Ruvuma: Wazazi 763 wakamatwa kwa kutopeleka Wanafunzi waliofaulu Shuleni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Idadi hiyo imefikiwa baada ya msako wa nyumba kwa nyumba uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro, kutokana Wanafunzi wengi wa Darasa la Kwanza na Kidato cha Kwanza kutoripoti Shuleni.

Maeneo mengi Nchini yamekuwa na mwitikio wa kusuasua kwa Wanafunzi waliofaulu kuripoti Shuleni ambapo hadi kufikia Januari 15, 2023 zaidi ya Wanafunzi 700,000 wa Kidato cha Kwanza, hawakuwa wamefika kwenye Shule walizochaguliwa.

Licha ya baadhi ya Wanafunzi kudaiwa kujiunga na Shule za Binafsi imeleezwa kuwa bado kuna idadi kubwa ya Wanafunzi waliofaulu wamebaki majumbani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Wazazi kutotaka Watoto waende Shule.

RADIO ONE
 
🤣 Dah! Naanza kuelewa kwanini watu wengine hukataa mimba! Kumbe ukizaa ndo yanakukuta mambo kama haya! Unyama sana.
 
Kwa ile mijeledi tuliyoona katika TV ya kucharazwa ktk ugoko na kukanyagwa magoti kama kuku anayechinjwa for 7 years plus next fours lazma vijana wakimbie shule ukizingatia sasa hivi wasomi wana degree hadi masters na hawana ajira.
 
Back
Top Bottom