Ruto: Wakenya hawatapigana tena sababu ya siasa, wajinga hawapo tena

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Naibu rais William Ruto amesema kwamba Kenya haitashuhudia machafuko tena kwa sababu ya siasa kama ilivyokuwa mwaka 2007.

Akihutumbia mkutano wa hadhara mjini Kisii siku ya Alhamisi, Ruto alisema kwamba baadhi ya wanasiasa walikuwa wakitumia vitisho kudai kwamba huenda kukazuka machafuko mwaka 2022.

“Wakenya hawatapigana kwa sababu ya uchaguzi, wajinga hawapo tena…nchi hii itakuwa na amani na mjuwe kwamba hakuna atakayeshurutishwa kufanya jambo kinyume na hiari yake,” alisema.

Aliendelea kusema “Nataka kuwahakikishia wakenya kwamba, kama bado mimi ni naibu rais, hakutakuwa na mapigano nchini Kenya tena kwa sababu ya siasa”.

Ruto kisii


Naibu rais alisema kwamba wakenya wako macho na wanafahamu ya kutosha kujiepusha na siasa za fujo.

Ruto aliyasema haya siku mbili tu baada ya kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwataka wandani wa naibu rais kutolipeleka taifa kwa enzi za ‘giza’ na machafuko.

“Tumeenda kwa vita 1992, 1997 na 2007 na mtu asijaribu kurejesha nchi hii kwa vita tena kwa sababu ya siasa,” Raila alisema katika mkao na wanahabari katika ofisi yake ya Capitol Hill.

Ingawa Raila hakutaja jina la Ruto, mwandani wake aliyezungumza baada ya Raila kuzungumza alimtaja.

“Naibu rais anafaa kuacha kutisha watu na ghasia. Asidhani kwamba ana ukiritimba wa ghasia,” mbunge wa Suna East Junet Mohamed, alisema.

Mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno na mwenzake wa Kapseret Oscar Sudi walikuwa wametowa matamshi ya kumdhalilisha rais Kenyatta na familia yake matamshi ambayo yalizua hisia kali nchini katika ulingo wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom