Ningependa kujuwa anapunguza mishahara na posho kwa watumishi wapi? Wanaopokea shilingi ngapi hadi ngapi? Je ni kwa wafanyakazi wote wa umma na wale wa kisiasa au ni baadhi ya watumishi wa umma wanaopokea mishahara mikubwa na minono? Maana kuna mwingine na wengine wanapokea mishahara mikubwa na ya kufuru ambapo hata ukipunguza inakuwa kama tone tu la mvua.wakati wengine unakuta mishahara yao tu walikuwa wanaona haitishi tangia awali.kwa hiyo ukipunguza maana yake unakuwa unaibua mgogoro mwingine na vurugu nyingine.
Kwa sababu hawa wenye vipato na mishahara ambayo inashindwa kutosheleza mahitaji yao kwa Mwezi ukiwapunguzia kwa asilimia hizo,maana yake unawakatisha tamaa,kuwavunja moyo wa kazi,kuwafanya waanze mgomo wa chinichini,kuzorotesha huduma kwa sababu hawawezi kuwa na nguvu wala morali ya kazi.
Ningemshauri afanye haya. Apunguze mishahara ya wanasiasa hususani wabunge ambao wao inasemekana wana mishahara mikubwa sana kuliko mbunge yeyote yule Barani Afrika. Wenyeviti na viongozi wa taasisi mbalimbali nao wapunguziwe mishahara. Kudhibiti masuala ya semina zisizo na ulazima na ikiwezekana zifanywe kidigitali.kudhibiti rushwa na ufisadi, kuhakikisha kila senti inayokusanywa na mamlaka ya mapato ya kenya inakwenda kwenye kapu kuu la Taifa.
Kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,kuvutia wawekezaji na uwekezaji, utalii ili kuongeza pesa za kigeni na mapato ya ndani.
Nitaendelea baadaye kidogo kufanya uchambuzi.