Rwanda: Msikiti mmoja na Makanisa 714, yamefungiwa kwa kukiuka sheria ya Usalama

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
paul-kagame_2.jpg

Serikali ya Rwanda imeyafunga makanisa zaidi ya 700 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kigali kwa kukosa kutimiza masharti yaliyowekwa ya usafi na usalama.

Gazeti la kibinafsi la The New Times linasema operesheni hiyo ilianza wiki moja iliyopita.

Kufikia sasa, makanisa 714 yamefungwa, pamoja na msikiti mmoja.

Afisa wa serikali Justus Kangwagye ameambia gazeti hilo la mtandaoni kwamba makanisa hayo yamekiuka sharia za usalama.

"Shughuli ya kuabudu inafaa kufanywa kwa utaratibu na kwa kutimiza masharti ya viwango vya ubora na usalama vilivyowekwa. Kutumia uhuru wako wa kuabudu hakufai kuingilia haki za watu wengine. Wametakiwa kusitisha shughuli zote hadi watimize masharti yaliyowekwa," amesema.

Amesema baadhi ya makanisa haya yalikuwa yakifanya kazi bila kuwasilisha upya maombi ya leseni na kwamba maafisa wa serikali hawataruhusu makanisa hayo yafunguliwe.

Taarifa zinasema baadhi ya makanisa yamekuwa yakifanya kazi kwa kutumia mahema na hayana maeneo ya kutosha ya kuegesha magari ya waumini.

Baadhi ya waumini wamekuwa wakiegesha magari yao pambizoni mwa barabara na kusababisha misongamano ya magari.

Wakazi wa Kigali, kwa mujibu wa gazeti hilo, wana hisia mseto kuhusu hatua hiyo.

Baadhi wanaiunga mkono lakini wengine wangependa wenye makanisa hayo wamepewe muda zaidi wa kutimiza masharti hayo.

Askofu Innocent Nzeyimana, rais wa Baraza la Makanisa katika wilaya ya Nyarugenge ameiomba serikali, kwa niaba ya makanisa, kuyaruhusu makanisa yaliyofungwa yaendelee kuhudumu yanapoendelea kufanya juhudi za kutimiza masharti yaliyowekwa.

Chanzo: BBC
 
Sawa Kabisa Watu Wanajenga Mabanda Tu Ili Mradi Wapate Pa Kupigia Pesa Funga Tu Kagame Hakuna Namna Vijikanisa Kama Mabanda Ya Nguruwe Eti Kanisa BARAKA ZA MUNGU NA ZIWE NASI KWA SABABU TUNAIJENGA NYUMBA YA BWANA
 
Hapa Bongo watu wanafunga mtaa kwa ajili ya ibada, nenda kariakoo ijumaa, mitaa inafungwa kwa ajili ya watu kuswali, yani swala zao zinaingilia uhuru wa watu wengine kutumia barabara.

Njoo mitaani, makanisa hayana sound proof, misikiti bila vipaza sauti wanaona kama hawajaswali, kupigia watu kelele, uchafuzi wa hali ya hewa(noise pollution).

Nawapongeza sana Rwanda, uhuru wa kuabudu wa mtu usiingilia uhuru wa mtu mwingine.

Hii ihamia Tanzania pia.
 
zumbukuku wee
 
Ukiona kiongozi anakua na matatizo na makanisa na misikiti jua huyo ana matatizo...watu wanaabudu unawafungia wafanye nini hapo kafungia maeneo wanayompinga akidhani uwepo wa hayo makanisa ni sehemu ya kuendelea kumjadili hajapenda yanayotokea kwa Kabila kanisa linaongoza maandamano...
 
Bure kabisa....watakua wameona kinachotokea Congo ...RC imemkalia kooni Kabila..sababu na wao hawajiamini wanaanza kujihami mapema..poor Rwandese
 
Hapa Bongo watu wanafunga mtaa kwa ajili ya ibada, nenda kariakoo ijumaa, mitaa inafungwa kwa ajili ya watu kuswali, yani swala zao zinaingilia uhuru wa watu wengine kutumia barabara.

Njoo mitaani, makanisa hayana sound proof, misikiti bila vipaza sauti wanaona kama hawajaswali, kupigia watu kelele, uchafuzi wa hali ya hewa(noise pollution).

Nawapongeza sana Rwanda, uhuru wa kuabudu wa mtu usiingilia uhuru wa mtu mwingine.

Hii ihamia Tanzania pia.
HUYU NI MTOTO WA DAWA HAHAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom