Ruto Amlipua Mwandishi - "Usiniletee Mambo ya Mtu Mjinga"

Ruto Amlipua Mwandishi - "Usiniletee Mambo ya Mtu Mjinga"

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
82
Reaction score
37

Rais William Ruto alikumbana na swali la Mwanahabari kuhusu madai ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhusu madini ya niobium na rare earth yaliyopo Mrima Hills, huko kaunti ya Kwale. Badala ya kujibu moja kwa moja madai hayo, Ruto alimkatiza mwanahabari huyo na kusema:

“Usiniletee maneno ya mtu mjinga kama huyo tafadhali. Tuongee maneno mengine, yule ni mpuuzi sana yule.”

Lakini swali lenyewe lilikuwa na uzito mkubwa kuliko majibu yake. Gachagua amekuwa akidai kwamba Serikali inapanga kuingia makubaliano na kampuni ya Marekani kuhusu uchimbaji wa niobium ya Mrima Hills. Pia amedai kuwa rasilimali hizo zina thamani ya takriban shilingi trilioni 8.2 na kwamba Wakenya wanapaswa kuhakikisha hazitumiki bila nchi kunufaika. Haya ni madai ya Gachagua na hapa ndipo mambo yanakuwa ya kuvutia zaidi kwa sababu;

Serikali tayari imeanzisha mchakato wa kutafuta wawekezaji wa kuendeleza Mrima Hills kupitia mchakato wa ushindani wa kuomba nia ya kuwekeza (expression of interest).

Hii si sawa na kusema tayari kuna mkataba wa mwisho wa uchimbaji na kampuni fulani. Zaidi ya hapo, nyaraka za mchakato huo zinaonyesha kuwa Serikali bado inahitaji kazi zaidi ya kitaalamu kuhusu uwezekano wa kibiashara wa mradi huo. Ripoti ya tathmini ya kiuchumi au utafiti kamili wa uwezekano wa mradi unaoweza kufadhiliwa (bankable feasibility study) haijaandaliwa, kwa mujibu wa taarifa kuhusu nyaraka hizo za zabuni. Na muhimu zaidi, thamani inayotajwa mara kwa mara ya takriban trilion 8 si kiasi cha pesa ambacho Serikali tayari inatarajiwa kupata bali ni makadirio yanayohusishwa na rasilimali zilizo ardhini na hayamaanishi moja kwa moja faida halisi ya mgodi.

Kwa upande wake, Rais Ruto hakujibu moja kwa moja madai ya Gachagua kuhusu Marekani au mkataba wa Mrima Hills. Badala yake, alizungumzia umuhimu wa kurekebisha sekta ya madini na akatoa mfano wa shughuli za zamani za uchimbaji katika eneo la Mlima Kenya, akisema nchi haikuwa na rekodi nzuri ya kufuatilia madini yaliyotolewa na yaliishia wapi.

Hivyo, kile kilichotokea kwenye hiyo interview ni zaidi ya exchange ya maneno makali. Kuna maswali halali yanayobaki mezani:

Ni kampuni gani itachimba Mrima Hills?

Serikali inatarajia Kenya na wakazi wa Kwale wanufaike kwa kiwango gani? Ni madini kiasi gani yanayoweza kuchimbwa kibiashara, tofauti na kiasi kilichokadiriwa kuwa kiko ardhini? Na Je, mchakato mzima utakuwa wazi kwa umma kwa kiwango gani?

Kwa sababu mwisho wa siku, mjadala wa Mrima Hills haupaswi kuwa tu kuhusu Ruto dhidi ya Gachagua. Ni kuhusu rasilimali ya Kenya, thamani yake halisi, nani ataiendeleza, na Wakenya watapata nini.
 
Kasongo ni kasongo tu kama ilivyo mbuzi ni mbuzi tu
Screenshot_2025-09-09-19-18-23-84.png
 
Back
Top Bottom