Rwanda imeweza kutangaza Utalii kupitia klabu ya Arsenal, Tanzania ilijaribu lakini fedha zikapigwa huko London

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
sei_13862042.jpg

Jezi ya timu ya Arsenal ya msimu wa ligi wa 2018/19 ikionyesha neno la "Visit Rwanda" zikiwa zimevaliwa na kiungo Mesut Ozil na washambuliaji Alexandre Lacazette na Pierre Emerick Aubameyang.

Hivi majuzi katika vyombo vya habari vya nchi za magharibi na Marekani kulitokea kelele nyingi kuhusu namna jinsi Serikali ya Rwanda ilivyoamua kutumia fedha zake kujitangaza kwenye klabu ya Arsenal ya Uingereza.

Vyombo hivyo vya habari vikaendelea kusema bila kuwa na ushahidi kwamba fedha zilizotumika karibu pauni milioni 30 zingefaa kuelekezwa kwenye miradi ya maendelo kwani ni sehemu ya fedha za misaada ambazo nchi hiyo inapokea kutoka Uingereza.

Kulingana na mkataba wa miaka mitatu kati ya Rwanda na timu hiyo ya Arsenal, kila mwaka Rwanda itakuwa ikilipa pauni milioni 10 na neno la "Visit Rwanda" au tembelea Rwanda litakuwa likionekana kwenye sehemu ya bega kwenye jezi wanazovaa wachzaji wa Arsenal.

Pia neno la "Visit Rwanda" litakuwa pia likionekana kwenye soksi za wachezaji na pia kwenye vioo vya kuonyeshea matangazo uwanjani humo yaani uwanja wa Emirates uliopo sehemu iitwayo Ashburton Grove..

Kwahiyo baada ya miaka mitatu kama mkataba utahitajika kurudiwa basi itafanywa hivyo au vinginevyo.

Nikiwa ni mmoja wa wafuatiliaji wa masuala ya kimataifa na nyuma ya mapazia yake na huku pia nikiwa ni mpenzi wa klabu yangu maarufu ya Arsenal na pia kwa kuzungatia kuwa niikuwepo kwenye sherehe za uzinduzi wa kampeni hiyo, nikaona na mimi nitoe maoni yangu machache kuhusiana na jambo hili.

Kwanza nikamsikiiza dada Clare Nkamanzi ambae ni afisa mtendaji mkuu wa bodi ya maendeleo ya Rwanda au "Rwanda Development Board", ambae alisema wazi kuwa fedha zinazosemwa ni kidogo cha fedha halisi zilizotumika na kwamba fedha hizo ni za kutoka kwenye mapato ya utalii.

Pia bibie Akamanzi akaendelea kufafanua kitaalam kwamba matangazo hayo yamesimamiwa vema nai yataitangaza Rwanda nchini Uingereza na pia yataongeza idadi ya watalii kutembelea Rwanda jambo litakalopelekea kuongeza mapato zaidi ya Utalii.

Lakini cha msingi zaidi bibie Akamanzi akasema kwamba hiyo ni moja za hatua za kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje.

UK aid mfuko unaotoa fedha za miradi ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Rwanda mwaka 2017/18 ilitoa kiasi cha pauni milioni 64 na zingine pauniu milioni 62 zikija kwa mwaka 2018/19, hiyi ni kwa mujibu wa taarifa za idara ya maendeleo ya kimataifa au DfID ya Uingereza.

Bibie Clare Akamanzi aliendelea kutoa ufafanuzi kwamba Serikali ya Rwanda imejaribu katika kipindi cha miaka 20 ilopita kupunguza utagemezi wa fedha za misaada kutoka asilimia 80 hadi asilimia 17 leo hii.

Alisema Rwanda inapata mapato ya utalii yanayotokana na kutoa vibali na viza zaidi ya pauni za Uingereza milioni 50 kwa mwaka.

Kufuatia kitendo hicho kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwenye vyombi vya habari vya nchi za magharibi na wale wanaojiita watetezi wa haki za binadamu kama bibie Rene Mugenzi ambae amedai mpango huo ungefutwa kabisa.

Walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo idara ya DfID wamesema kwamba wao hawajatoa fedha kwenda kwenye mpango wa Visit Rwanda au kwenda Rwanda Development Board bai fedha wanazotoa zinaenda kwa miradi inayotambulika rasmi kwenye maeneo ya Kilimo na Elimu.

Mapema tarehe 23 mwezi huu wa Mei akitangaza mpango huo wa Visit Rwanda afisa masoko mkuu wa Arsenal bwana Vinai Venkatesham aliielezea Rwanda kwamba ni moja ya nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi barani Afrika na huku utalii ukizidi kupanuka basi tutashuhudia idadi ya watalii wakitembelea Rwanda na Afrika kwa ujumla.

Bwana Vinai Venkatesham alisema Rwanda imebadilika na klabu ya Arsenal na wapenzi wake watapata nafasi ya kuifahamu zaidi nchi hiyo.

Rwanda inakuwa nchi ya kwanza kutoka Afrika kuwekeza kwenye utalii kupitia matangazo kwenye uwanja wa mpira barani Ulaya pamoja na jezi ya klabu husika kitendo ambacho hakijawahi kufanywa miaka ya nyuma.

Hata serikali ya awamu ya nne iloongozwa na Jakaya Kikwete ilijaribu kufanya matangazo kupitia kwenye mabasi ya jiji la London lakini hukukuwa na matokeo yoyote chanya kimapato au "Money for value" na fedha zinapigwa na kupigika.

Hivyo basi kitendo hiki kinapaswa kupongezwa kwa moyo wote na imani kwamba serikali zingine za kiafrika zenye vivutio mbalimbali vya Utalii na viunga vyake zinafuata mkondo.

======
 
tatizo la tanzania kila mtu mwizi mpaka baba yako aliye kuzaa(samahani maana naye ni mtanzania mmoja wapo) pili kila mmoja ni mchumia tumboni(mpaka wewe tukikupa nafasi uzarendo utakuwa tumboni mwako)
 
Wazungu bado wanaendelea kuzinyonya nchi za afrika kwa ujinga wetu. Suala la kujitangaza nchi haikuwa lazima kufanya hayo inatakiwa itengeneze mazingira ya nchi na kuweka demokrasia, pamoja na sera nzuri za utalii ikiwemo nafuu ya kodi. Mambo yote yako kwenye utandawazi kama nchi umeitengenezea vivutio na ukaweka kwenye website. Hata ukitangaza kama miundo mbinu mibovu sera mbovu hakuna demokrasia ni kupoteza kodi.
 
Binafsi naona ni waste of money. ..... ngoja watupe marejesho baada ya miaka hiyo mitatu!!

Africa kwa sasa waangalie namna ya kuweka 0 % kodi on foreign investment na kuangalia namna ya kumanage..!!
 
Binafsi naona ni waste of money. ..... ngoja watupe marejesho baada ya miaka hiyo mitatu!!

Africa kwa sasa waangalie namna ya kuweka 0 % kodi on foreign investment na kuangalia namna ya kumanage..!!
Well said!
 
Binafsi naona ni waste of money. ..... ngoja watupe marejesho baada ya miaka hiyo mitatu!!

Africa kwa sasa waangalie namna ya kuweka 0 % kodi on foreign investment na kuangalia namna ya kumanage..!!

Siyo waste of money kwasababu Rwanda wana ndege yao ambayo sasa inaenda London Gatwick, hivyo pamoja na kampeni hii, pia itawasaidia watalii kukata tiketi za moja kwa moja kwenda Kigali badala ya kuunganisha ama Dar au Nairobi.

Pili, kumbuka wamesema fedha zinazotumika ni sehemu ya fedha ya mapato yatokanayo na utalii huohuo, hivyo kuonyesha kwa kiasi kikubwa kwamba wanaweza kutumia fedha za aina hii kwa nidhamu badala ya kuzitapanya huku na kule.
 
Wazungu bado wanaendelea kuzinyonya nchi za afrika kwa ujinga wetu. Suala la kujitangaza nchi haikuwa lazima kufanya hayo inatakiwa itengeneze mazingira ya nchi na kuweka demokrasia, pamoja na sera nzuri za utalii ikiwemo nafuu ya kodi. Mambo yote yako kwenye utandawazi kama nchi umeitengenezea vivutio na ukaweka kwenye website. Hata ukitangaza kama miundo mbinu mibovu sera mbovu hakuna demokrasia ni kupoteza kodi.

Dah! haya mkuu, unazungumzia demokrasia.

Lakini Rwanda inapiga hatua mbele, Tanzania je tuliweza kuweka mabango huko London kutangaza vivutio vyetu vya utalii kwa angalau miezi sita?
 
tatizo la tanzania kila mtu mwizi mpaka baba yako aliye kuzaa(samahani maana naye ni mtanzania mmoja wapo) pili kila mmoja ni mchumia tumboni(mpaka wewe tukikupa nafasi uzarendo utakuwa tumboni mwako)

Hiyo sio kweli, wapo watanzania ambao wamekuwa ni waadilifu na wenye kutimilika.
 
Wazungu bado wanaendelea kuzinyonya nchi za afrika kwa ujinga wetu. Suala la kujitangaza nchi haikuwa lazima kufanya hayo inatakiwa itengeneze mazingira ya nchi na kuweka demokrasia, pamoja na sera nzuri za utalii ikiwemo nafuu ya kodi. Mambo yote yako kwenye utandawazi kama nchi umeitengenezea vivutio na ukaweka kwenye website. Hata ukitangaza kama miundo mbinu mibovu sera mbovu hakuna demokrasia ni kupoteza kodi.
Twambie ni lini Demokrasia ilikulipia bill ya umeme nyumbani kwako. Unaleta upuuzi in serious smart economic moves.
 
Huyo nkamanzi anaongea kiswahili bibi Hindu au haji manara atasubiri..

Amekulia Uganda lakini Kiswahili hazungumzi "fluent" ila anasikia maneno machache.

Ni binti "smart" sana na ni mmoja wa wanadiplomasia wadogo walio na vyadhifa za juu kwenye serikali ya raisi Paul Kagame.
 
Tukubali tukatae Rwanda wametupiga bao kwenye upande wa kuingia mkataba na Arsenal ila si kwa mengine...ile project ya Kina Pinto na Bodi ya Utalii enzi za JK waliyoingia mkataba na Sunderland ambayo imeshuka daraja naona kulikua na upigaji mkubwa sana hakuna value for money Sunderland ni katimu kadogo sana.. nashauri Tanzania Tuingie mkataba na Manchester United au Liverpool ndio team zilizokaa vzuri kwenye soko...ukianzia mashabiki wao walivyo na hamasa..naona kama Chelsea na Manchester City zimepoa kibiashara... (nadeclare interest mimi ni Mshabiki wa Arsenal wa ukweli na roho inaniuma Kagame kutuwahi)..Mheshimiwa Rais JPM Hawez kukosa bilioni 80 za kututangaza Premier league kwani ndiyo league inayoongoza kuangaliwa dunian ata na wamarekani ..Wachina...Waarabu etc so watalii Tanzania itakayopata si Waingereza tu ni dunia nzima hivyo (NCHI YETU YA TANZANIA ITAONGEZA WATALII WENGI NA FEDHA NYINGI ZA KIGENI PIA TUTAPATA PRESTAGE YA KUFAHAMIKA DUNIANI KOTE KWANI KUFAHAMIKA/WORLD PRESTAGE NI MOJA YA CURRENT MARKERTING STRATEGIC AMBAYO INATUMIKA KATIKA MASHIRIKA YA NDEGE NA SOKA BILA KUJALI FAIDA UNAYOPATA AMBAYO NAAMINI KUFAHAMIKA/PRESTAGE NDIYO SABABU KUU YA KAGAME KUSPONSOR ARSENAL KWANI ATA SHIRIKA LA NCHI YAKE LA RWANDA AIR LIMETANGAZA KUPATA HASARA KUBWA KATIKA MWAKA HUU WA FEDHA ILA RWANDA NA KENYA WAMEWEKEZA KWENYE PRESTAGE ZAIDI AMBAYO BAADA YA MUDA HUA INALIPA)..na Watanzania tutatembea kifua mbele kwa majirani zetu, Wizara ya MaliAsili Na Utalii wapeleke proposal nzuri au waombe kibali tu kwa Mheshimiwa Rais( TANAPA NA NGORONGORO WATOE HIYO ELA WANA UWEZO HUO UZURI HAITOLEWI KWA MKUPUO NI KILA MWAKA FOR 3YEARS) (NOTE: Nina wasiwasi Wakenya watafanya bonge la suprise wanaweza kuiwah Man UTD au liverpool/Man City)Tuwahi hii fursa...NAIPENDA TANZANIA....(NB..Nisamehen kwa kuchanganya herufi kubwa na ndog lengo kubwa ni msisitizo)..NAIPENDA TANZANIA
 
Twambie ni lini Demokrasia ilikulipia bill ya umeme nyumbani kwako. Unaleta upuuzi in serious smart economic moves.

Hayo matangazo hawakutangaziwa kwa wapiga debe walokua hawajui maana ya demokrasia, ndio mana hayakuletwa manzese.
 
Back
Top Bottom