RUSSIA na Ugaidi

RUSSIA na Ugaidi

We ulitegemea Russia wawe na usalama kwa level ipi kama rais wao tu ni afisa usalama wa taifa wa zamani? Matukio mengi hua yanagundulika kabla hayajatekelezwa
 
Mkuu Palantir,

Ahsante kwa kunikaribisha kwenye hii mada... have a rough week ndo maana nilishindwa ku-respond mapema!

Niseme jambo moja... am Pro-Russia na inaonekana wengi waliochangia ni pro-Russia kama mimi!

Tofauti ni kwamba, michango ya wenzangu imetawaliwa na ushabiki... I'll refrain from doing that. Nikipata muda, and of course nitapata baadae, nitakuja kueleza kirefu kwanini wale Magaidi wanaoiandama Marekani hawaindami Russia

Lakini kwa kifupi tu ni kwamba, Magaidi hawa hawana sababu za msingi za kuanzisha vita nyingine mpya na mbabe mwingine duniani!

Kwamba wanaogopa, hakuna kitu kama hicho!

Hivi mtu anayeteka ndege na kwenda kujibamiza kwenye jengo anamuogopa vipi mtu ambae hawezi kuwa tayari kufanya hivyo?! Mtu anayejifunga mabomu na kwenda kuripua, anaanzaje kumuogopa mwingine ambae hawezi kuthubutu kufanya hivyo?

Wape magaidi sababu, kesho wapo mlango pako na manyukulia yako!!! Hawa watui ni vichaa...!!! And in fact, sio magaidi tu!! Peleka ukandamizaji wako kwenye foreign nation, siku inayofuata, the very same polite people like Tanzanians, utashangaa wanageuka kuwa monsters wasioogopa mvamizi!!

Endapo hawa watu (tuichukue Waarabu in general) wangekuwa wanaogopa aliyekuzidi maguvu, vijana wadogo wa Kipalestina wasingeenda mstari mbele kupambana na majeshi ya Israel huku wakiwa na mawe mkononi huku wakifahamu kabisa nini kitawakuta!!!

Aidha, tusisahau, Soviet Union ikiwa at full capacity bado haikuwafanya Mujaheedin kuogopa kupambana nao ndani ya Afghanistan!

And trust me, Soviet walikuwa ruthless ambao hawakuona taabu kufanya kinachofanywa hivi sasa na Marekani!

And in fact, hata huko Afghanistan, Soviet walienda kwa staili ile ile ya Kimarekani... wamevamia, wakaua kiongozi aliyekuwa madarakani, wakaweka kibaraka wao lakini bado hilo halikufanya Mujaheedin kuacha kuingia kwenye mapambano na Soviet Union!!

Hapo sijaitaja Chechnya... hata kama Putin aliwafyeka kweli kweli ( second Chechnya war) lakini Russia ilipata damage kubwa sana kutoka kwa Wa-Chechnya And remember, Chechnya ni kisehemu kidogo sana kisichofika hata watu 2 Million over Russia yenye watu zaidi ya 100M.

Sio hivyo tu, ni kikundi kidogo sana cha watu waliokuwa wanafanya hizo vurugu!!

Unawakumbuka au umewahi kuwasikia Shahidka, maarufu kama Black Widows?!

Inasemekana majority ya hawa walikuwa ni Wajane wa wake (wives) wa askari wa Chechnya ambao waliuawa na majeshi ya Urusi!! Hawa Wanawake waliendesha mashambulizi kadhaa ya kigaidi na mengine yakiwa ndani ya Moscow yenyewe huku Putin akiwa ama rais au PM na mashambulizi mengine yakiwa less than 10 years ago!!
 
Miaka ya 2006-10 Russia ilisumbuliwa sana na jimbo lake la Chechnya, kipindi walipotaka kujitenga na dola la Russia, ilibidi Vladimir Putin na Medvedev wajitahidi sana kulinda pride ya warusi.

Kipindi hicho kuna maeneo mengi ya majiji ya Russia kama St. Petersburg na Yekaterinburg yalishambuliwa na "magaidi" toka Chechnya, subways nyingi zilikuwa zinafungwa mara kwa mara kwa sababu ya woga wa kushambuliwa au tetesi za kushambuliwa.

Mwisho Putin aliweka kibaraka wake Chechnya na imebaki hadithi sasa, kusema kweli Chechnya ilisumbua sana Russia.
 
Russia ahangaiki na maisha ya mtu zaidi yake
C kweli Russia ishakuepo middle East kitambo kabla hata ya USA...

nchi mfano Afghanistan Russia ilikueko huko kitambo kabla haijazidiwa influence na USA
 
Mtu katuma comment toka mwaka 2018 unakuja kumjibu leo hii 2020, wala hata ujamjulia hali yake kuwa ni mzima au vp
Daahh we jamaaa banaa....mi sijaona haja kwasababu tuko hapa kuchangia hoja tu...hata atufahamiani so hata ningemjulia hali isingesaidia au hata yy angeweza shangaa
 
Back
Top Bottom