RwandAir Bankrupting Rwanda

Kuna mengi kuhusu Rwanda yamekuwa yakifichwa fichwa kwa muda mrefu sasa yanafumuka moja baada ya jingine!
Madini ya DR Congo hayo!
Uvamizi wa Rwanda nchini DRC = Uhai wa uchumi wa Rwanda
Kama gdp ya rwanda ni $8 wapi wanapata hundred of $ ku rescue airline wanapata wapi reserve yote hiyo kwa biashara ipi wakati haina natural resource
 
Tatizo siasa imefanya hata uwezo wetu wa kufikiri umekuwa mdogo sana na kibaya ziadi hatujui tunachotaka ndio maana wanasiasa wanatuchezea wanavyotaka.

Tatizo sio ku-invest hizo hela kwenye ndege sababu hata tungeivest huko kwenye madawa ndio matatizo ya afya yangeisha ?

Tanzania ni maskini lazima tuinvest kwenye project zitakasaidia kukuza sekta mbalimbali za uchumi ili kuongeza pato la nchi ili tuweze kuhudumia hizo sekta za afya na maji

Tatizo kubwa la Tanzania ni usimamizi wa project zetu hata hizo hela zikipelekwa kwenye maji zinaweza zikatumika ovyo usione kabisa impact ya hizo fedha

Pamoja na mashirika mengi kuingiza hasara lakini serikali zao bado wanaendelea kuya-support kwa sababu wanafahamu impact yao,aviation industry inachangia karibia 35% ya GDP ya Dubai
 
hii habari hii yaan inawafanya watu wasilale usingizi
 
na ukubali tuu kua hatuwezi kushindana nao
 
Pia mkumbuke Kagame aliyefeli kwenye hili ndiyo mentor wa Jiwe kwenye maswala ya ununuzi wa ndege.
 
Oh Lord! I like this observation:
Tatizo siasa imefanya hata uwezo wetu wa kufikiri umekuwa mdogo sana na kibaya ziadi hatujui tunachotaka ndio maana wanasiasa wanatuchezea wanavyotaka.
Ukweli ni kwamba, hata wewe ni muathirika wa hilo tatizo... I MEAN IT!

How come unatoa mfano wa Dubai ambayo mazingira yetu kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni hayafanani hata kidogo?!

FYI, post ambayo niliandika awali niliweka mambo mengi sana including suala la Emirates na mashirika mengine ya Dubai! Hata hivyo, yote ambayo niliandika nili-erase na kuacha ulichokuta kwa sababu nafahamu, watu aina yako mnasukumwa na siasa na kwahiyo kuwaambia uhalisia ni kupoteza muda! Mmeathiriwa na siasa na kuacha kuchezewa na wanasiasa! Wao wanachosema ni RIGHT, you don't argue!

Tena basi umesema:
Tanzania ni maskini lazima tuinvest kwenye project zitakasaidia kukuza sekta mbalimbali za uchumi ili kuongeza pato la nchi ili tuweze kuhudumia hizo sekta za afya na maji
Hiyo ni kweli kabisa lakini inawezekana pale yasipofanyika maamuzi ya kisiasa! Rational Decision Makers hawasukumwi na maamuzi ya kisiasa ambayo hayajali vipaumbele!

Huwezi kufikia hayo uliyosema endapo hufahamu au hutaki kufahamu uanze na kipi na umalizie na kipi!

Tanzania kuna sekta kibao za kiuchumi ambazo hazijawa exploited! Leo hii kama serikali inaandaa future investment portfolio, zenye impact kubwa kiuchumi na hata zenye socio-economic impacts, uwekezaji kwenye ndege KATU hauwezi kuwa hata miongoni mwa Top 5 Best Possible Investments in Tanzania!

Hayo unayosema wewe yangewezekana endapo tu serikali ingewekeza kwenye best investment alternatives ambazo probability ya return ni kubwa! Na hata kama return yake inachukua muda mrefu lakini socio-economic impact yake ingekuwa kubwa!

Ni hizo best investment ndizo zingenunua ndege kutokana na re-investments!
 
Isiwe mbinu ya kutufanya tusiingie huko ili wao ndio watawale soko la anga.
 
Sijausoma uzi wote but nilivyo kua naendelea kuusoama UZI hu mtazamo wangu ulikua kama hu wako, kwa ufupi siamini ushauri wa aina yoyote from PK; jamaa labda kaanza kuona ushindani mkali from Bongo air na kufuatia udogo wa nchi yake, hope wateja wake wengi within this region (I mean the EAC) lazima alilenga Tanzania na Uganda hope na Congo, sasa kama Bongo ndio hivyo Magu kadhamilia is to say, he will lose all customers from Tanzania and hence wil start scrambling with Congolese, Ugandans and of course even Rwandese; hapa imekula kwake, twendage hivyo hivyo tu
 
Fitna za Kenya Airways ili waendelee ku-dominate airspace ya East Africa. Hatutakubali kuendelea kuwa wateja wa kudumu wa KQ. Tumeanza local routes na tutapenya mpaka Sydney mpka Pariii
 
Miaka 20 iliyopita Dubai haikuwa ilivyosasa na nimetoa mfano kukuonyesha economic impact ya aviation business kama itasimamiwa vizuri na Tanzania tuna advantage kubwa sana(bahari,maziwa,madini,mbuga,population) ukilinganisha na competitors wetu

Kufa kwa ATCL nchi jirani walikuwa wanapata faida kubwa sana kutoka kwetu

KQ ana hisa nyingi Precision na ndio walikuwa wame-dominate domestic route zote hapa TZ ,Fastjet walivyoanza kuoperate bongo ikawa threat kwa PW walivyoomba vibali kwenye Kenya Uhuru akawagomea kuwapa leseni
 
Pia mkumbuke Kagame aliyefeli kwenye hili ndiyo mentor wa Jiwe kwenye maswala ya ununuzi wa ndege.
Sio ndege tu, inasemekana hata "Concept" ya kuua upinzani (wapinzani) inaonekana imetoka kwake. Ni mtu "Bogus" kabisa huyu.
 
Ili uweze kuona faida ndani shirika la ndenge la taifa ni lazima ujumuishe faida mbali mbali za shirika hilo kwa taifa, mfano kufungua milango ya biashara na nchi ambazo hufikiwa, uwekezaji, utalii nk.
 
Uko sahihi by 100% ila wale "Party fanatics with parochial mind" kamwe hawatakuelewa kwani wao ni kusifia kila kitu.

Hata leo mabwana zao wakiamua kuuza e.g. Mlima Kilimanjaro au Ngorongoro bado watashindana kusifia..
Bila uwekezaji mkubwa ktk kilimo yoote yale yatakayofanywa itakuwa ni kazi bure tu.
 
unasema nchi ya viwanda lkn kwenye kilimo unatenga 1% tu ya bajeti
lk. ndeg unatenga ma billion hivyo viwanda malighafi zitatoka kwenye ndege?
badala ya kuwekeza kwenye sekta inayoajir watu wengi kilim unawekeza ndge ambayo totaly faida yak n ndg mno tena Mara nyingne hakuna
maana kamati ya bunge ilisema atcl imepata hasara miaka 3 mfululizo tangu ndege hizo zije
 
Ili uweze kuona faida ndani shirika la ndenge la taifa ni lazima ujumuishe faida mbali mbali za shirika hilo kwa taifa, mfano kufungua milango ya biashara na nchi ambazo hufikiwa, uwekezaji, utalii nk.
huwez kuacha sekta kilimo inayoajir 75%, uwekeze vi ndege afu utegemee faida,mqzwazwa pekee ndio wataamin kuna faida
 
hapana swala liko hivi, travel destination za in tanzania ziko nyingi ni kwa sababu ya rasilimali tulizo nazo mfano mbuga za wanyama na migodi na biashara, kwa hiyo wageni wa kuingia huenda wanaweza wakaipa nchi kipato kizuri kwenye kuwekeza kwenye ndege ila lazima pasiwepo na vikwazo na usumbufu unao weza kuleta shida mfano ukiukwaji wa haki za watu, haki za watu kujieleza....

nchi kama Rwanda huwezi amini kuwa maswala ya kisiasa bado inafanya Rwanda isiwe na mvuto sana ki vile, ujue watalii na wanao penda kuja Rwanda kwa kupumzika na kufanya biashara na kuwekeza tu ni wengi sana kutokana na haliya hewa na mazingira ila sasa wengi wanaogopa hawana imani kabisa kwa hiyo kuna fact za kila nchi ambazo hata nchi iboreshe vipi kama hakuna democrasia, haki za binadamu haziheshimiki kikamilifu na watu wawe huru kujieleza lazima wanapoteza sana biashara. ebu angalia kenya ilivyo inakuwa vizuri sana maana hamna figisu na chuki za hapa na pale hata siasa zao ni za msimu lazima tujifunze kwanini kenya imefaulu pamoja na wakati flani kupitia misukosuko ila wanakwenda tu
 
Tutembee kifua mbele tuko kwenye right track
 
Na je RwandAir imeleta wageni wangapi kwa maana ya utalii na mikutano
Unadhani wasingeweza kuletwa na mashirika mengine ya ndege bila kutumia raslimali za nchi kwa sifa za kijinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…