Russia: Magavana 4 wajiuzulu

Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
2,344
1,771
Magavana wa majimbo manne ya nchini Urusi wamejiuzulu jana wakati huu ambao nchi hiyo ikijiandaa kukabiliana na athari za vikwazo vya kiuchumi kutoka katika Nchi za Magharibi, REUTERS wameripoti.

Majimbo yaliyotajwa kujiuzulu kwa Viongozi hao ni pamoja na Tamsk, Saratov, Kirov na Mari El ambapo tayari uchaguzi wa kuwachagua Magavana wapya umepangwa kufanyika Septemba mwaka huu.

Hatua hii inaelezwa kuwa ni ya kawaida kwa nchi ya Urusi kwani mara kadhaa Magavana wasiopendwa au kuonekana kutiliwa shaka wamekuwa wakiondolewa mara kwa mara na hivyo huachia ofisi kwa njia ya kutangaza kujiuzulu.

Wizara ya uchumi ya Urusi imesema kuwa uchumi wa Urusi utapungua kwa asilimia 8.8% katika mwaka huu 2022 kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za magharibi. #MillardAyoUPDATES
 
Kweli hakuna bingwa wa njaa, hata hao wazungu wangekuwa wametawaliwa na makoloni ya weusi toka Africa, hakika usaliti usingeepukika kama ule wa Yuda Iskariote kwa mikataba feki ili matumbo yajitetee, sawa na ilivyo sasa hivi nchi zinazoendelea kama URT
 
Back
Top Bottom