Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Rushwa ya Ngono kwa baadhi ya shule binafsi Mkoani Arusha limeelezwa kushamiri kiasi cha baadhi ya Mashirika yanayojihusisha na utetezi kuingilia kati yakidai wamiliki wa shule hizo wanawakumbatia walimu wao wabaojihusisha na mchezo na mchezo huo kwa watoto wa Mike.
Wakizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni hiyo ya kupinga ukatili wa wanawake na watoto iliyofanyika katika shule ya Msingi Moshono jijini Arusha ,ambayo kilele chake ni disemba 10,2018 ,mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Sasa foundation, Jovita Mlay amesema pamoja na wao kupiga kelele dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kwa mtoto pamoja na rushwa ya ngono lakini bado jamii imekuwa na mwamko mdogo wa kutoa ushirikiano hasa suala la ushahidi linapofikia hatua ya mahakamani.
Katika hatua nyingine amesema kuwa jitihada nyingi zinazofanywa na taasisi yake za kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji lakini bado shule ambazo siyo za serikali haziwachukulii hatua walimu wao wanaowanyia vitendo vya ukatili wanafunzi na kutaka serikali kuzinyooshea kidole shule hizo ili kikomesha vitendo vya rushwa ya ngono.
Baadhi ya wazazi wamepongeza taasisi hiyo ya Sasa kwa kuwapatiwa elimu ya kisheria na sasa wameanza kuwafichua wanaoomba rushwa ya Ngono kwani wanakabiliwa na matatizo mengi hasa majumbani kuna baadhi ya wanawake wananyanyasika sana kutokana na baadhi ya wanaume wao wengine wamekuwa wakiwataka kinyume na maumbile.
Naye kaimu afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha,Denisi mndee amesema wahanga wengi wa matukionya ukatili yapo kwa watoto na wanawake na takwimu za mwaka 2016/17 zinaonyesha kuwa matukio yaliyoripotiwa ni 1437 huku mengi yakiwa ni ubakaji ,mimba za utotoni na shambulio la kudhulu mwili.
"Kutokana na jamii kuanza kuwa na mwamko wa kuyatolea taarifa matukio ya ukatili kwa watoto na wanawake takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa matukio hayo" Amesema
Hata hivyo amesema changamoto kubwa ya matukio yaliyo mengi huwa hayaripotiwi na hivyo kufanya tatizo hilo kuendelea kuwa kubwa .