangu S2kizzy ni wa kawaida ila anafanya kazi na wasanii wakubwa. Kabla yake pia alikuwepo Lizer classic nae hivyohovyo kufanya kazi na wakubwa kukampa airtime.

Ila tu yeye kaona fursa ya kuongelewa karuka nayo chap, hajataka kuremba.
 
Zombie apewe heshima yake katengeneza midundo ya Ngoma nyingi zilizoenda masafa marefu kutoka bongo

Mpaka sasa rayvanny anatambia tetema ambayo idea na beat vyote vimetoka kwa s2kizzy
 
Zombie apewe heshima yake katengeneza midundo ya Ngoma nyingi zilizoenda masafa marefu kutoka bongo

Mpaka sasa rayvanny anatambia tetema ambayo idea na beat vyote vimetoka kwa s2kizzy
Ila sio namba moja mkuu!
 
Mziki huu ambao kila kitu unaweza piga hapo kwenye keyboard yako sio ule wa Kaka zetu.

Kujivika taji au kujipigia makofi ni dalili ya kuona watu hawakupi unachodhani unastahili.

"Hakuna Mungu Kama wewe naskia ilipigwa na Master fulani ?"

Bila misingi ya wakubwa sidhani Leo hii mziki ungekuwa hapa ulipo.
Iheshimiwe Mipaka na Zama zake.
 
Nice Mkuu! Na kwa sasa kuna programu za Kompyuta pia zamani walikuwa tofauti
 
Wakongwe wa muziki wakubali kuwa rekodi za mambo mbalimbali zinavunjwa na vijana. Leo hii Filbert Bayi akikimbia kwa mwendo aliokimbia wakati anavunja rekodi ya dunia miaka ya 70 ataonekana kama anatambaa kwa sababu vijana washaivunja rekodi yake kwa mbali. Dunia inaenda mbele hairudi nyuma.
 
Singeli ni mziki wa kihuni, taifa haliwezi kusifika kwa miziki ya kihuni huni.
Darubini kali hivi katengeneza Mika??? Sio Soggy?

Mzungu ni producer bora ila hajawapa wenzake credits nyingi saana.....mmoja akiwa Soggy.

Hongera kwa S2kizzy anamchango mkubwa saana wa kuupeleka Muziki wa wasanii wa Tanzania nje.

Laiti kama Singeli ingepewa nguvu....
Iki
 
Wakongwe wa muziki wakubali kuwa rekodi za mambo mbalimbali zinavunjwa na vijana. Leo hii Filbert Bayi akikimbia kwa mwendo aliokimbia wakati anavunja rekodi ya dunia miaka ya 70 ataonekana kama anatambaa kwa sababu vijana washaivunja rekodi yake kwa mbali. Dunia inaenda mbele hairudi nyuma.
Muziki wa Miika Mwamba umetambuliwa na kupigwa mpaka kwenye movies za Marekani.

Ukiangalia movie ya "Peeples" utaona wamepiga "Maria Salome (Wenye Wivu Wajinyonge)".

Huu wimbo kina Diamond wame u sample pia.

Sasa unamlinganisha vipi Kanye West au DJ Premier on one hand na Isaac Hayes na James Brown on the other?

Alichofanya Miika Mwamba bado hakijarudiwa mpaka leo Tanzania.
 
Miika Mwamba was one special producer mkuu! Asante kwa analysis nzuri
 
Back
Top Bottom