beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Sakata la mishahara hewa katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limefikia hatua mpya baada ya Halmashauri hiyo kuwabana na kuwafikisha Polisi watumishi waliokuwa wakilipwa mishahara wakati walishastaafu na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 31 ambapo watumishi 24 kati ya 45 wamerejesha na wanaendelea kurejesha fedha hizo na bado kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 20 kurejeshwa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Bw. Venance Mwamengo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema katika Halmashauri yake yake jumla ya watumishi hewa 45 wamepatika katika uhakiki wa watumishi hewa na kwamba wengine 15 wanahojiwa polisi kwa makosa ya kupokea pesa wakati wakijua walishastaafu.
Mkurugenzi huyo amesema baada ya kuwabana watumishi waliokuwa wakipokea mishahara ilhali wakijua walistaafu zoezi litahamia ofisini kwake kufuatilia ni kwa nini waliwalipa watu waliokwishastaafu na kuisababishia serikali hasara.
Bw. Mwamengo ametoa wito kwa wote waliokuwa wakilipwa fedha ilihali wakijua walishastaafu kuzirejeshe fedha hizo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.