Rwanda na hatima ya tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rwanda na hatima ya tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Nov 6, 2009.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hali ya mambo ilivyo hapa Nchini Tanzania haina tofauti sana wakati Wanyarwanda wanaelekea kwenye mauaji ya Kimbari. wakati huo kwa kutumia vyombo vya habari ambavyo vilikuwa havikemewi na wenye mamlaka baadhi ya wahutu wenye misimamo mikali waliwahimiza watusi wenzao kuuu watutsi ambao wao waliwaita "mende" ambao kazi yao kubwa ni kueneza "ugonjwa' wa ubwana mkubwa.

  Hapa Tanzania sasa hivi kuna mambo ya kutisha sana yaandikwa dhidi ya watu wengine kwenye vyombo vya habari ni kama vile kuchochea watu hao kuuawa na jamii. na CCM nayo imeanzisha kabila na dini yake mpya.

  Ukiwa ni mwana-CCM huguswi na Sheria ilmradi unakichangia chama na kupeperusha bendera ya CCM kwenye biashara yako haramu.wana CCM walipiga watu mapanga Tarime, walikamatwa na shahada za kupigia kura zisizo zao huko Busanda na Biaharamulo lakini hakuna kilichowapata!

  Na wimbo wa " wapinzani tuwalete tuwachanechane tuwatupe!!" unaendelea kurindima kwenye kampeni za CCM bila kukemewa na yeyote ndani ya CCM wala vyombo vya dola.

  Itafikia wakati wasiokuwa kwenye dini na kabila la CCM wataletwa na kuchanwachanwa na kutupwa huku wenye CCM yao wakipiga makofi huku wakishangilia!!

  Ni mtazamo TUU!!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bwana Kigarama umelisema neno hili katika wakati sahihi sana!..Big-up kwa ujasiri wakulitamka tu!
  Hapa kwetu jambo lolote utalifanya ili mradi tu uwe mwanasisiemu, na wala hakuna anayestuka!....Hatari uliyoitaja katika bandiko hili iko jirani, just around the corner...God Bless Tanzania!
   
Loading...