Rushwa traffic imekithiri

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,778
2,298
Leo nilikuwa abiria nikielekea mlandizi. Kufika Kibaha eneo la loliondo kuna askari alitusimamisha. Dereva akamwambia konda wake, kamalizane naye. Akafika dogo kapewa mshiko tukaondoka. Kwanini alitusimamisha?
 
Leo nilikuwa abiria nikielekea mlandizi. Kufika Kibaha eneo la loliondo kuna askari alitusimamisha. Dereva akamwambia konda wake, kamalizane naye. Akafika dogo kapewa mshiko tukaondoka. Kwanini alitusimamisha?
Kwa nn usingekataaa kutoa rushwaa,kwani amekuomba au ww tu ukaona umpe ili usilipe faini, kua mzalendo lipa faini.
 
Mbona mnapenda kuwaona sana polisi wetu, kila kitu polisi, JW mnawaogopa, I wish I could be IGP by sizonje voice
 
Mimi huwa nafiki wananchi wenyewe ndio wanawashawishi hao askari wa barabarani kupokea mlungula. Ukitaka usitoe mlungula hakikisha huvunji sheria za barabarani na gari lako lipo salama na lina vibali vyote husika. Sasa kama unaona askari anakuchomekea kosa lazima na wewe ujue haki zako na si kumtuliza kwa kumpatia kitu kidogo. Kawaida hawa askari huwa hawaombi hizo rushwa ila mkosaji au anaejihisi mkosaji ndio huanza kumshawishi askari apokee rushwa (askari hana allergy na cash atapokea tu). Na ujue MFANO: ukimpa rushwa askari ukiwa Kibaha wakati unaenda Morogoro kwa road licence imepitwa na muda, ujue Mlandege utatoa rushwa nyingine, Chalinze utaendeleza rushwa nk. Abiria huwa hatujui hayo tumekuwa tukilalama tu.. lakini wote ni wakosaji. Kama hutatoa rushwa hakuna atakae pokea rushwa.
 
Back
Top Bottom