Rushwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji

mabambase

New Member
Feb 24, 2016
2
0
Kwa amsikitiko makubwa naandika ujumbe huu nikiwa kama kijana niliyejiajiri lakini ndoto zangu za kujiajiri zinaonekana kuzimwa na serikali yetu eidha ni kwa makusudi au kimfumo lakini sioni mwanga tena Zaidi ya giza,mimi ni kijana baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 2008 kwenye fani ya uhandisi niliamua kujiajiri kwa kufungua kampuni yangu ya ujenzi ili niweze kufungua mwanya wa kuajiri na vijana wengine pia.

Nilianza kuendesha kampuni kwa shida na hii ni kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha na miaka 4 baadae mambo yalikaa sawa nikaanza kwenda vizuri kwa kupata miradi mingi sehemu tofauti tofauti hasa MIRADI YA MAJI VIJIJINI chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na serikali ya Tanzania.

Mwaka 2014 kampuni yangu ilipata takribani miradi mine ya maji vijijini yenye thamani ya Zaidi ya Tsh 2.8 bilioni tulianza kazi vizuri hku tukilipwa kwa wakati,tatizo lilianza mwishoni mwa mwaka 2014 baada ya Sakata la Escrow kuibuliwa bungeni na hivyo wafadhili wa miradi hii walisitisha ufadhili wao kwenye miradi hii ya maji vijijini ambayo kwa kiasi kikubwa ilkuwa kwa ufadhili wa bank ya dunia na serikali yetu kwa kiasi kidogo.

Mateso yalianzia hapo tangu Januari 2015 hadi leo serikali haikuweza tena kutulipa madeni yetu na hivyo kupelekea miradi yetu yote kusimama huku tukiwa na madeni kwenye taasisi mbalimbali za fedha,kampuni yangu imeajiri wahandisi wenye shahada watano mafundi wenye ujuzi mbalimbali kumi na mbili.

Madereva sita watu wasio na ujuzi ambao walikuwa wanafanya kazi za kutumia nguvu kama kuchimba mitaro,kubeba zege, tofali au mchanga kama 200 kwa site zote hali yetu kimaisha imekuwa ngumu sana tangu kipindi hicho hadi hivi leo ninavyoandika ujumbe huu mimi kama Mkurugenzi wa kampuni nimeishi kwa stress kubwa kuna wakati huko Shinyanga.

Nimefikishwa kwa mkuu wa Wilaya na mahakama ya mwanzo kwa wale wanaonodai lakini tulijitahidi kwa kadiri tulivyoweza kupunguza madeni kilichonifanya kuandika uzi huu ni RUSHWA ya waziwazi inayoendelea wizara ya maji kwa sisi wakandarasi tuliofanya miradi ya maji ambao hatujalipwa pesa zetu na miradi yetu imesimama hadi leo.

Wakati wa kufunga bunge waziri wa maji alijigamba wanakwenda kulipa makandarasi wa miradi ya maji ili kazi zilizosimama zimalizike nchi nzima,cha kusikitisha hakuna kilichofanyika na si waziri,naibu wala katibu wa wizara aliyewahi kulitolea ufafanuzi suala hili ili tujue tutalipwa lini.

Mchezo uliopo kwa sasa ni kwamba wizara ya maji ina fedha ambazo zinatakiwa kutumwa halmashauri kulipa wakandarasi wanaodai na ili pesa itumwe kwenye halmashauri unayodai wewe mkandarasi ukipata mtu pale wizarani akakuunganisha na wakubwa watakuuliza UNATUACHA ACHAJE ukiweza kuwahahakikishia kwamba kwenye hayo malipo kuna chao pesa inatumwa kwenye halmashauri unayodai ikiwa na barua ya maelekezo ulipwe wewe muhusika uliyeelewana nao,tofauti na ilivyokuwa awali pesa inayotumwa ilikuwa ikigawanywa kwa wote mnaodai.

Hii imetuvunja moyo sana sisi vijana wadogo tuliojiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana wenzetu na hatuna namna ya kufanya maana hatuna ndugu zetu IKULU wala WIZARA YA MAJI ila tunachosema ni kwamba Biblia inasema haki huinua Taifa kama kwenye taifa hakuna haki hata ustawi wake ni mdogo sisi tusio na ndugu ikulu au wizarani wa kutuandikia memo ili tulipwe tutaendelea KUPIGA MAGOTI NA KUMLILIA MUNGU maana yeye hapokei rushwa.

Yeye ni wa haki na yeye atatutetea ili haki itendeke na tunaamini machozi yetu hayatakwenda bure,sambaza ujumbe huu kwenye mitandao ya kijamii labda utawafikia wahusika maaana sisi wanyonge hatuna namna ya kufikisha ujumbe kwa wakubwa hawa Zaidi ya mitandao yetu hii ya kinyonge.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Halmashauri ni tatizo. ...na wizara nyingine pia zina matatizo. Solution ya tatizo lak ni nini?
 
Pole ndugu,
Kufanya kazi za halmashauri ni janga kubwa, mwaka juzi nilipata kazi za halmashauri katika wilaya 4 tofauti, kazi zilipokamilika tatizo likawa jinsi ya kupata malipo kwa kazi tulizokamilisha, tuliambiwa tusubiri pesa ziingie kutoka serikali kuu kipindi hicho serikali likuwa inatuma pesa au inaagiza halimashauri zitumie pesa zao za ndani ambazo kwa baadhi ya wilaya pesa hizo ni kama hazipo.
Mwaka jana wakati tunaendelea kusubiri malipo yetu, serikali ikatoa agizo kuwa kila wilaya kuhakikisha kila shule ya sekondari imejenga baabara ya kisasa kwa kutumia pesa za ndani ya halmashauri, na mkurugenzi yeyote wa wilaya ambaye angekiuka agizo hilo atakuwa amejifukuzisha kazi, huo ukawa ni mkwamo mwingine mpya.
Mwaka jana huo huo wakati tunafukuzia malipo yetu tukaambiwa kuwa serikali imetumia pesa yake yote kwenye uchaguzi mkuu, tuendelee kusubiria.
Mwaka huu tukiwa na serikali mpya, tukaambiwa kwa sasa serikali imeanza kukusanya kodi kwa nguvu kubwa na kuvuka malengo, pamoja na jitihada hizo bado hatujalipwa na hatujui ni lini tutalipwa.
Mwaka jana nilifunga kampuni kwa muda, sababu ya madeni, baada ya kupata kazi hizo za halmashauri nilichukuwa pesa za bank kama mtaji wa kazi, ili miradi niliyopewa imalizike kwa muda uliotakiwa, nikabaki ninadaiwa pesa za bank pamoja na riba, nimeuza shamba na nyumba kurudisha pesa ya bank na kulipa wafanyakazi nikisubiria malipo yasiyoeleweka serikali hii italipa lini?
 
Back
Top Bottom