Rwanda: Nchi ya Asali na Shubiri ya kutosha

Rwanda: Nchi ya Asali na Shubiri ya kutosha

kimpe

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
911
Reaction score
862
Rwanda bado inauguza makovu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyoteketeza maisha ya watu kati ya 800,000 na milioni moja, ikiwa ni asilimia 80 ya idadi ya watu wa kabila la Watutsi ikiwa ni pamoja na Wahutu wengi. Inakadiriwa kuwa sehemu moja ya sita ya idadi ya raia wa nchi hiyo waliuawa ndani ya majuma kadhaa.

Miaka ishirini baadae mchakato wa maridhiano bado una safari ndefu kufikia mafanikio. Rais Paul Kagame anatuhumiwa kuwadhibiti wapinzani wake, moja yapo ya vitendo vingi vya uvunjifu wa haki za binadamu. Lakini jitihada za kujenga upya nchi hiyo zimeanza kuleta matokeo yanayoonekana.


Habari Njema


Moja ya mafanikio makubwa ya nchi ya Rwanda ni kukua kwa usawa wa kijinsia katika maeneo mengi. Idadi ya wanawake kwenye bunge la Rwanda, ni asilimia 64, ambayo ni idadi kubwa kuliko kwenye mabunge mengine duniani, kwa mujibu wa orodha ya 2014 ya Umoja wa Mabunge katika nchi 189.

Mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano kwenye eneo la teknolojia mpya. Ulibuniwa mwaka 2001, umeonyesha mafanikio makubwa.

Wakati wa awamu ya pili ya mpango huo, iliyoishia mwaka 2010, Rwanda ilishuhudia asilimia 8,900 ya ongozeko la watumiaji, ukifananisha na asilimia 2,450 kwenye sehemu nyingine barani Afrika na asilimia 44 duniani. Jarida la African Renewal, linalomilikiwa na Umoja wa Mataifa, liliandika kwamba maeneo manne ya sekta ya umma (mawaziri, mawakala, majimbo na wilaya) na takribani theluthi ya sekta binafsi imeunganishwa na mtandao wa intaneti. Mji mkuu wa Rwanda, Kigali unafanya vyema kwenye maendeleo ya mfumo wa rada na mawasiliano ya anga kwenye eneo lote.


Rais Kagame anashikilia msimamo kwamba "intaneti ni huduma inayohitajika kwa umma kama ilivyo kwenye maji na umeme." Kwa ushirkiano na kampuni ya mawasiliano ya Rwandan Telecentre Network (RTN), serikali imetekeleza mpango wa maendeleo ya upatikanaji wa huduma ya intaneti katika maeneo ya vijijini.


Habari za Matumaini


Baada ya mauaji ya kimbari, nchi hiyo ilichukua hatua za kisheria, kujenga Tume ya Kitaifa ya Umoja na Maridhiano (NURC). Tume hiyo, iliyoanzishwa mwaka 1999, inakusudia kuchangia kwenye hatua za utawala bora; kukuza mshikamano, maridhiano na ushirikiano wa kijamii miongoni mwa Wanyarwanda; na kujenga nchi ambayo kila mmoja ana haki sawa.


Habari Mbaya


Kwa bahati mbaya, kazi hii inayoleta matumaini imefukiwa kwenye kaburi la ukiukwaji wa haki za binadamu unaoripotiwa na makundi ya utetezi. Vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu zimekuwa vikitokea kwa miaka mingi. Mwaka 2012, baada ya kutuma wajumbe kadhaa kwenye nchi hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International liliishutumu nchi hiyo kwa vitendo hivyo:

Kati ya mwezi Machi 2010 na Juni 2012, Amnesty International ilikuwa na matukio 45 ya kukamatwa kwa watu kinyume cha sheria na shutuma 18 ya utesaji au vitendo visivyo vya kiungwana kwenye Camp Kami, kambi ya kijeshi ya Mukamira, na kwenye nyumba salama kwenye jiji la Kigali.

Wanaume walikamatwa na J2 katika kipindi cha kati ya siku 10 na miezi kadhaa bila kuonana na wanasheria, madaktari na wanafamilia.
Matukio ya kuuawa kisiasa kwa wapinzani yamekuwa yakiripotiwa nje ya nchi hiyo. Waandishi wa habari na viongozi wa zamani wa kisiasa walio karibu na rais wa Rwanda wamekuwa wakikamatwa na kuuawa.

Matukio ya ukamataji ya hivi karibuni yalithibitishwa mwanzoni mwa mwezi Aprili 2014. Mwimbaji maarufu Kizito Mihigo, mhangan wa mauaji ya kimbari, na watu wengine watatu, akiwemo mwanandishi wa habari kwa tuhuma za kupanga shambulizi la bomu kwenye jengo moja jijini Kigali. Kizito Mihigo, hata hivyo, anafahamika kwa uanaharakati wake kwa masuala ya amani. Alianzisha Asasi isiyo ya Kiserikali kwa ajili ya kutoa elimu ya amani.

Mwimbaji huyo alipatwa na hatia, lakini mashaka makubwa yanazunguka maeneo mengi ya kesi hiyo.Zaidi, kwa miaka kadhaa iliyopita Kigali imekuwa mahusiano duni ya kidiplomasia na nchi nyingine kadhaa. Nchi ambayo iliwahi kuwa kipenzi cha nchi za Magharibi, Rwanda sasa imeanza kuwa eneo la kukwepwa na inakosa misaada ya kijeshi pamoja na ile ya kimaendeleo. Mahusiano ya kidiplomasia na Afrika Kusini yamekuwa mabaya kufuatia mauaji ya kisiasa ya wapinzani waliokuwa nchini humo. Tayari kumekuwa na matukio ya kuwafukuza wanadiplomasia katika pande hizo mbili.


Source: Global Voice.
 
wabunge wanawake kuwa 64% si usawa wa kijinsia bali ni mbinu nzuri ya kuepuka kupigiwa kelele na kufanya uogopwe.

hapa Tz wabunge wengi wanaume ndio maana wanasumbua bungeni na wako free wanasema vitu bila kuogopa .
 
Back
Top Bottom