Rwanda: Wakili wa Paul Rusesabagina afukuzwa nchini

Ashukuru Mungu kwa hatua hizo vinginevyo yangekuwa kama yale ya Area D hapo dodoma
Ashukuru wapi? Akifika kwa wazungu akapime afya yake uenda akawa ashawekewa sumu mwilini mwake itakayomuua kidogo tuuu
 
Wakili wa Paul Rusesabagina, anayeelezwa kuwa shujaa katika filamu ya mwaka 2004 ya Hollywood ya Hotel Rwanda kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda" na ambaye anatuhumiwa kwa "ugaidi", amefukuzwa na mamlaka ya Rwanda Jumamosi jioni kwa "kukiuka sheria ya uhamiaji", kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Uhamiaji.


Mamlaka ya Rwanda inamshutumu Vincent Lurquin, raia wa Ubelgiji, ambaye aliwasili nchini Rwanda Jumatatu kwa visa ya kitalii, kwa kuhudhuria kesi katika mahakama ya Kigali Ijumaa akiwa amevaa mavazi yake ya wakili, wakati "visa yake ilimruhusu kutembelea nchi hii (...) lakini sio kufanya kazi, ”Regis Gatarayiha, Mkuu wa idara ya Uhamiaji nchini Rwanda, ameliambia shirika la habari la AFP.
Uamuzi wa kesi ya Paul Rusesabagina utatolewa Septemba 20, kulingana na taarifa kutoka mahakama ya Kigali.

Mwaka mmoja uliopita, alikamatwa, na kutekwa nyara kulingana na familia yake, na kurudishwa Kigali ambako tangu wakati huo anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi. Hukumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ambayo ilipangwa kutolewa Alhamisi, Agosti 19, iliahirishwa hadi Septemba 20.

Hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa kwa mwezi mmoja kwa sababu ya ukubwa wa kesi hiyo, mahakama ya Rwanda ilisema. Uamuzi wa mahakama utacheleweshwa kwa mwezi mmoja kabla ya kujuwa hatima ya Paul Rusesabagina, ambaye anakabiliwa na kifungo cha maisha, na washtakiwa wenzake 20. Wote wanashukiwa kuwa katika kundi la FLN, kundi lenye silaha ambalo lilidai kuhusika katika mashambulio kusini mwa Rwanda mnamo 2018. Kundi hilo linachukuliwa kama tawi la kijeshi la MRCD, vuguvugu la upinzani la Paul Rusesabagina.

Tangu kuanza kwa kesi hii ya muda mrefu, familia ya Paul Rusesabagina inalaani kuingiliwa kwa mahakama na serikali na kutaka aachiliwe. Ubelgiji na Bunge la Ulaya pia wameelezea wasiwasi wao juu ya mazingira ya kukamatwa kwake na jinsi kesi hiyo inavyoshughulikiwa.

RFI
Huko ubelgiji ndiko aliko TUNDU LISSU.......


Naunga mkono KUFUKUZWA KWA HUYO JAMAA......

#SovereigntyOverIdiocy
 
Back
Top Bottom