Rwanda yaua wakimbizi watano wa DRC

Rwanda yaua wakimbizi watano wa DRC

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
WAKIMBIZI 2.jpg
​

Wakimbizi watano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wameuawa na wengine wengi, wakiwemo afisa wa polisi kujeruhiwa, wakati vikosi vya usalama vilipokuwa vinajaribu kuzima maandamano ya wakimbizi wa kambi ya Kiziba magharibi mwa Rwanda.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR limesema limeshtushwa na taarifa za vifo vya wakimbizi hao nchini Rwanda.

Msemaji wa UNHCR, Cecile Pouilly, amewataka wahusika nchini Rwanda kuhakikisha usalama wa wakimbizi baada ya maandamano yaliyokuwa yakiendelea tangu Febuari 20 kusababisha vifo na majeruhi

Taarifa zinasema kuwa mkasa huo ulitokea baada ya takribani wakimbizi 700 wa DRC kutoka kambi ya Kiziba kuandamana nje ya ofisi ya UNHCR sehemu za Karongi kupinga kupunguzwa kwa mgao wao wa chakula.

Chanzo: EATV
 
Mr Slim alijua akiruhusu hayo maandamano, wanyarwanda wengine wangejiunga na wakimbizi ktk maandamano. Nadhani wajua nini kingetokea ukizingatia wanyarwanda wana hasira inayothibitiwa na dola kwa muda mrefu sasa.
 
Back
Top Bottom