Mkuu
MUKAMASIMBA yapo mambo mengi yanayochangia PK kuhangaika sana la kwanza ni uhusiano wake na Tanzania uko katika hali tete anajua position ya Tanzania inaweza kuamua hatima yake.
Pili ukiangalia Generals wote aliogombana nao wememzidi shule sana hawataki kuburuzwa kama watoto wadogo wanapenda Rwanda huru yenye uhakika wa upatikanaji wa haki (mahakama huru)wanapenda kuona Rwanda ikongozwa kwa kuheshimu misingi ya katiba tofauti na kinachoendelea Rwanda sasa kila kitu ni Kagame ukikwaruzana naye utapachikiwa kesi ya kuhatarisha amani ya Rwanda na kwa hakika lazima utafungwa kwasababu mahakama si huru.
Tatu tumeona nchi zote za EA wakuu wa nchi wakitofautiana na wakuu wa upinzani na wakabaki salama hali ni tofauti huko Rwanda.Ukiangalia Uganda yupo Col Kiza Bisegye wamesuguana sana na Gen Museveni hadi akakimbia nchi lakini leo yupo Uganda salama.Ukienda Kenya Raila anaipeleka puta serekali ya Uhuru Kenyatta sijasikia kawekwa ndani au kuzuiliwa nyumbani kwake au kanyimwa kuongea na wanahabari.Ukija hapa Tanzania ndio usiseme kabisa Mtikila aliwahi kumtyukana Rais Kikwete ni gaidi kesi imekwenda mahakamani Mtikila kashinda na hii si mara ya kwanza au pili hii inatokea kila mara.Wapo wapinzani wengi sana wanaisumbua serekali ya CCM wapo salama.